Maneno Ya Pongezi

(Commendations)

 

Niliposoma kitabu kipya cha Ndugu Bernie Koerselman kiitwacho Uasi Ndani Ya Kanisa, niliguswa sana na ujumbe wake muhimu kuhusu nafasi ya Yesu Kristo kama Bwana. Bernie, kwa njia iliyo wazi kabisa japo kwa kifupi, amefunua kosa kubwa sana kiitikadi lililomo kanisani siku za leo. Mimi kama mchungaji, mwalimu na mishenari tangu miaka ya 1970 katikati, nimeona bayana uharibifu ambao umefanyika kanisani kutokana na fundisho hili ambalo si sahihi. Usipoteze nafasi yako ya kushambulia na kuangusha ngome za mafundisho ya uongo katika eneo lako la utendaji! Soma hiki kitabu – Uasi Ndani Ya Kanisa – na ukitumie chombo hiki muhimu sana kuwafikia wengine kwa ujumbe wenye kuweka huru ambao ni Habari Njema za Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo.

 

Chuck King

Mtumishi Mwenzi

 

Ndugu Bernie Koerselman ameandika kitabu kifupi lakini kilichokamilika kabisa, ambacho ingekuwa mapenzi yangu, kingekuwa kitabu cha kiada katika kila Shule ya Biblia duniani. Kwa njia hiyo, watumishi vijana wangepata msingi mzuri ambao juu yake wangejenga kwa muda wote wa huduma zao. Vile vile ninatamani kwamba kila mchungaji aliyeko kazini wakati huu na kila mwinjilisti asome kitabu hiki Uasi Ndani Ya Kanisa. Kingebadilisha huduma nyingi sana na kuanzisha uamsho. Ndiyo sababu huduma yetu inafanya kazi kwa bidii sana kuona kitabu hiki kikifasiriwa katika lugha nyingi na kugawanywa kwa viongozi wa Kikristo duniani kote. Tunatumaini kwamba kitasomwa na mamilioni.

 

David Servant

Mkurugenzi, Huduma ya Heaven’s Family

 

Ndugu Bernie Koerselman amegusa panapohusika kabisa kwa kitabu hiki. Mimi nimekuwa rais wa huduma ya uinjilisti gerezani na mtaani kwa miaka thelathini na tatu. Kanisa la Marekani limejaribu kila kitu ili uamsho uje – na limeshindwa. Limevaa vito vya thamani vinavyosema “Je, Yesu angefanya nini?”, limekimbizana na miujiza na ishara bandia, limetumia mbinu za kidunia za kuuza vitu, lakini yote hayo yamezaa Wakristo bandia, au walio dhaifu sana. Neno la mwisho la Yesu kwa kanisa Lake lilikuwa, “Tubuni”. Watu wengi hawajui vizuri yale Yesu aliyowaambia wafuasi Wake waamini na kutenda. Kitabu hiki kinaweka hayo yote wazi kabisa.

 

Tom Adcock

Kituo cha Habari cha Watu wa Yesu (Jesus People Information Center)

Sacramento, CALIFORNIA, Marekani

 

“Tunaishi katika siku za hatari, siku za kurudi nyuma, ambapo mamilioni ya waongofu bandia huketi katika Kanisa kama magugu katikati ya ngano, kwa sababu hawajawahi kukabiliwa na Injili ya KiBiblia. Baadhi ya hawa waongofu bandia wamefanikiwa kuingia katika madhabahu na kuwa wahubiri maarufu. Wengine wameshika nyadhifa za juu katika mashirika ya uchapishaji vitabu ya Kikristo, na wengine ni mameneja kwenye maduka ya vitabu ya Kikristo. Hii ndiyo sababu mafundisho ya uongo yamekuwa na ushawishi mkubwa na kukubalika bila kuchambuliwa sana katika Kanisa la kisasa. Namshukuru Mungu sana kwa ajili ya watu kama Ndugu Bernie Koerselman na kitabu chake – Uasi Ndani Ya Kanisa. Namwomba Mungu akitumie kitabu hiki kufungua macho ya vipofu.”

 

Ray Comfort

Mwandishi na Mtangazaji Mwenza wa “Njia Ya Bwana” (“The Way Of The Master”)

 

Hiki ni kitabu kizuri sana, chenye kushughulikia mada hatari sana iliyopo. Ni ukweli. Zaburi ya 11:3 inasema, “Kama misingi inaangamizwa, wenye haki wafanye nini?” Ninakupa changamoto wewe kama msomaji – futilia mbali mawazo yako uliyokuwa umekwisha jenga na ukipokee kitabu hiki bila ya ubaguzi. Kitabadilisha msingi wako wa kufikiri. Mimi binafsi ninajionea mada za kitabu hiki zikibadilisha kusanyiko la watu ambao Mungu ameniita kuwaongoza.

 

Trent Renner

Mchungaji, Parkway

 

Katika nyakati hizi tunazoishi, mimbari na viti katika madhehebu mengi vimejazwa na watu wa uvugu-vugu ambao wanapenda kujifanya watu wa dini, lakini wenye kukana nguvu ambazo zingeweza kuwafanya watauwa (2Tim. 3:5). Hii ni dhambi inayopuuzwa hata na baadhi ya watu ambao wamejitoa kweli kukubali kwamba Kristo ni Bwana. Bwana amemhimiza Ndugu Bernie kuandika ujumbe huu wenye nguvu, wa kipekee na wenye kushawishi ili kuwashtua viongozi vipofu wa watu vipofu, na wafuasi vipofu wa viongozi vipofu, na pia kupata usikivu na ushirikiano wa maombi kutoka kwa wale ambao wamezaliwa mara ya pili kweli na ambao wanaishi maisha yenye kumpa Kristo nafasi muhimu. Naomba matokeo ya kitabu hiki yawe ni kuzaliwa kwa makanisa yasiyo na idadi, yenye kufanya watu kuwa wanafunzi.

 

Joe Simmons

Mkurugenzi Mstaafu Wa Huduma Ya Navigators, Kanda ya Pacific

 

Ndugu Bernie anathibitisha kutoka Maandiko kwamba, yeyote anayedai kuwa amesamehewa na Mungu dhambi zake kwa kukiri kumpokea Yesu Kristo kama Mwokozi wake binafsi na haonyeshi shauku wala haja ya kumfuata huyo Mwokozi na kumpa nafasi kama Bwana, anadai kitu bandia. Bila ya kuonyesha shauku halisi na uamuzi wa kumruhusu Yesu kuwa Bwana katika maisha kamili ya mtu binafsi, ukiri kwamba mtu kampokea Yesu kama Mwokozi hautasimama mbele Zake Yeye ambaye lazima sote tutoe hesabu yetu mbele Yake. Matokeo hayo ni janga kubwa, lenye matokeo ya milele. Kitabu cha Ndugu Bernie kinaweka jambo hili wazi kabisa, kwa msingi wa Maandiko.

                                                                                             

Ndugu Bernie, kwa uwazi na ustadi kabisa, amefunua fundisho potofu lililo kuu katika kanisa la siku hizi. Tumia kitabu hiki – Uasi Ndani Ya Kanisa – ili kuwafikia wengine kwa ujumbe wa Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo.

 

Harvey Hoekstra

Mwanzilishi wa huduma ya Audio Scriptures International

Mishenari, Afrika

 

Hiki ni kitabu kilichotakiwa kuandikwa. Na Ndugu Bernie Koerselman, msomi makini wa Biblia na mchunguzi wa tamaduni zetu na Kanisa ndiye mtu anayefaa kufanya hivyo. Ingawa kuna sehemu sehemu za uhai wa kiroho wenye nguvu na uwezo katika Kanisa la siku hizi, kwa sehemu kubwa, Kanisa katika karne hii ya Ishirini na Moja limezorota na kupoa. Kulikoni? Ndugu Bernie amegusa mahali ambapo ndiyo mzizi wa hilo.

 

Kusoma kitabu hiki kutakuhimiza na kukutia moyo.

 

Cecil Martens

Mchungaji

 

Mwandishi huyu, ambaye amesomea hesabu, sayansi na sheria, ameandika kitabu chenye usahihi na kilichokamilika, kama ambavyo ingetazamiwa. Nilikutana na Ndugu Bernie Koerselman mara kadhaa wakati nikikaa New Zealand – mwaka wa 1992 hadi 2000 – kabla ya kurudi kwangu Brisbane, Australia. Hii ni pamoja na wakati mmoja ambapo alikuja kunisikiliza nikihubiri huko mjini Christchurch. Vile vile nilichapisha baadhi ya maandiko yake katika gazeti letu la kimataifa liitwalo Contending EARNESTLY for THE Faith (CETF). Katika kitabu hiki Uasi Ndani Ya Kanisa, anaanzia mahali ambapo sote tunapaswa kuanzia – hali yetu ya moyo kuhusu  Neno la Mungu – “Uasi huanza wakati tunapoacha kuamini kwamba Biblia ni kweli.” Dibaji yake inasema kile ambacho kimekuwa msimamo wangu kwa muda mrefu – Biblia imevuviwa kabisa na Mungu, lakini uvuvio huo huonekana vizuri zaidi na kwa ubora zaidi katika Kristo. Halafu, katika kurasa zinazofuata kuanzia sura ya kwanza – Uasi Dhidi ya Yesu kama Bwana – hadi sura ya pili – Uasi Dhidi ya maneno ya Yesu – na katika sura ya Kumi na Moja – Tubu, Badilika Na Ufundishe – anaendeleza na kufafanua zaidi mada yake. Ndugu Bernie yuko sahihi. Kaa tayari kupokea changamoto. Unaweza kukosolewa isivyostahili kwamba unafundisha Injili ya matendo kutokana na kufanyia kazi mafundisho haya ya Ndugu Bernie, kwamba Kristo ni Bwana. Paulo aliomba hivi: “Bwana, unataka mimi nifanye nini?” (ktk Mdo. 9:6). Kutii UBwana wa Kristo ilikuwa alama ya kuokoka kwake, na ndivyo inavyotakiwa na kwetu pia.

 

Philip Powell

Mkurugenzi, Huduma ya Christian Witness Ministries (CWM)

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

UASI ndani ya Kanisa

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Vingine Vilivyoandikwa na Ndugu Bernie Koerselman

Vinapatikana

www.bereanpublishers.com

 

Kitabu: Imani Yenye Kuokoa (kwa Kiswahili)

 

Somo La Biblia: Mafundisho na Amri za Yesu (Kiingereza)

 

Makala:

(Zote Hizi Ni Kwa Kiingereza)

 

Imani Yenye Kuokoa – Ni Nini?

Injili Ni Nini?

Sura Nyingi Za Imani Yenye Kuokoa

Yesu Lazima Awe Bwana!

Fanya Mapenzi Ya Mungu

Lazima Wakristo Wawe Wenye Haki

Kufananishwa Na Mfano Wake

Kaa Ndani Ya Yesu

Jinsi Mungu Anavyoiona Dhambi

Lazima Uzaliwe Mara Ya Pili

Torati Ya Musa Au Sheria Ya Kristo

Jipimeni Wenyewe!

Mwaminini Yeye

Yesu Ni Bwana

Kutii: Alama Ya Mkristo (Wa Kweli)

Kutii: Ushahidi Wa Imani Yenye Kuokoa

Matendo Mema: Ushahidi Wa Imani Yenye Kuokoa

Matunda: Ushahidi Wa Imani Yenye Kuokoa

Maswali Muhimu Sana

Ulaghai Katika Kuihubiri Injili

Udanganyifu Katika Kuihubiri Injili

Kusikiliza

Barua Ya Wazi Kwa Wachungaji

Bwana “Wetu”

Je, Mkristo Anatii Sheria Gani?

Sabato, Jumapili, Au …

Je, Kutenda Dhambi Kunaweza Kumpotezea Mtu Wokovu?

Kutazama Tena Warumi Sura Ya Saba

Je, Wakristo Wanaweza Kuachana? (Na Kuwa Na Ndoa Nyingine?)

Je, Wakristo Ni Wenye Dhambi Au Watakatifu?

Je, Wakristo WAMWOGOPE Mungu?

Maandiko Muhimu Sana Ni Mekundu

Kila Kitu Kinaruhusiwa Kwangu

Mungu Huwaletaje Watu Kwa Yesu?

Utatu

Dhamana Yenye Kutuhakikisha Urithi Wetu

Barua Yenye Kupinga Mapatano Ya Madhehebu:

“Wanaoamini Injili Na Wakatoliki Wakiwa Pamoja; Utume Wa Ukristo Katika Miaka Elfu Moja Ya Tatu”

Dhiki Kuu, Unyakuo Na Ghadhabu Ya Mungu Ya Mwisho

Sabato Ya Miaka Elfu?

Kutimizwa Kwa Ufunuo 12:1-4

Je, Aaminiye Yuko Salama Milele?

Wakristo Husamehewa Lini?

Je, Upendo Wa Mungu Hauna Masharti?

Vithibitisho Vya Wokovu Wenye Masharti

Kujua Kabla Au Kuchaguliwa Kabla

Kujua Kabla: Yakobo Na Esau

Fundisho La Kuchaguliwa Kabla

Kuhusu Imani Ya Branham

Itikio La Ugaidi (Mtazamo Wa Kikristo)

Wakati Wa Ukweli

Yesu Kristo: Huyu Ni Nani?

 

[ANGALIZO LA MFASIRI: Katika kitabu hiki, vitabu vyote na makala zote ambavyo havipatikani na havimo katika Kiswahili vitaonyeshwa kwa majina yake ya Kiingereza, au kama majina yakitafsiriwa, itawekwa wazi kwamba havipatikani kwa Kiswahili. Hata majina ya tovuti yataachwa hivyo hivyo kwa sababu si za Kiswahili.]

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

UASI

 

NDANI YA

 

KANISA

 

 

 

 

Kimeandikwa Na

 

Bernard Koerselman

 

Kimefasiriwa Na

 

Mchungaji Simon Joel Vomo

 

Berean Publishers

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Uasi

Ndani Ya Kanisa

 

Chapisho la Kwanza Kwa Kiingereza: Julai 2008

 

© 2008 – na Bernard Koerselman, J.D.

 

Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu yoyote ya kitabu hiki inayoruhusiwa kunakiliwa kwa namna yoyote ile bila ruhusa ya mchapishaji, isipokuwa sehemu fupi fupi kwa madhumuni ya uchambuzi wa kitabu.

 

Maandiko yote ya Biblia yanayotumiwa humu yanatoka katika Biblia ya Kiswahili, Union Version, isipokuwa kama ikionyeshwa vinginevyo.

 

ISBN:  978 – 0 – 941879 – 07 – 1

 

Jalada Limeandaliwa na: CJ McDaniel

Kitabu Kimefasiriwa na: Mch. Simon Joel Vomo

 

 

Kitabu Kimetolewa na:

 

Berean Publishers

Anwani ya Barua Pepe kwa ajili ya Kuagiza Vitabu: editors@bereanpublishers.com

Anwani ya Barua Pepe ya Mwandishi: b.koerselman@bereanpublishers.com

Tovuti: http:// www.bereanpublishers.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kwa Heshima Ya Maria Duran

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Yaliyomo

 

Maneno Ya Kuanza

(Prologue)

 

Dibaji

(Preface)

 

Utangulizi

(Introduction)

 

1. Uasi Dhidi Ya Yesu Kama Bwana

(Rebellion Against Jesus As Lord)

 

2. Uasi Dhidi Ya Maneno Ya Yesu

(Rebellion Against Jesus’ Words)

 

3. Uasi Mkuu Wawekwa Wazi

(The Great Rebellion Exposed)

 

4. Je, Viongozi Wa Kanisa Watahukumiwa?

(Will Church Leaders Be Condemned?)

 

5. Uasi Dhidi Ya Sheria Ya Kristo

(Rebellion Against the Law Of Christ)

 

6. Mtoto Wa Kupinga Sheria: Usalama Milele Usio Na Masharti

(A Child Of Antinomianism: Unconditional Eternal Security)

 

7. Mtoto Mwingine Wa Kupinga Sheria: Ulaghai Katika Kuhubiri Injili

(Another Child Of Antinomianism: Fraud In The Presentation Of The Gospel)

 

8. Mtoto Mwingine Wa Kupinga Sheria: Udanganyifu Katika Kuhubiri Injili

(Another Child Of Antinomianism: Deceit In The Presentation Of The Gospel)

 

9. Tafuteni Kwanza … Haki Yake

(Seek First … His Righteousness)

 

10. Maneno Yaliyozoeleka, Yanayosemwa Kupinga Haki

(Popular Anti-Righteousness Expressions)

 

11. Tubu, Badilika, na Ufundishe!

(Repent, Change, and Teach!)

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Maneno Ya Mwanzo

(Prologue)

 

Wakati Ndugu David Kirkwood alipoandika kitabu chake kiitwacho Mtumishi Anayefanya Watu Kuwa Wanafunzi, chenye kusisimua sana, alijitahidi kueleza anawaandikia akina nani. Alisema wazi kabisa kwamba alikuwa anawaandikia viongozi wa kanisa, lakini hasa wale wanaoishi nje ya Marekani, Ulaya Magharibi na Australia/New Zealand. Japo alisema kwamba yawezekana watu wote kila mahali wakafaidika na kitabu chake, alijua kwamba wasomaji ambao wangefaidika zaidi ni wale walio katika mataifa ambayo si ya Magharibi.

 

Mimi nimekuwa nikijali sana kanisa la nchi za Magharibi – kwanza la Marekani, na baadaye, la New Zealand. Bado ninajali sana, pengine kwa sababu ninajua vizuri sana hali halisi ya kanisa katika nchi hizo mbili. Wale wa mataifa ya dunia ya tatu wanaweza pia kufaidika na kitabu hiki kwa sababu, kanisa la nchi za Magharibi limepeleka uasi wake duniani kote. Kanisa la nchi za Magharibi lilidai kuwapelekea Injili, lakini kwa kiasi fulani limepeleka injili nyingine – si ile ya Biblia ya Bwana wetu Yesu.

 

Kama ambavyo Ndugu David Kirkwood anavyoamini kwamba viongozi wa kanisa wangeweza kufaidika kutokana na kitabu chake – yaani wachungaji, wainjilisti, waalimu, wamishenari, waanzisha makanisa, manabii, watenda kazi katika Shule za Jumapili na viongozi wengine – mimi pia ninalenga kitabu changu kwa watu hao. Ninakiri kwamba ninajisikia kama Yeremia, aliyeambiwa na Mungu kusema neno la Mungu kwa kizazi ambacho kingeyakataa maneno yake. Viongozi wa kanisa ndiyo wenye kumwasi Mungu na kuliasi Neno Lake, nao si rahisi kubadilika. Kutokana na ujuzi nilio nao wa kusema nao, wamezama katika njia zao. Wanaamini kwamba wanajua zaidi na hawako tayari kubadilika.

 

Nadhani kitabu hiki kitakuwa na nguvu sana miongoni mwa washirika wa kawaida kanisani (walei) ambao wanamtafuta Mungu kwa dhati kabisa, japo wanajua rohoni mwao kwamba kuna kitu kisicho sahihi katika mambo wanayofundishwa, ila hawana uhakika ni kwa nini, au kosa ni nini. Kitabu hiki kitafunua kwamba wamesalitiwa na viongozi ambao wanamwasi Mungu.

 

Ninaamini kwamba wengi katika kanisa ambao wanamwasi Mungu na Neno Lake ni matokeo ya mapokeo ya kanisa ambayo mimi nayaita “Ukanisa”, kitu ambacho ni kinyume na Ukristo. Kwanza, hii injili tofauti imeingia katika vyuo vikuu vya Ukristo, halafu ikaingia katika mimbari, na hatimaye ndani ya kanisa. Kama isipopingwa, injili hii ya uongo itaendelea kuzuia wokovu kwa mamilioni wanaoikubali bila ya kuichambua.

 

Yesu aliwaonya wale mabingwa wa Torati, hivi: “Ole wenu ninyi mabingwa wa Torati, kwa sababu mmeondoa ufunguo wa maarifa. Ninyi wenyewe hamjaingia, na mmewazuia wale waliokuwa wanaingia” (ktk Luka 11:52, TLR). “Mabingwa wa Torati” wa siku za leo ni wachungaji waliohitimu katika vyuo vikuu vya Ukristo. Wengi wao wanakataa kutoa ufunguo wa maarifa kwa wale wanaowahudumia. Hawajifunza na kutii wao wenyewe, na wanazuia kweli ya Maandiko kuwafikia wengine. Utaelewa vizuri zaidi kadiri tunavyoendelea. Mambo ni yale yale yaliyokuwa katika siku za Yesu. Mabingwa wa siku za leo wanawazuia wale wenye kuingia. Injili yao ya uongo itawanyima wokovu mamilioni.

 

Ni kama tunaishi katika wakati ule uliotabiriwa na Mungu katika Amosi 8:11, kwamba, “’Siku zinakuja,’ asema Bwana Mwenyezi, ‘ambapo nitatuma njaa katika nchi – si njaa ya chakula au kiu ya maji, bali njaa ya kusikia maneno ya BWANA’.” (TLR) Andiko hili litakuwa wazi zaidi kadiri tunavyoendelea.

 

Nimesema katika kitabu hiki kwamba “mamilioni” ya watu watanyimwa wokovu kwa sababu ya injili ya uongo ambayo inatangazwa na wale wanaomwasi Mungu. Ingawa idadi hiyo haina uthibitisho kiutafiti, inatumika kueleza idadi kubwa ya watu ambao watanyimwa wokovu. Yaani, utakapoelewa vizuri dhana ya kitabu hiki, pengine utatumia “makumi ya mamilioni” kusema kuhusu idadi ya watu unaoamini kwamba wananyimwa wokovu na injili hii ya uongo.

 

Kitabu hiki kitaonyesha tofauti iliyoko kati ya Injili ya KiBiblia ya Bwana Yesu Kristo, na ile injili ya uongo ambayo inahubiriwa sana siku hizi. Injili ya KiBiblia ndiyo chanzo cha uzima wa milele. Hii nyingine ni bandia tu iliyotengenezwa na mwanadamu zamani na kukubalika na kukuzwa na kuendelezwa na vizazi vilivyofuata. Ni Injili itakayoendelea kuwaongoza mamilioni wasiohesabika kutengwa na Mungu na hatimaye kuangamia milele.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Dibaji

(Preface)

 

Tunapoanza, hebu tuweke msingi wa kukubaliana. Hapa tutawapoteza baadhi ya watu kwa sababu wengi hawatakubaliana na yafuatayo. Inasemekana kwa uhakika sana kwamba baadhi ya watumishi hawaamini kwamba Biblia inamaanisha inachosema. Wengine wanakataa kwamba Yesu si Mungu, na hakuzaliwa na bikira. Wengine wanakana miujiza ya Biblia, na wengine wanakataa habari za uumbaji katika Biblia. Orodha hii ni ndefu, sawa tu na itikadi zilizotokana na hali hiyo ya moyo wa kuchanganyikiwa na kutokuamini Maandiko.

 

Kama Biblia ni kweli – kama ni Neno la Mungu – basi tunapaswa kuiheshimu na kutafuta kutii amri zake. Lakini kwa wale wanaodai kwamba Biblia si kweli, au si ya kweli kikamilifu, wanatengeneza UKanisa wao. Watu kama hao wanaeneza dini ya mwanadamu, ambayo ndani yake wanaokota na kuchagua kile watakachoamini na watakachohubiri na kukifundisha.

 

Kama wewe uko miongoni mwa kundi lile lisilohesabu Biblia kuwa ni Neno la Mungu na hukubali kuruhusu akili yako ishawishiwe na kweli ambazo ziko kinyume na unavyoamini kwa sasa, basi usihangaike kuendelea kusoma. Wale wasiokubali Maandiko kama yalivyo, lakini wataendelea kusoma kitabu hiki watafika mahali watambue kwamba wamekwisha jihifadhia nafasi katika mahali pale ambapo Yesu alipaita nje katika giza, ambapo kitakuwepo kilio na kusaga meno – mahali penye moto uwakao utakaowateketeza maadui wa Mungu. Angalia Waebrania 10:26.

 

Baada ya kusema hayo, ni muhimu kuweka LAKINI. Kwa kuwa Maandiko yote yametolewa na Mungu kwa njia ya uvuvio haimaanishi kwamba Maandiko yote yanatumika kwa namna moja na Wakristo wote waaminio. Tutashughulikia hili katika sura nyingine. Mafundisho mengi ya uongo yametokana na kushindwa kuelewa ni Maandiko gani ambayo Mkristo mwamini anapaswa kutii.

 

Ukweli wa Maandiko unaweza kuthibitishwa kwa njia ya unabii unaomhusu Yesu. Wengi wanasema kwamba kuna zaidi ya unabii 300 katika Agano la Kale unaomhusu Masiya – Mpakwa Mafuta – aliyekuwa aje. Wakati Yesu alipokuja, alitimiza unabii wote ambao alitakiwa kutimiza katika ujio Wake wa kwanza.

 

Ndugu Josh McDowell aliandika juu ya utafiti uliofanywa na Peter Stoner na kuchapiswa katika jarida liitwalo Science Speaks, katika kitabu chake kiitwacho Evidence That Demands A Verdict. Bwana Stoner alichambua nane tu katika tabiri nyingi sana zinazomhusu Kristo – kwamba angezaliwa Betlehemu, kwamba angetanguliwa na mjumbe, kwamba angeingia Yerusalemu akiwa amepanda punda, kwamba angesalitiwa na rafiki, kwamba angesalitiwa kwa vipande 30 vya fedha, kwamba fedha hiyo ingetupwa katika nyumba ya Mungu halafu itumike kununua Konde la mfinyanzi, kwamba angenyamaza kimya mbele ya washtaki Wake, na kwamba angetobolewa mikono na miguu na kusulubiwa. Kulingana na sayansi inayochunguza uwezekano wa mambo, kwamba mtu yeyote angeweza kutimiza hizo tabiri nane tu ni kitu kinachowezekana mara 1 katika nafasi 100,000,000,000,000,000.

 

Bwana Stoner alifafanua ukubwa wa namba hiyo kwa njia hii: Tuseme kwamba tumechukua sarafu za shilingi 200 za Kitanzania 100,000,000,000,000,000 na kuzitandika chini juu ya Tanzania. Kiasi hicho cha sarafu kingefunika nchi ya Tanzania na kufikia kimo cha futi mbili. Sasa, chukua sarafu moja uitie alama, kisha uichanganye ndani ya hizo zingine. Mfunge mtu kitambaa machoni na umwambie ana uhuru wa kusafiri popote katika nchi ya Tanzania ili aokote sarafu moja tu. Je, atakuwa na uwezekano gani wa kuiokota ile iliyotiwa alama? Ndiyo hivyo kwamba, mtu yeyote angeweza kutimiliza zile tabiri zote nane, kwa kubahatisha tu. Yesu, si kwamba alitimiza hizo zote nane, bali pia na zingine zote zilizokuwa zinamhusu Kristo, isipokuwa zile ambazo zitatimizwa wakati wa kuja Kwake mara ya pili. Bwana Stoner aliona kwamba, uwezekano wa Yesu kutimiza hizo tabiri zote 48 ni nafasi 1 katika 10157  - idadi ambayo ni kubwa sana, na uwezekano ambao pengine hata akili haiwezi kuelewa.

 

Sasa hebu tafakari kwamba kuna kitabu kimoja, tena kimoja tu – Biblia – chenye unabii huo. Kwa njia ya unabii wake, Biblia inamtaja kwa usahihi kabisa yule mtu wa kipekee aliyetimiza tabiri hizo zote kuhusu Kristo. Tena, kimefanya hivyo kwa njia ya waandishi wengi tofauti, katika kipindi cha mamia ya miaka. Hivi kwa mawazo yako, inawezekanaje kwa kitabu kimoja tu kubahatisha kuwa na tabiri nyingi kiasi hicho ambazo hata Wayahudi waliziamini, zinazomhusu Masiya wao anayekuja? Halafu, zote zitimizwe na mtu m moja? Uwezekano huo ni sawa na kudhani kwamba mtu mmoja anaweza kwa bahati tu kutimiza tabiri hizo zote.

 

Wakati wa Yesu na kwa karne nyingi kabla ya hapo, Wayahudi waliamini hizo tabiri zote, kwamba zilikuwa zinahusu Masiya wao ajaye. Katika Injili, kuna sehemu nyingi zinazotajwa kuonyesha jinsi Yesu alivyotimiza unabii wa Agano la Kale kuhusu Kristo.

 

Shahada yangu ya kwanza ni katika hesabu ya sayansi. Uwezekano wa huo unabii kutimizwa kwa bahati ni kitu kinachoshangaza sana. Kwamba mtu mmoja alitimiza unabii huo wote ni kitu kisichoeleweka kama si Yeye. Ushahidi huo wote unanifanya nijione mjinga kabisa kama nisingeamini. Halafu, nilikuwa wakili, na katika fani hiyo nilikuwa natafuta ushahidi na kuutoa ili niwe na msingi wa kusimamia katika kesi nilizotetea. Siwezi kufikiria ushahidi wenye nguvu zaidi kuthibitisha kwamba Biblia ni kweli na kwamba Yesu ndiye Kristo, kuliko yale ambayo umesoma mpaka sasa. Ni ushahidi ambao hauwezi kutiliwa shaka.

 

Bado kuna ushahidi mwingine zaidi wenye kuthibitisha Yesu ni nani. Yesu alichagua mitume kumi na mbili. Yule aliyemsaliti alitambua kwamba amefanya kosa, akajiua. Lakini tunaambiwa kwamba, wale wengine wote isipokuwa Yohana waliuawa kwa sababu walihubiri kwamba Yesu alikuwa ndiye Bwana Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, aliyekufa msalabani lakini akafufuka kutoka kwa wafu. Bila shaka wangeweza kujiokoa wenyewe kwa kukana tu ushuhuda wao au kwa kutoweka na kunyama kimya, na kuacha kuendelea kutangaza kwamba Yesu ni nani. Msema kweli ni wakati unapokabiliwa na kifo. Watu wachache sana watakubali kufa kwa ajili ya kitu wanachojua si kweli. Lakini, hakuna hata mtume mmoja aliyekana ushuhuda wake. Kinyume chake, walichagua kufa kuliko kumkana Bwana Yesu na kile walichojua kuwa ni kweli juu Yake.

 

Uasi huanza wakati Biblia inapoonekana kuwa si ya kweli. Katika Yohana 14:6, Yesu alisema hivi: “Mimi ndiye njia na kweli na uzima. Hakuna mtu anayekuja kwa Baba bila kupitia kwangu” (TLR). Si Biblia tu iliyo ya kweli – yaani kitabu kilichofunua kwamba Yesu ni nani – bali hata Yesu Mwenyewe ni kweli.

 

Wale wanaoasi dhidi ya kweli ya Biblia pia wanakataa kumjua na kumwamini Yesu kuwa ni nani. Yesu alionya katika Yohana 12:48-50, hivi: “Yupo hakimu wake yeye anikataaye mimi na asiyekubali maneno yangu; neno lile lile nililosema litamhukumu siku ya mwisho” (TLR).

 

Kitabu hiki kina Maandiko mengi sana. Mistari mingine itatumiwa mara kadhaa kwa sababu ya umuhimu wake katika kufafanua kweli tunazojadili hapa. Kila mara, mistari hiyo itatumiwa makusudi na ni muhimu katika mantiki husika.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Utangulizi

(Introduction)

 

Mimi na Scott Hillstrom tulikutania New Zealand. Sisi wote ni mawakili tuliohamia New Zealand na familia zetu, na tumepewa vibali vya kuishi kama raia.

 

Mimi na Scott tulikuwa tunakutania kwenye Mgahawa wa Kahawa huko Durham, nyumba kadhaa kutoka Kituo cha Uchoraji katika mji wa Christchurch. Katika kuzungumza juu ya mada moja baada ya nyingine, wakati mwingine tungejikuta tumekaa na Mmarekani mmoja, na mwingine, na hata wa tatu.

 

Kwa sababu Scott na mimi ni Wakristo, mara nyingi tulijadiliana kuhusu imani yetu, kuhusu Yesu na kuhusu itikadi mbalimbali za Kikristo. Siku moja tukiwa tunajadili kuhusu Biblia, Scott alisema hivi: “Ninachohitaji mimi ni zile herufi nyekundu tu katika Biblia.” [Wenzetu katika Nchi za Magharibi wana Biblia ambazo, maneno ya Yesu yote yameandikwa kwa rangi nyekundu.]

 

Maneno ya Scott yakanishtua. Mimi naelewa kwamba Maandiko yote yamevuviwa na Mungu na hayana makosa hata kidogo katika nakala zake za asili. Bila shaka Scott alifikiri kwamba kuna mistari mingine ambayo ni ya muhimu zaidi ya mingine. Maneno yake yakanifanya nitambue kwamba mimi nilikuwa nahesabu Maandiko yote katika Agano Jipya kuwa na umuhimu unaolingana. Nilikwisha jifunza kwamba Agano la Kale halikuwa na umuhimu ule ule kwa waamini wa siku hizi kama Maandiko katika Agano Jipya. Lakini hapa, Scott akawa amesema kwamba sehemu zingine za Agano Jipya zilikuwa muhimu kuliko zingine.

 

Nikawa na mawazo sana kuhusu Scott. Mimi niliona kwamba alikuwa eneo hatari. Je, mtu angeweza kuwa mwamini wa kweli kama hakufikiri kila kitu katika Agano Jipya kina maana kwa imani yake na kuelewa Injili kwake? Nisingeweza kutoa hoja zozote wakati huo kwa sababu sikuwa nimefikiri kwa kina kuhusu swala hilo.

 

Nilipofikiri uwezekano kwamba kuna sehemu zingine za Agano Jipya ambazo ni muhimu kuliko zingine, nikakumbuka kwamba, wakati nikiwa Mkristo mpya mwenye umri wa miaka 43, nilisoma sana Injili, na kuzirudia tena na tena. Kwa kuwa mtume Petro alisema kwamba maandiko ya Paulo yalikuwa magumu kuelewa, ambayo hupotoshwa na watu wasiojua na wasiokuwa imara, kama wafanyavyo na Maandiko mengine pia, kwa hasara na uangamivu wao (2Petro 3:16), niliyaepuka maandiko ya Paulo kwa kitambo, nikisoma tena na tena Injili, halafu maandiko ya Yakobo, Petro, Yohana na Yuda. Mwishowe nikashindwa kujizuia, nikasoma nyaraka za Paulo. Nilikuta ni nzuri tu, zinakubalika, na ni rahisi kuzielewa kwa nuru ya mafundisho ya Yesu katika Injili, pengine pia kwa sababu nilizisoma kwa mara ya kwanza katika Biblia ambayo ina lugha rahisi kuelewa. Nitajitahidi kutumia tafsiri hiyo hiyo katika kitabu hiki, isipokuwa mahali nitakaposema ni tafsiri nyingine.

 

Haikunichukua muda mrefu kutambua kwamba Scott alikuwa sahihi. Yesu Mwenyewe alisema kwamba maneno Yake yalikuwa na umuhimu mkubwa kuliko maneno mengine yote yaliyowahi kuandikwa. Katika Mathayo 24:35 Yesu alisema hivi: “Mbingu na nchi vitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe” (TLR). Yesu alionyesha ni kwa nini maneno Yake yawe na nguvu kiasi hicho, katika Yohana 6:63, aliposema hivi: “Roho hutoa uzima; mwili si kitu. Maneno niliyowaambia ninyi ni Roho, na ni uzima” (TLR). LOO! Ni mtu gani aliyewahi kusema hivyo kuhusu maneno yake?

 

Hakuna madai mengine kuhusu maandiko mengine yoyote katika Biblia yenye madai yanayofanana na aliyotoa Yesu kuhusu maneno Yake. Mitume walitambua kwamba maneno ya Yesu yalikuwa tofauti. Katika Yohana 6:68, Petro alishuhudia hivi: “Wewe unayo maneno ya uzima wa milele” (TLR).

 

Hoja ya Scott ikanitazamisha tena kwenye maneno ya Yesu. Kwa miaka mingi sana nimekuwa nikijali sana kuhusu kushindwa kwa kanisa la mahali kufundisha watu wake kutii amri za Yesu. Mara nikatambua kwamba kujali kwangu kwa sehemu kulitokana na ukweli kwamba mafundisho na amri hizo zilikuwa maneno ya Yesu – ya herufi nyekundu – maneno ambayo yalikuwa maalum, maneno yaliyokuwa Roho na uzima, na ambayo yasingepita kamwe.

 

Kwa miaka mingi tangu hapo, nimetambua kwamba huku kupuuza, huku kushindwa na kukataa kwa kanisa kufundisha watu wake kutii mafundisho na amri za Yesu ni UASI. Sehemu iliyosalia ya kitabu hiki itaeleza kwa nini hii si tofauti ndogo tu ya maoni, au uelewa tofauti wa lugha. Huu uasi dhidi ya Yesu na amri Zake umegharimu na utagharimu wokovu wa mamilioni ya watu, wasiohesabika. Cha kushangaza ni kwamba uasi huu unalelewa na kuendelezwa na wachungaji na waalimu katika kanisa, walio kinyume na amri za Bwana Yesu Kristo, ambaye ndiye Kichwa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sura Ya Kwanza

(Chapter 1)

 

Uasi Dhidi Ya Yesu Kama Bwana

(Rebellion Against Jesus As Lord)

 

Yawezekana uasi unaanza kwa kukataa kumkubali Yesu kama alivyo. Hebu tuanze kwa kutazama Yesu ni nani, na jinsi kukataa jambo hilo kunavyokuwa msingi kwa ajili ya UASI mkubwa huu.

 

Katika Yohana 8:24, Yesu aliingiza swala la wokovu aliposema hivi, “Niliwaambia mtakufa katika dhambi zenu. Kama hamwamini kwamba Mimi ndiye, hakika mtakufa katika dhambi zenu” (TLR).

 

Hakuna mtu anayekufa katika dhambi zake atakayeingia katika ufalme wa mbinguni. Katika Ufunuo 21:27 mtume Yohana aliandika hivi kuhusu mbinguni: “Hakuna chochote kisichokuwa safi kitakachoingia huko, wala yeyote afanyaye mambo ya aibu au ya udanganyifu, bali wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo” (TLR). Kama dhambi zetu hazijasamehewa, tutaendelea kuwa wachafu. Ushahidi zaidi unapatikana katika Wakolosai 1:22, mahali ambapo Paulo aliandika hivi: “Lakini sasa, Yeye [Mungu] amewapatanisha ninyi kwa mwili wa Kristo kwa njia ya kifo, ili kuwafikisha mbele yake mkiwa watakatifu, msio na waa na lawama …” (TLR). Wale ambao dhambi zao hazijasamehewa wamejaa mawaa ya dhambi na ni watu wa kulaumiwa.

 

Yesu alisema tutakufa katika dhambi zetu kama hatuamini kwamba Yeye ndiye. Je, alidai kuwa nani? Katika Yohana 13:13, Yesu alisema hivi: “Ninyi mnaniita mimi ‘Mwalimu’ na ‘Bwana’, na ni sawa, maana ndivyo nilivyo” (TLR). Alipokamatwa na Wayahudi, kuhani mkuu alimwambia Yesu, “Nakuapisha kwa Mungu aliye hai: Tuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu. Yesu akajibu, ‘Ndiyo. Ni kama ulivyosema. Lakini nawaambia ninyi nyote: Katika siku za baadaye mtamwona Mwana wa Adamu ameketi upande wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija, akiwa juu ya mawingu ya mbinguni’.” (Ona Mathayo 26:63, 64, TLR).

 

Katika mistari hii michache, Yesu alidai kuwa Yeye ni Mwalimu, Bwana, Kristo, Mwana wa Adamu, na Mwana wa Mungu. Je, unaamini kwamba Yesu ni hayo yote? Wengi watasema, “Ndiyo! Mimi naamini hivyo kabisa!” Sawa. Basi lazima niulize hivi: Je, Yesu ni hayo yote kwako? Kwa mfano, ni Bwana wako? Je, unamtii Yesu kwa sababu ni Bwana wako? Hapa uwe makini sana na jibu lako. Usijidanganye mwenyewe wala usimdanganye Mungu kuhusu swala ambalo ni muhimu sana.

 

Hata katika siku za Yesu, watu walimwita Bwana, lakini wakakana kwa matendo yao. Yesu akauliza, “Kwa nini mnaniita ‘Bwana, Bwana’ na hamfanyi ninavyosema?” (ktk Luka 6:46, TLR). Ni dhahiri kwamba Yesu alitazamia wale wanaomwita Bwana wamtii.

 

Nia yangu ni kukuthibitishia kutokana na Maandiko kwamba, kumwamini na kumpokea Yesu kama BWANA ni muhimu katika imani yenye kuokoa. Paulo alituambia hivi katika Warumi 10:9, “Ukikiri kwa kinywa chako ‘Yesu ni BWANA’, na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka.” Katika Warumi 10:13, Paulo alisema hivi: “Kila atakayeliitia jina la BWANA ataokolewa” (TLR). Paulo aliweka wazi kwamba wokovu wenyewe umejengwa kwenye kumkiri Yesu kuwa ni Bwana. Alipoulizwa na askari magereza wa Filipi kwamba afanye nini ili aokoke, Paulo alimjibu hivi: “Mwamini BWANA Yesu, nawe utaokoka, wewe na wote wa nyumbani mwako” (ktk Matendo 16:31, TLR).

 

Bila shaka umesikia mara nyingi sana mwaliko huu kutoka mimbarani: “Ukimkubali (au kumpokea au kumwamini) Yesu kama Mwokozi wako, utapata uzima wa milele.” Madai kama hayo hayapo katika Maandiko – ni kitu cha ziada hicho. Inaonekana kwamba wachungaji na wanatheolojia wametengeneza mawazo yao kuhusu jinsi ya kuokoka. Kwa kuwa kila kitu kuhusu wokovu wa KiBiblia unatoka katika Maandiko, mtu anathubutuje kuingiza kitu tofauti kuliko kinachofunuliwa na Maandiko? Tusithubutu kabisa! “Injili” zinazotokana na wanadamu ni “injili nyingine”.

 

Kulingana na tafsiri yetu ya Union Version, hakuna swala la “kumkubali” Yesu kwa namna yoyote ile. Kuna mara mbili ambapo neno “kupokea” linatumiwa. Ya kwanza ni katika Yohana 1:11-13, ingawa hapo, hatuambiwi wazi kwamba tumpokee Yesu kwa namna gani. Angalia:

 

Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. 12Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 13waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

 

Matumizi mengine ya “kupokea” ni katika Wakolosai 2:6, kama ifuatavyo: “Basi, kama mlivyompokea Kristo Yesu Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye, wenye shina na wenye kujengwa katika yeye …” Hii inadhihirisha kwamba Wakolosai walimpokea yesu kama BWANA! Kwa nini wampokee Yesu kama BWANA? Paulo aliweka wazi jambo hilo aliposema hivi: “Sisi hatujihubiri wenyewe, bali tunamhubiri Yesu Kristo kama BWANA” (ktk 2Wakor. 5:4, TLR).

 

Tena Paulo aliweka wazi kabisa kwamba wokovu u katika Yesu kama BWANA. Alisema hivi, “Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira Yake, bali tupate wokovu, kwa BWANA wetu Yesu Kristo” (1Wathes. 5:9). “Mshahara wa dhambi ni kifo, lakini zawadi ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu BWANA wetu” (Warumi 6:23, TLR). Petro alishauri hivi, “Mtakaseni Kristo Yesu BWANA mioyoni mwenu” (1Petro 3:14).

 

Uthibitisho mwingine unaonishawishi mimi sana ni muunganiko wa Maandiko mawili. La kwanza ni katika Matendo 20:21, mahali ambapo Paulo aliwaambia wazee kutoka Efeso hivi: “Nimetangaza kwa Wayahudi na Wayunani kwamba lazima wamgeukie Mungu kwa toba, na kumwamini BWANA wetu Yesu” (TLR). Sasa, unganisha mstari huo na ile mistari inayojulikana sana katika Waefeso 2:8, 9 – “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani [katika BWANA wetu Yesu]; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”.

 

Sehemu ya kwanza ya kitabu changu cha kwanza, Imani Yenye Kuokoa, inashughulika na vithibitisho kwamba Yesu ni lazima awe Bwana wa wote watakaookolewa. Pengine njia ya kupata mtazamo wa Mungu kuhusu umuhimu wa Yesu kuwa Bwana ni kuona anaitwa BWANA mara ngapi katika Agano Jipya. Orodha ifuatayo inaonyesha majina mengi ya Yesu, na yanatumika mara ngapi katika Agano Jipya.

 

                        Mara 618 anaitwa BWANA

                        Mara 543 anaitwa Kristo

                        Mara 84 anaitwa Mwana wa Adamu

                        Mara 42 anaitwa Mwalimu

                        Mara 37 anaitwa Mwana wa Mungu

                        Mara 35 anaitwa Mfalme

                        Mara 32 anaitwa Mwanakondoo

                        Mara 15 anaitwa Mwokozi

                        Mara 15 anaitwa Nabii

                        Mara 11 anaitwa Mkuu

                        Mara 7 anaitwa Kuhani Mkuu

 

Bila shaka ujumbe umefika, sivyo? Sasa, inakuwa na nguvu zaidi tena tunapojifunza kwamba jina “Kristo” limehusisha jina “Bwana” ndani yake. Katika Warumi 1:4, Paulo aliandika hivi: “ … alidhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho y utakatifu kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo BWANA wetu.” Hapa, Paulo alitangaza kwamba Mwana wa Mungu ni Yesu Kristo BWANA wetu. Aliunganisha pamouja majina makuu ya Yesu katika kuhakikisha kwamba tunatambua Yesu ni Mwana wa Mungu, ni Kristo, na ni BWANA.

 

Andiko lingine linanishawishi sana. Katika Warumi 14:9, Paulo anafafanua kitu, hivi, “Maana Kristo alikufa akaw ahai tena kwa sababu hii, awe BWANA wa walioikufa na walio hai pia” (TLR). Hapa, Paulo anadhihirisha kwamba sababu ya Yesu na thawabu Yake kufa na kufufuka ilikuwa ili aweze kuwa BWANA wetu.

Kuna maandiko mengine mia sita na zaidi yanayohusu Yesu kuwa BWANA. Ni mada kuu katika Agano Jipya. Mungu anasisitiza kwamba Yesu lazima awe BWANA wa wote watakao-okolewa.

 

Je, kuna mabwana wengi? Je, Mungu Baba ni Bwana wetu? Katika 1Wakorinto 8:5 na 6, Paulo alifafanua hivi: “Kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani (kama vile walivyoko ‘miungu’ mingi na ‘mabwana’ wengi); lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na BWANA mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo.”

 

Wengi katika kanisa la Nchi za Magharibi wako katika UASI dhidi ya BWANA Yesu Kristo. Viongozi wake wanakataa kutambua kwamba Yeye ni Bwana, na badala yake, wanatengeneza UKanisa katika Ukristo. Ingawa wakati mwingine wanatumia jina Bwana kwa habari ya Yesu, hawafundishi maana ya Yesu kuwa BWANA wa mtu. Hawafundishi kwamba ni muhimu kumtii Yesu kama BWANA katika maisha ya mtu. Ndani ya hicho ndipo kuna msingi wa UASI mkuu dhidi ya Yesu kama BWANA.

 

Kama Yesu alifundisha, na mistari mingine inathibitisha hivyo, kwamba lazima awe BWANA wa watu wote watakao-okoka, mbona mtu asikubali kumpigia Yesu goti, kumpokea kama Bwana na kuwafundisha wengine kufanya hivyo? Nadhani jibu lake ni kukataa na kutokuwa tayari kuwa chini ya mamlaka ya Yesu. Swali tunalopaswa kuuliza ni hili: “Yesu atafikiri nini kuhusu watu kuacha kumkubali kama Bwana?” Katika Luka 19:12-27, Yeye Mwenyewe alijibu swali hilo katika mfano ambao ulikuwa na mafundisho mawili tofauti. Tutachunguza ile sehemu ya mfano inayomhusu Yeye tu. Yesu alizungumza juu ya mtu mkuu aliyekwenda nchi ya mbali ili kupewa ufalme, kisha arudi. Lakini watu wake walimchukia, mpaka wakamtumia ujumbe kumwambia, “Hatumtaki mtu huyu awe mfalme wetu.” Pamoja na hayo, alifanywa kuwa mfalme na akarudi nyumbani. Mfano uliishia pale Yesu aliposema, “Lakini, wale adui zangu waliokataa mimi nisiwe mfalme juu yao – waleteni hapa, mkawaue mbele yangu” (TLR). Kutakuwa na mwisho wa kutisha sana kwa wale wanaokataa kumkubali Yesu kama Bwana maishani mwao!

 

Kanisa la siku hizi kwa sehemu kubwa linatafuta njia za kujenga majengo makubwa yaliyojaa watu maelfu. Wachungaji hukimbia-kimbia toka kwa kiongozi mmoja wa kanisa hadi mwingine, ambaye ameunda kanisa kubwa karibuni. Wanapuuza mafundisho ya Yesu yenye kuonyesha kwamba cha muhimu ni sifa na utii wa mtu yule atakayemfuata, si idadi ya watu wanaodai kuwa wanamfuata.

 

Watu wengi ni kama hawatambui masharti ambayo Mungu ameweka kwa wale watakaopata wokovu. Ukweli ni kwamba, kuna wenye kukazia sana kwamba hakuna masharti yoyote. Huo ni udanganyifu na ulaghai. Tutazungumza zaidi kuhusu hili katika sura zinazofuata.

 

Ukitaka kutazama kwa upana zaidi Maandiko yenye kuonyesha ukuu wa Yesu kama Bwana, tazama kwenye tovuti ifuatayo: www.bereanpublishers.com, halafu tafuta kitabu kiiitwacho Imani Yenye Kuokoa, Ukurasa wa Pili, Yesu Ni Bwana. [Hiki kitabu kinapatikana kwa Kiswahili]

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sura Ya Pili

(Chapter 2)

 

Uasi Dhidi Ya Maneno Ya Yesu

(Rebellion Against Jesus’ Words)

 

Mimi naamini kwamba UASI katika kanisa hauwezi kuonekana kwa uwazi zaidi kuliko katika kanisa kushindwa kwa makusudi na kukataa makusudi kufanya yale ambayo Yesu aliamuru.

 

Uasi si dhana ngumu sana. Watoto ni waasi wanapokataa kufanya yale wanayoambiwa na wazazi wao, au waalimu, au wengine walio katika mamlaka. Wahalifu huasi dhidi ya mamlaka; wameazimia kufanya wanachotaka, wakati wanaotaka, bila kujali jamii itaumia kiasi gani. Uasi pia hutokea dhidi ya serikali. Taarifa ya leo ilionyesha vurugu katika barabara za nchi mbili ambazo wananchi walikuwa wanaasi dhidi ya serikali za kiimla.

 

Wakati mwingine uasi unaweza kuwa kitu cha kisiri, mtu anapoacha kutii sheria za mwenye mamlaka. Wakati mwingine inaweza kuwa kitu kinacho-onekana, kwa kushawishi na kuwafundisha wengine kuasi kwa kuacha kutii sheria.

 

Neno uasi linaweza kuwa na maana zifuatazo:

 

 

Pengine unajiuliza ikiwa maana yoyote katika hizo inaweza kuhusiana na matendo yafanyikayo kanisani. Ni matumaini yangu kwamba kadiri tunavyoendelea, utashawishika kuamini kwamba matendo hayo yote ni kitu halisi katika kanisa la Nchi za Magharibi, katika hii Karne ya Ishirini na Moja.

 

Je, kanisa linaasi dhidi ya mwenye mamlaka gani? Ingawa itaonekana kama si hivyo, Kanisa la Kikristo linamwasi mkuu wake – BWANA Yesu Kristo. Je, Maandiko yanatufundisha nini kuhusu mamlaka ya Yesu?

 

Paulo aliwafundisha Wafilipi hivi: Mungu alimtukuza Yesu na kumpa Yeye jina lipitalo kila jina, kwamba, kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, mbinguni na duniani na chini ya nchi, na kila ulimi ukiri kwamba Yesu Kristo ni BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba (ktk Wafilipi 2:9-11).

 

Paulo alishuhudia kwamba Yesu ndiye mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote (ktk Wakolosai 1:15). Paulo anasema BWANA Yesu alihusika na uumbaji. “Kwa kuwa katika Yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyo-onekana na visivyo-onekana, ikiwa ni viti vya enzi, au usulatani, au enzi, au mamlaka, vitu vyote viliumbwa kwa njia Yake, na kwa ajili Yake” (ktk Wakolosai 1:16).

 

Paulo alituambia juu ya mpangilio wa mamlaka unaotuhusu, hivi: “Naye [Yesu] amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika Yeye. Naye [Yesu] ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote” (Wakolosai 1:17, 18).

 

Paulo alishuhudia kwamba Mungu alimweka Yesu upande Wake wa kuume katika ulimwengu wa roho, juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia. Na Mungu akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa …” (Waefeso 1:22)

 

Nimeirejea mistari hiyo kama kukumbushia tu kwamba Yesu ni nani kwa habari ya kanisa Lake – Yeye ndiye kichwa, mwenye mamlaka yote, uwezo na ukuu. Je, hicho kiko wazi? Kinaeleweka? Hakuna mamlaka mbinguni au duniani iliyo kuu kuliko Bwana Yesu. Anapoanza kutoa Agizo Kuu katika Mathayo 28:18, Yesu alisema hayo hayo, kama ifuatavyo: “Nimepewa mamlaka yote, mbinguni na duniani.”

 

Mungu Mwenyewe aliamuru kwamba tumsikilize Yesu. Wakati Yesu na Petro na Yohana walipokwenda juu mlimani, na Yesu akageuzwa sura mbele yao, sauti ya Mungu ilitoka katika wingu ikasema hivi, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependwa naye. Msikilizeni!” (ktk Mathayo 17:5; Marko 9:7 na Luka 9:35, TLR) Tafsiri mbalimbali za Biblia zinaonyesha kwamba maana ya “msikilizeni” ni tofauti na “msikieni”. Biblia ya mafunzo iitwayo Zodhiates inaonyesha kwamba maana ya “kusikiliza” ni kusikiliza kwa akili zote (yaani, kutilia maanani, kutii, na kadhalika). Tafsiri inayofaa ya agizo la Mungu ni hii: “Sikilizeni kwa makini, na mumtii Yeye”! Hiyo inakubaliana kabisa na Maandiko mengine katika Agano Jipya.

 

Je, Bwana Yesu alitazamia wafuasi Wake kumtii? Ndiyo! Aliwauliza hivi, “Kwa nini mnaniita ‘Bwana, Bwana’ na hamfanyi ninayosema?” (ktk Luka 6:46, TLR). Hata siku hizo – kama leo tu – watu walimwita Yesu Bwana, lakini walikataa kumtii.

 

Kuna sababu nyingine muhimu sana kwetu kumwamini na kumtii Bwana Yesu. Yesu alikazia tena na tena kwamba kila kitu alichosema na kufanya akiwa hapa duniani kilikuwa kile ambacho Baba Yake alimwambia afanye na kusema. Katika Yohana 12:49-50, Yesu alisema hivi: “Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, Yeye Mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.” Ona pia katika Yohana 3:34; 8:28; 14:10; 14:24 na 14:31. Ndiyo maana Mungu alitwambia tumsikilize Yeye.

 

Kwa kuwa Mungu ndiye alimwambia Yesu cha kusema na jinsi ya kukisema, sasa tunaweza kuelewa vizuri zaidi alichokisema Yesu kuhusu maneno Yake. “Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe” (ktk Mathayo 24:35; Marko 13:31 na Luka 21:33, TLR). Yesu pia alisema hivi: “Maneno niliyowaambia ninyi ni roho, tena ni uzima” (ktk Yohana 6:63, TLR). Hata yale aliyosema kuhusu maneno Yake ni ambayo Mungu Baba alimwambia aseme.

 

Yesu alitoa mifano mingi sana kuhusu umuhimu wa maneno Yake. “Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa, kwa kuwa imejengwa vizuri. Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa" ” (ktk Luka 6:47-49. Ona pia Mathayo 7:24-27).

 

Mitume walitambua kwamba maneno ya Yesu yalikuwa tofauti. Simoni Petro alimjibu Yesu hivi: “Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele” (ktk Yohana 6:68, TLR).

 

Ukweli kwamba Yesu alisema na kufanya yale tu ambayo Mungu Baba Yake alimwamuru kusema na kufanya ni muhimu sana, kwa sababu maana yake ni kwamba kila kitu Yesu alichosema na kufanya kilikuwa mapenzi ya Mungu. Hilo likawa swala la wokovu aliposema hivi:

 

“Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana’ atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (ktk Mathayo 7:21).

 

Jambo linahusu wokovu wakati sharti linapotamkwa kwa ajili ya wokovu. Hapa, Yesu alifunga idadi ya wale watakaoingia katika ufalme wa mbinguni. Ni wale watendao mapenzi ya Baba Yake. Basi, kufanya mapenzi ya Baba ni swala la wokovu – sharti ambalo lazima litoshelezwe kama mtu ataingia katika ufalme wa mbinguni. Mtume Yohana aliunga mkono jambo hilo katika 1Yohana 2:17, hivi: “Dunia na tamaa zake inapita, lakini mtu atendaye mapenzi ya Mungu ataishi milele.” Kwa maneno mengine, anacchosema Yohana ni kwamba, wale tu watendao mapenzi ya Mungu ndiyo watakaoingia mbinguni. Anatuhakikishia kwamba wote wanaofanya mapenzi ya Mungu wanao uzima wa milele.

 

Je, kanisa linatenda mapenzi ya Mungu kwa kutii yale aliyoagiza Bwana Yesu? Hapana – na inasikitisha sana! Viongozi wa kanisa wanasema, “Bwana! Bwana!” lakini wanakataa kufanya mapenzi ya Mungu – kutii kila kitu ambacho Yesu alifundisha na kuamuru. Hatuwezi kuingia katika ufalme wa mbinguni mpaka tufanye mapenzi ya Mungu. Hilo ndiyo sharti kubwa lililo juu ya yote, kuhusu wokovu. Tukirudia tena, ni hivi: Hatuwezi kuokoka (au, kuingia katika ufalme wa mbinguni) kama hatufanyi mapenzi ya Mungu. Ni mapenzi ya Mungu kwamba waamini wa Agano Jipya watii mafundisho na amri za Yesu. Ni mapenzi ya Mungu kwamba kanisa lifanye watu kuwa wanafunzi kwa “kuwafundisha kuyatii yote ambayo Mimi [Yesu] nimewaamuru ninyi” (ktk Mathayo 28:20, TLR).

 

Wengi katika kanisa siku hizi ni kama wanayaonea aibu maneno ya Yesu. Hawa watu ni kama wanaamini kwamba maneno ya Yesu hayafai katika kile wanachodai kwamba ni mfumo mpya katika kutafuta jinsi ya kuwafikia wasiokwenda kanisani katika njia mpya za kisasa zinazofaa. Lakini, Maandiko yanasema kwamba Yesu Kristo ni yule yule jana na leo na milele (ktk Waebrania 13:8). Yesu alisema hivi: “Maana kila mtu atakayenionea haya mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu” (ktk Marko 8:38. Ona pia Luka 9:26). Kama tulivyoona hapo nyuma kidogo, Yesu alionya hivi, “Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho” (ktk Yohana 12:48-50).

 

Umeona mkazo mkubwa unaowekwa kwenye maneno ya Yesu? Tutahukumiwa tusipoyakubali maneno ya Yesu; yale yale aliyosema yatawahukumu wale wasiokubali maneno Yake. Maneno ya Yesu hayatapita kamwe. Maneno ya Yesu ni roho na ni uzima. Mtu asikiaye maneno ya Yesu na kuyatenda, anafananishwa na mtu aliyejenga msingi wake kwenye mwamba.

 

Tufanye marudio kidogo: Bwana Yesu ana mamlaka yote mbinguni na duniani, na ndiye kichwa cha kanisa Lake. Maneno yote aliyosema Yesu na matendo aliyofanya hapa duniani yalikuwa yale ambayo Mungu Baba Yake alimwagiza kusema na kutenda. Maneno ya Yesu yote na matendo Yake yote yalikuwa mapenzi ya Mungu. Wale tu watendao mapenzi ya Mungu ndiyo watakaoingia katika ufalme wa mbinguni.

 

Vipi kuhusu Agano la Kale? Wengi wanadai kwamba kuna sheria, maagizo na amri katika Agano la Kale ambazo lazima wafuasi wa Kristo wazitii. Hebu tuchunguze Wakristo wanapaswa kutii nini.

 

Wakristo Ni Lazima Watii Hizi.

Kwanza, hebu tuweke wazi kabisa kwamba katika Agano Jipya, mara nyingi linapotumika, neno “sheria” linamaanisha zile sheria za Agano la Kale – zilizotolewa na Musa. Ndiyo “sheria” pekee za kidini zilizojulikana na Wayahudi wakati ule. Kisiasa, Wayahudi walikuwa chini ya sheria za serikali ya Warumi waliokuwa wanawatala wakati wa Kristo.

 

Musa alitabiri kuhusu Masiya aliyekuwa anakuja wakati aliposema hivi: “Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi. Na itakuwa ya kwamba kila mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake” (ktk Matendo 3:22, 23). Petro akitumia maneno ya Musa, alisema kwamba Musa alimaanisha Yesu. Hata Musa, karne nyingi kabla, aliwaagiza Wayahudi kumsikiliza Yesu wakati alipokuja. Kumbuka kwamba “kusikiliza” ni sawa na kusikiliza kwa makini, na kutii kinachosikiwa.

 

Kumbukumbu la Torati ni mahali pazuri pa kupata habari juu ya amri za Mungu zilizotolewa kwa njia ya Musa – yaani, Torati ya Wayahudi. Tunajifunza hii sheria ilimhusu nani wakati Musa aliposema na wana wa Israeli kabla ya kuitoa. Tazama kwa makini sana lugha anayotumia katika fungu hili.

 

“Na sasa, ee Israeli, zisikilizeni amri na huku niwafundishazo, ili mzitende, mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi awapayo Bwana, Mungu wa baba zenu. Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za Bwana, Mungu wenu, niwaamuruzo

(Kumbu. 4:1-2).

 

“Na hii ndiyo sheria, na amri, na hukumu, alizoziamuru Bwana Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki; upate kumcha Bwana Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za maisha yao; tena siku zako ziongezwe” (Kumbu. 6:1-2).

 

Je, Musa alikuwa anazunguma na nani? Waisraeli. Alirudia tena na tena kwamba hayo yalikuwa kwa ajili “yenu” – Israeli. Halafu akaongeza na watoto, wajukuu na vizazi vijavyo vya Israeli, ambao wangefaidika kutokana na mahusiana haya binafsi na Mungu, na ambao wangefurahia baraka Zake kwa kuzishika sheria Zake.

 

Je, Mungu aliwaambia Israeli wawaongoe jirani zao waliokuwa wa Mataifa, na kuwafundisha zile sheria alizokuwa anawapa? Hapana. Yeye aliwaamuru Israeli wawaue wale watu wasiokuwa Wayahudi katika nchi ya Kanaani, kwamba wasimwache hai hata mmoja ili wasije kuwanajisi Waisraeli kwa kuabudu sanamu kwao. Ona Kumbukumbu la Torati 7:16.

 

Amri hizo zilikuwa kwa ajili ya Israeli ya siku hizo, pamoja na vizazi vya baadaye. Mungu aliamuru hivi:

 

“Na maneno haya ninayokuamuru leo yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. Tena, yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako” (Kumbu. 6:4-8).

 

Amri hizo zilikuwa binafsi kwa Israeli na uzao wake. Kila kizazi kilipaswa kuzifundisha amri hizo kwa watoto wake. Pamoja na amri, Mungu aliweka mbele yao baraka na laana.

 

“Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana: baraka ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya Bwana Mungu wenu, niwaagizayo leo; na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya Bwana Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua” (Kumbu. 11:26-28).

 

Sheria, amri, mahusiano na Mungu, baraka na laana – vyote hivyo vilielekezwa kwa watu wa Israeli na vizazi vyao vilivyofuata. Mungu aliwajali kipekee sana wageni waliokuwa wanakaa katika nchi ile, maana aliwaagiza Israeli kuwapenda wageni kwa sababu wao pia walikuwa wageni katika nchi ya Misri. Ona Kumbu. 10:19. Lakini mgeni hakuwa chiniya sheria ambazo Mungu aliwapa Israeli. Mungu alipowaamuru wana wa Israeli wasile kitu chochote watakachokuta kimekwisha kufa, alisema hivi: “Msile nyamafu yoyote. Waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula, au kumliza mtu wa mataifa, kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako” (Kumbu. 14:21).

 

Torati ya Musa ilitolewa kwa Israeli; wao walitakiwa kuitii. Hawakuamriwa wawafundishe watu wa Mataifa kuitii Torati (isipokuwa wale ambao wangeongoka na kufuata dini ya Kiyahudi kabla ya kuja kwa Yesu). Torati ilikusudiwa kwa ajili ya taifa la Israeli.

 

Agizo la tohara lilitolewa na Mungu kwa Ibrahimu kama sehemu ya agano Lake na Ibrahimu na wazao wake, kabla Torati haijatolewa kwa Israeli. Tutazame mistari husika.

 

“Mungu akamwambia Ibrahimu, ‘Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako. Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako: Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa … na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi.

… Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu” (Mwanzo 17:9-12, 14).

 

Paulo aliwafundisha hivi Wagalatia, “Fahamuni basi ya kuwa wale walio wa imani, hao ndiyo wana wa Ibrahimu. Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani kusema, ‘Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa’.” (Wagalatia 3:7-9).

 

Kusoma mistari hiyo juu-juu inaweza kumfanya mtu kuamini kwamba mwanamume yeyote ambaye ni mzao wa Ibrahimu anapaswa kutahiriwa, hata siku hizi. Hata waamini wa Mataifa wanahesabiwa kuwa “watoto wa Ibrahimu” kama Paulo alivyowaambia wagalatia. Basi bila shaka ni dhahiri kwamba hata waamini wa Mataifa lazima watahiriwe. Sivyo!

 

Paulo aliwafundisha Wakorintho hivi, “Je, mtu fulani ameitwa hali amekwisha kutahiriwa? Asijifanye kana kwamba hakutahiriwa. Mtu fulani ameitwa hali hajatahiriwa bado? Basi asitahiriwe. Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu; bali kuzihifadhi amri za Mungu” (ktk 1Wakor. 7:18, 19). Paulo alikuwa mkali sana alipowakemea Wagalatia, kama ifuatavyo:

 

“Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno. … Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo”

(Wagalatia 5:2, 6).

 

Je, Paulo alikuwa amepotea? Mungu alimwambia Ibrahimu vizuri kabisa kwamba yeye na wazao wake walipaswa kutahiriwa. Tunasoma bila ya kuwa makini. Alama ya tohara ilikuwa ishara ya agano kati ya Mungu na Ibrahimu, na wazao wa Ibrahimu. Haikuwa ishara ya agano kati ya Mungu na wale ambao wangemwamini Kristo Yesu kama Bwana wao – waitwao watoto wa Ibrahimu. Mzao ni wa ukoo huo – mtu yeyote aliye hai, wa ukoo huo. Neno watoto linatumiwa kuhusu wale wanaoamini, kama jinsi Ibrahimu alivyomwamini Mungu.

 

Yesu alisema hakuja kuitangua Torati wala Manabii. “Sikuja kutangua bali kutimiliza” (ktk Mathayo 5:17, TLR). Pia alisema hivi: “Kwa maana, amin nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapo-ondoka, yodi moja wala nukta moja ya Torati haitaondoka, hata yote yatimie” (ktk Mathayo 5:18). Je, umeona angalizo lililopo mwishoni mwa Mathayo 5:18? Yesu alisema kwamba hakuna chochote kitakachotoweka kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kitakapotimizwa.

 

Hoja inaweza kutolewa kwamba kila kitu katika Torati kilitimizwa muda mfupi kabla ya kifo cha Yesu msalabani, aliposema maneno yake ya mwisho kwamba, “Imekwisha!” (Yohana 19:30). Dhabihu za wanyama hazikuhitajika tena. Yesu alitimiza kusudi Lake kiukombozi kama mwanakondoo wa dhabihu wa Mungu ili aziondoe dhambi za dunia. Inaonekana ndivyo Paulo alivyoelewa wakati alipowaambia Warumi kwamba “Kristo ndiye mwisho wa Torati …” (Warumi 10:4, TLR). Maelezo ya ziada katika Biblia ya NIV ya kujifunzia yanaonyesha kwamba neno “mwisho” (telos) linaweza kuwa na maana kadhaa – (1) “kukomeshwa”, “kwisha”, au (2) “lengo,” “kufikia kilele,” au “kutimizwa” na inashauri kwamba ni afadhali kulielewa neno hilo katika maana yake ya mwisho, kwamba, ni kutimizwa kwa Torati. Biblia ya Amplified inasema hivi:

 

“Maana Kristo ndiye mwisho wa Torati – mahali ambapo inakoma kuwepo, kwa sababu Torati inaendelea mpaka Kwake Yeye aliye utimizo wa mifano yake yote, na katika Yeye kusudi la kutengenezwa kwake inatimia. – Yaani, kusudi la Torati linatimizwa katika Yeye – kama njia ya haki (mahusiano sahihi na Mungu) kwa kila mtu anayemwamini na kukubaliana Naye na kumtumaini” (Warumi 10:4, Tafsiri ya Amplified).

 

Sheria ya Agano la Kale ilitimizwa, na ndani ya Kristo inakoma. Haitawali maisha ya mwamini wa Agano Jipya. Paulo alisisitiza sana kwamba, “… ninyi hamko chini ya sheria …” (ktk Warumi 6:14, TLR).

 

Uthibitisho zaidi kwamba waaminio wa Agano jipya hawako chini ya sheria unatolewa na Paulo anaposema kwamba Yesu aliiondoa sheria kwa njia ya dhabihu Yake pale msalabani.

 

“Kwa maana Yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja, akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake, ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo, ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake, akafanya amani. Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba” (Waefeso 2:14-16).

 

Hapo basi tunaona kwamba Sheria imetimizwa na imeondolewa. Ingawa Yesu alikuja kuitimiza Sheria, alipoitimiza aliiondoa pia ili waamini wote waweze kuwa mmoja ndani Yake, wala wasiwe tena chini ya nira ya Torati ya Agano la Kale.

 

Kuna wanaosema ni maagizo tu ndiyo yaliondolewa. Maandiko yametamka wazi wazi kabisa kwamba ni “sheria ya amri zilizo katika maagizo”.

 

WaSabato mara nyingi hutoa hoja kwamba zile amri kumi hazihusiki. Wanaziita Amri Kumi kuwa ni Sheria ya Maadili (hata ingawa amri ya nne haina mantiki yoyote ya maadili). Hebu fikiri kidogo kinachofafanuliwa katika mstari huu:

 

“Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si kwa andiko, bali kwa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha. Basi, ikiwa huduma ya mauti iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe …” (2Wakor. 3:6, 7).

 

Tunajua kwamba zile Amri Kumi zilitolewa kwa Musa zikiwa zimeandikwa kwenye mawe. Hakuna sheria nyingine iliyoandikwa na Mungu kwenye mawe. Bila shaka mstari huo hapo juu unahusiana na zile Amri Kumi. Paulo anasema juu yake kwamba ni sawa na ile ile Torati ambayo imepita, lakini kwa sasa anaitaja kuwa ni “huduma ya mauti”. Zile Amri Kumi ni sehemu ya hiyo “Torati” ambayo Paulo anaitaja mara kwa mara. Lakini kama ambavyo tumekwisha ona, na kama tutakavyoona tena na tena, Torati hiyo imeondoka kwa mfuasi wa Kristo – Yesu aliiondoa Torati kwa njia ya mwili Wake.

 

Paulo alisisitiza jambo hilo hilo kwa Wakolosai, kama ifuatavyo: “Mungu … akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu, akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani” (Wakolosai 2:14). Torati ya Agano la Kale pamoja na maagizo na sheria zake imetimizwa, imekoma kuwepo, imeondolewa, na imegongomelewa msalabani.

 

Sasa, kwa kuwa tu Mkristo hayuko chini ya Torati ya Agano la Kale haimaanishi kwamba Agano la Kale halina thamani kwa mwamini wa Agano Jipya. Zipo sababu nyingi sana za kujifunza Agano la Kale.

 

Kwanza kabisa – kuna unabii mwingi sana kuhusu Yesu Kristo katika Agano la Kale. Sababu kubwa sana ya kumfuata Yesu ni kwamba Yeye alitimiza unabii unaopatikana katika Torati ya Agano la Kale, na katika manabii wake. Ni mtu mmoja tu ambaye ametimiza unabii wa Masiya wa Wayahudi anayekuja. Yesu alitimiza unabii wote huo, isipokuwa ule ambao wakati wake bado.

 

Pili – Agano la Kale linatuambia mengi sana kuhusu Mungu. Linaeleza sifa Zake, uwezo Wake, mamlaka Yake, na kutuambia majina Yake. Tunajifunza juu ya  nguvu Zake za ajabu, jinsi alivyoumba ulimwengu, jinsi anavyojali kuhusu uumbaji Wake na jinsi anavyowaheshimu wale wanaolicha jina Lake, wanaomtumaini, wanaomwabudu, wanaompenda n akumtii Yeye. Kwa kuwa Mungu habadiliki, kweli hizo zinatufaa sisi na kuwa na maana kama ilivyokuwa zilipoandikwa. Ona Waebrania 13:8.

 

Tatu – Agano la Kale linaonyesha jinsi Mungu anavyoshughulika na watu Wake, jinsi atakavyowaadhibu na kuwatia nidhamu wanapomwacha kwa ajili ya kufuata miungu mingine, jinsi atakavyowabariki, kuwalinda na kupigana kwa ajili yao wakati wanapodumu kuwa waaminifu Kwake na kumtumaini Yeye kama Mungu wao. Katika Waebrania, mwandishi alitumia maneno ya Agano la Kale alipoeleza kutokuamini na kutokutii kwa wana wa Israeli baada ya kuondoka Misri. Mungu aliwazuia kuingia katika raha Yake – yaani, ile nchi ya ahadi ya Kanaani. Mwandishi akashauri hivi, “Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu yeyote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi” (Waebrania 4:11). Petro naye alifafanua ni kwa nini tumeambiwa habari za Sodoma na Gomora katika Agano la Kale: “Tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya” (2Petro 2:6).

 

Nne – Agano la Kale hutoa shuhuda binafsi za watu ili kutuhamasisha katika mwendo wetu na Bwana. Tunajifunza kuhusu watu kama Henoko ambaye alikuwa na mahusiano ya karibu sana na Mungu. Siku moja akaenda kuishi pamoja na Bwana – hakuonja kifo. Tunapewa mfano wa uvumilivu wa Nuhu ambaye alijenga safina kama alivyoagizwa na Mungu kwa kipindi cha miaka zaidi ya mia na ishirini. Ingawa bila shaka alidhihakiwa na kile kizazi kiovu cha wakati wake, alivumilia na kuokoa familia yake isiangamie katika gharika. Yusufu alidumu kuwa mwaminifu kwa Mungu na akawa wa pili kwa mamlaka katika nchi ya Misri, na Mungu akamtumia yeye kuiokoa familia yake yote pamoja na nchi ya Misri kutokana na njaa. Danieli alimheshimu Mungu na kumtii maisha yake  yote, akakombolewa na Mungu katika pango la simba na kutumiwa kwa hali ya juu sana katika falme zilizofuata. Shedrak, Meshak na Abednego wanatuonyesha jinsi ya kusimama kwa ajili ya Mungu mbele ya mamlaka kuu sana duniani. Mungu alionyesha nguvu Yake kuu ya kukomboa watu Wake wanaomwamini kutokana na tanuru la moto. Shuhuda zingine nyingi za watu waaminifu na wasiokuwa waaminifu husaidia kutufundisha jinsi ya kuishi maisha ya kutii mafundisho na maagizo ya Bwana wetu Yesu.

 

Ingawa kuna mengi sana ya kujifunza kutoka katika Agano la Kale, hatupaswi kutii amri zake, sheria na maagizo. Paulo alishughulika na Wagalatia ambao walikuwa wameshawishiwa na watu waliotaka kufanya Mataifa kuwa Wayahudi kwamba watii mila na desturi ya Kiyahudi, ikiwa ni pamoja na tohara. Hao watu walikuwa Wayahudi waliodai kuwa ni Wakristo, lakini walidai kwamba Wakristo wasiokuwa Wayahudi waishike Torati ya Kiyahudi. Je, hiyo ilikuwa tofauti ndogo tu kiitikadi? Je, yalikuwa ni maoni tofauti, yasiyokuwa mazuri wala mabaya? Hapana kamwe!

 

Yaani! Paulo alikosa hata lugha ya kukemea hilo kwa ukali sana. Alisema jambo hili ni “injili nyingine – ambayo si injili hata kidogo” (ktk Wagalatia 1:6, 7, TLR). Aliwahukumu vikali wale walioleta hiyo injili bandia akisema, “Kama mtu yeyote anawahubiria ninyi injili ambayo si ile mliyopokea, na alaaniwe milele!” (ktk Wagalatia 1:9, TLR).

 

Yesu Kristo alileta agano jipya – lile la kale liliondolewa. “Kristo ndiye mjumbe wa agano jipya, ili wale walioitwa waweze kupokea ule urithi wa milele, ulioahidiwa …” (ktk Waebrania 9:15, TLR). Ile ishara ya agano la kale – tohara – haitumiki tena; si ishara ya agano jipya. Tena Paulo alifundisha kwamba, kibaya zaidi ni hivi: kurudi chini ya Torati ili kudai tohara kulimaanisha kwamba walikuwa wanaacha uhusiano wao na Yesu Kristo – Kristo asingekuwa na maana tena kwao. Walikuwa wanaonyesha imani yao kwamba Yesu, maneno yake na dhabihu aliyotoa havitoshi – kwamba, kunatakiwa kitu zaidi.

 

Muda mrefu tu kabla Kristo hajaja, Mungu alimfanya Yeremia atabiri hivi: “Angalia siku zinakuja, asema Bwana, nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya; halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, mimi nami sikuwajali, asema Bwana” (Waebrania 8:8, 9, kwa kutumia maneno kutoka Yeremia 31:31, 32).

 

Katika Pasaka ya mwisho ambayo Yesu alishiriki na wanafunzi Wake, alichukua kikombe (kile cha upatanisho baada ya kula), akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu Yangu, imwagikayo kwa ajili yenu” (ktk Luka 22:20, TLR). Ishara ya agano jipya si tohara – kama ilivyokuwa katika Torati ya Agano la Kale – bali ni kile kitu kinachoitwa na Wakristo, Meza ya Bwana – kule kushiriki mkate na divai (au kitu badala ya divai) kusherehekea mwili wa Kristo na damu Yake iliyomwagika kwa ajili ya msamaha wa dhambi, mara moja tu kwa ajili ya wakati wote (Waebrania 9:26, 28; 10:10; 1Petro 3:18).

 

Sit u kwamba kulikuwepo na badiliko la agano, bali hata ukuhani pia ulibadilika. Mungu alimtangaza Yesu kwamba, “Wewe ni kuhani milele, kulingana na utaratibu wa Melkizedeki” (Waebrania 7:17, kutumia maneno ya Zaburi 110:4). Akisema kwanza juu ya sheria ya zamani na halafu juu ya ukuhani wa Yesu, mwandishi wa Waebrania aliendelea hivi:

 

“Maana, kuna kubatiliwa kwa ile amri iliyotanguliwa, kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake. Kwa maana ile sheria haikukamilisha neno; na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwa hayo twamkaribia Mungu. Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo – maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye (Yesu) pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, ‘Bwana ameapa, wala hataghairi: Wewe u kuhani milele.’ Basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi” (Waebrania 7:18-22).

 

Mungu alifanya mambo yote kuwa mapya kwa njia ya Yesu. Yesu ambaye ni kuhani mkuu mpya kwa kufuata utaratibu wa Melkizedeki, alithibitisha agano jipya. Tena, si jipya tu, pia ni bora zaidi.

 

“Lakini, huduma (ukuhani) ambayo Yesu amepokea ni bora zaidi kuliko yao (Walawi), kama ambavyo hata agano ambalo yeye ni mdhamimi wake lilivyo bora zaidi kuliko lile la kale, tena, limejengwa juu ya ahadi zilizo bora zaidi” (Waebrania 8:6, TLR).

 

Sasa, kama agano lilibadilika na ukuhani ukabadilika, kuna kingine ambacho Mungu alibadilisha?

 

Ndiyo. Mungu aliibadilisha sheria! Tunasoma hivi katika Waebrania 7:12, “Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike”.

 

Na, kuna sheria mpya. Katika Wagalatia 6:2, Paulo anaiita hiyo sheria mpya “sheria ya Kristo”. Ni lile kundi la amri na maagizo na mafundisho ambavyo Yesu aliagiza vifundishwe kwa kila mwanafunzi mpya, hivi: “… na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi” (ktk Mathayo 28:20).

 

Paulo aliilinganisha sheria ya Mungu na sheria ya Kristo.

 

“Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria. Si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo, ili niwapate hao wasio na sheria” (ktk 1Wakor. 9:21).

 

Paulo aliwashauri Wagalatia kama ifuatavyo: “Mbebeane mizigo ninyi kwa ninyi. Kwa njia hiyo mtaweza kuitimiza sheria ya Kristo” (ktk Wagalatia 6:2, TLR). Paulo akasema tena, “Ruhusuni neno la Kristo likae ndani yenu kwa wingi, mnapofundishana na kupeana ushauri ninyi wenyewe kwa hekima yote, na mnapoimba zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho mkiwa na shukrani kwa Mungu mioyoni mwenu” (ktk Wakolosai 3:16, TLR). Mkazo unaoendelea wa Agano Jipya ni kwenye yale aliyoagiza Yesu, na yale aliyosema Yesu!

 

Yesu hakupendekeza tu kwamba waamini wamtii. Alisema kama ukweli thabiti kwamba, waamini wa kweli – wale wanaompenda Yeye – watamtii. Alisema hivi, “Kama mnanipenda, mtatii ninayoamuru” (ktk Yohana 14:15, TLR). Hapo tena, mkazo ni kutii yale ambayo Yesu aliamuru. Ona jinsi hayo yote yanavyofanana na 1Yohana 5:3, kwamba, “Huku ndiko kumpenda Mungu: kutii amri Zake” (TLR).

 

Petro naye akaongeza kwamba, waamini walichaguliwa ili watii. Aliwasalimu wasomaji wake kwa kuwaita wateule wa Mungu, “waliochaguliwa kulingana na kujua kabla kwa Mungu Baba, kwa njia ya kazi ya utakaso ya Roho, kwa ajili ya kumtii Yesu Kristo na kunyunyizwa kwa damu Yake” (ktk 1Petro 1:2, TLR). Petro aliyekuwa mtume kwa Wayahudi, hakusema waamini wanapaswa kuitii Torati ya Musa. Hapana. Anasema walichaguliwa “kwa ajili ya kumtii Yesu Kristo”.

 

Yesu alisisitiza kwamba alikuja kutoka kwa Mungu Baba Yake. Akatuambia asili ya mamlaka Yake. “Maana, Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu” (ktk Yohana 3:34, TLR). Akasema tena, “Mimi peke yangu siwezi kufanya chochote. Ninahukumu kulinganana ninavyosikia, na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu sitafuti kujipendeza mwenyewe, bali Yeye aliyenituma” (ktk Yohana 5:30, TLR). Akizungumza kuhusu Mungu Baba Yake, Yesu alisema hivi, “Siko hapa kwa sababu yangu mwenyewe, bali Yeye aliyenituma ni kweli. Ninyi hamumjui, lakini Mimi namjua kwa sababu nimetoka Kwake, Naye amenituma” (ktk Yohana 7:28, 29, TLR).

 

Akizungumzia kusudi Lake, Yesu alisema hivi: “Maana, sikushuka toka mbinguni kufanya mapenzi yangu bali mapenzi Yake Yeye aliyenituma” (ktk Yohana 6:38, TLR). Na katika Yohana 8:54-55, Yesu alisema hivi: “Baba Yangu, mnayedai ninyi kuwa ni Mungu wenu, ndiye anayenitukuza. Ingawa ninyi hamumjui, Mimi namjua. Ningesema simjui ningekuwa mwongo kama ninyi, lakini, ninamjua, na ninalishika neno Lake” (TLR).

 

Yesu alidhihirisha chanzo cha mafundisho Yake na jinsi ya kuthibitisha ukweli wake. “Mafundisho yangu si yangu. Yanatoka Kwake Yeye aliyenituma. Kama mtu yeyote atachagua kufanya mapenzi ya Mungu, atagundua ikiwa mafundisho yangu yanatoka kwa Mungu au kama ninasema mambo yangu mwenyewe” (ktk Yohana 8:26, TLR). … “Yeye aliyenituma anaaminika, na yale niliyosikia kutoka Kwake ninaiambia dunia” (ktk Yohana 8:28, TLR).

 

Yesu alizungumza dhahiri kabisa kwamba aliyokuwa anafundisha na kuagiza yalitoka kwa Mungu.

 

“Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo” (ktk Yohana 8:28)

“Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu, bali Baba aliyenipeleka, Yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. … Basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndiyvo ninenavyo” (ktk Yohana 12:49-50).

“Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake” (ktk Yohana 14:10).

“Neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka” (ktk Yohana 14:24).

“Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru, ndivyo nifanyavyo” (ktk Yohana 14:31).

 

Kwa kuwa Mungu alimwagiza Yesu cha kusema na kutenda, na kwa kuwa Yesu alitii kikamilifu kabisa, chochote alichosema Yesu na kufanya kilikuwa mapenzi ya Mungu. Kila fundisho, kila agizo, kila muujiza – vyote vilifanywa na Yesu kwa sababu Mungu Baba alimwagiza kufanya, Naye alifanya sawasawa na jinsi alivyoambiwa. Kila kitu ambacho Yesu alifanya na kusema kilikuwa mapenzi ya Mungu.

 

Yesu aliwaambia wafuasi Wake kwamba, wale tu watendao mapenzi ya Baba ndiyo watakaoingia katika ufalme wa mbinguni. Kwa ukweli huo huo angeweza pia kusema, “Wale tu wanaotii mafundisho Yangu na maagizo Yangu ndiyo watakaoingia katika ufalme wa mbinguni.” Tunafanya watu kuwa wanafunzi kwa agizo la Yesu na mapenzi ya Baba, “na kuwafundisha kuyatii yote ambayo Mimi nimewaamuru ninyi” (ktk Mathayo 28:30, TLR).

 

Je mchungaji na mwalimu wa Biblia, itakuwaje kwako kama ukiendelea kukataa kufanya yale ambayo Yesu anaamuru? Itakuwaje kwenu wazee? Maana ninyi ndiyo mnaotakiwa kuwa viongozi wa kiroho katika makanisa yenu!

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sura Ya Tatu

(Chapter 3)

 

Uasi Mkuu Wawekwa Wazi

(The Great Rebellion Exposed)

 

            Yesu alifundisha kwamba wale tu wanaofanya mapenzi ya Mungu ndiyo watakaoingia katika ufalme wa mbinguni. Kwa kuwa wokovu unategemea kufanya mapenzi ya Mungu, swali la kwanza linalotakiwa kuingia katika akili ya mtu ni hili: “Mapenzi ya Mungu ni nini?”

 

Tunajua jibu la swali hilo. Mapenzi ya Mungu ni kla neno na tendo la Yesu – mafundisho Yake yote na maagizo Yake. UASI mkuu ulio kanisani ni kushindwa na kukataa kwa viongozi wa kanisa, wachungaji na waalimu kutii amri ya Yesu itolewayo katika Agizo Kuu la Mathayo 28:19-20, kwamba

 

“Basi, nendeni na kufanya wanafunzi katika mataifa yote, mkiwabatiza katika jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kutii kila kitu nilichowaamuru ninyi” (TLR).

 

Amri ya moja kwa moja ya Yesu na mapenzi ya Mungu ni kwamba kanisa lifanye watu kuwa waafunzi kwa kuwafundisha wafuasi kutii kila kitu ambacho Yesu aliamuru. Je, wachungaji na waalimu wa kanisa wanafanya hivyo? Kulingana na ujuzi nilio nao mimi, hawafanyi. Nimeuliza wachungaji mara nyingi sana kwamba, “Mnafanya nini ili kuwafundisha watu kutii mafundisho na maagizo ya Yesu?” Mara zote hizo, wachungaji wanasimama kimya tu, kama paa aliyenaswa kwenye taa za gari. Hawafanyi chochote! Na huku Yesu alionya kwamba wale tu watendao mapenzi ya Mungu ndiyo watakaoingia katika ufalme wa mbinguni, nasi tunajua kwamba mafundisho na maagizo ya Yesu ni mapenzi ya Mungu. Agizo la kuwafundisha waongofu kutii mafundisho na amri za Yesu ni mapenzi ya Mungu. Sasa, itakuwaje kwa wachungaji na waalimu wenye kuamua kwa busara zao tu kwamba wao wanajua kuliko Bwana Yesu, na kwa sababu hiyo watafundisha na kuhubiri wanachotaka, bila ya kujali kwamba Mkuu wa kanisa aliagiza kile wanachopaswa kufanya? Je, ni watumishi waovu, wasiokuwa waaminifu?

 

Katika miaka elfu mbili na zaidi tangu Kristo alipotoa agizo hili kwa kanisa Lake, ungetazamia kwamba katika kulitii agizo hilo la kuwafundisha “kuyatii yote niliyowaamuru ninyi,” vingekuwepo vitabu maelfu kwa maelfu vya kujifunza Biblia, vilivyoandikwa hayo mafundisho na maagizo ya Yesu. Sivyo kabisa! Uchunguzi niliofanya kwenye mtandao kuhusu mafundisho na maagizo ya Yesu ulionyesha kwamba masomo yangu – www.bereanpublishers.com | Bible Studies | Teachings and Commands of Jesus -  ndiyo ya kwanza kuingizwa hapo. Kulikuwa na kutajwa tu kwa maneno au mafungu ya maneno, lakini sikuona masomo mengine yenye upana kuhusu mada hii. Niharakishe tu kusema kwamba sikufuatilia kila jibu kwenye mtandao, maana nilipata majibu milioni moja na nusu.

 

Ona kwamba Bwana Yesu aliwaamuru wafuasi Wake kufanya watu kuwa wanafunzi. Hakusema kwamba twende duniani kote na kufanya watu kuwa washirika. Lakini hilo ndilo lengo kuu la viongozi wengi wa makanisa siku hizi. Makanisa mengi yanasisitiza kumfanya mtu “aamue kwa ajili ya Kristo,” lakini Yesu hakuagiza hivyo. Uasi unaendelea.

 

Kitabu kiitwacho Wikipedia kinatoa tafsiri ya “mwanafunzi” katika Ukristo hivi:

 

Mwanafunzi ni mwenye kumfuata na anayejifunza kwa mkufunzi, mwalimu au yeyote mwenye hekima. Neno hilo pia linaweza kumaanisha wafuasi wa Yesu Kristo, katika dini.

 

Kwa nini iwe muhimu kwamba tufanye watu kuwa wanafunzi? Yesu alifundisha hivi: “Inatosha kwa mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake” (ktk Mathayo 10:25, TLR). Katika Luka 6:40, Yesu alisema hivi: “Mwanafunzi hayuko juu ya mwalimu wake, lakini yeyote aliyefundishwa kikamilifu atakuwa kama mwalimu wake” (TLR).

 

Yesu anasema kuhusu mwalimu gani hapo? Katika Mathayo 23:10, alituambia hivi: “Wala msiitwe ‘mwalimu’, kwa sababu mnaye Mwalimu mmoja tu, Kristo” (TLR). Yesu alisema kwamba kila ambaye amfundishwa kikamilifu atakuwa kama mwalimu wake – yaani, kama Kristo. Je, hili ni muhimu? Mtume Yohana aliona hivyo. Katika 1Yohana 2:6, aliandika hivi: “Yeyote anayedai kuwa anakaa ndani Yake lazima aenende kama Yesu alivyoenenda” (TLR). Katika Warumi 8:29, Paulo naye alifanya jambo hili kuwa swala la wokovu wakati aliposema, “Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.” Ndiyo! Mungu alichagua tangu asili hali ya wale ambao wangeokolewa: Lazima wafananishwe na mfano wa Mwana Wake!

 

Je, watu wanapaswa kufundishwaje kikamilifu ili wawe kama Yesu? Yesu aliutambia cha kufanya – tunatakiwa kuwafundisha kuyatii mafundisho Yake na maagizo au amri Zake. Yeye aliyatii kikamilifu kabisa yale maagizo aliyotupa. Tunapojifunza kutii amri Zake tunakuwa kama Yesu – ambacho ndicho tunacholazimika kufanya kama tunataka kufananishwa na mfano Wake na kuenenda kama Yeye alivyoenenda. Tunapotii mafundisho na amri za Yesu, tunafanya mapenzi ya Mungu – kile kitu ambacho lazima tufanye kama tunataka kuingia katika ufalme wa mbinguni.

 

Haya ni mawali nyeti kabisa ya wokovu. Mungu aliweka sharti kwa ajili ya wale ambao wataokolewa: lazima wafananishwe na mfano wa Mwana Wake, yaani Bwana Yesu. Nini alama au tabia ya msingi kabisa ya Yesu? Yeye alikuwa mtiifu kabisa kwa Baba Yake, akisema na kufanya yale tu ambayo Baba Yake alimwambia aseme na kufanya. Vivyo hivyo, sisi nasi tunaweza kufananishwa na mfano wa Yesu na kufanya mapenzi ya Mungu – kitu kinachotakiwa kwa watakaoingia katika ufalme wa mbinguni – kama tu tutajifunza na kutii mafundisho na amri za Yesu.

 

Kulingana na maswala hayo mawili ya wokovu, mamilioni wasiohesabika hawataingia mbinguni kwa sababu wachungaji na waalimu wao walimwasi Bwana Yesu, wakikataa kuwafundsiha watu kutii kila kitu alichoamuru. Matokeo yake ni kwamba, kwa sababu hao mamilioni hawakufundishwa kutii mafundisho ya Yesu na maagizo Yake, watashindwa kufanya mapenzi ya Mungu, na hawataruhusiwa kuingia katika ufalme wa Mungu.

 

Jiulize mwenyewe maswali machache. Kama alivyoshauri Paulo, “Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe” (ktk 2Wakor. 13:5). Je, kanisa lenu linawafundisha waongofu wapya kutii yote ambayo Yesu aliamuru? Je, wewe binafsi umewahi kufundishwa kutii mafundisho na amri za Yesu? Je, wewe mwenyewe umejifunza mafundisho na amri za Yesu na kujitolea kutii kila kitu? Je, unafananishwa na mfano wa Yesu? Je, unatenda mapenzi ya Mungu kwa kutii mafundisho na amri za Yesu?

 

Inasikitisha sana kwamba ni wachache tu watakaokuwa wameipata njia ya wokovu kupitia kwa wachungaji wa makanisa yao, waalimu na viongozi. Kinyume chake ni kwamba, wale ambao wamejitafutia kwa bidii kweli ya Neno la Mungu na kuamua kumtii Bwana Yesu ndiyo tu watakaofanya mapenzi ya Mungu na ndiyo watakaoingia katika ufalme wa mbinguni.

 

Mafundisho na amri za Yesu hutuonyesha jinsi ya kuishi katika ufalme tofauti – ule ambao Bwana Yesu Kristo ndiye Mfalme wake. Tukisha kuwa wafuasi wa kweli wa Yesu na kuamua kumtii, tunazaliwa mara ya pili katika ufalme wa Bwana (Yohana 14:15-17; ona pia Matendo 5:32) na Mungu anakuwa Baba yetu (Yohana 1:12-13; ona pia Mathayo 23:9). Hapo tunakuwa wageni katika dunia hii. Mimi na Dar tunajua dhana hiyo vizuri sana. Tulipohamia nchi ya New Zealand, tulikuwa wageni huko. Tuliacha kuwa wageni tulipofanyika raia wa New Zealand. Vivyo hivyo, kabla ya watu kufikilia imani yenye kuokoa katika Yesu Kristo, wao ni raia wa dunia hii. Wanapofikia imani yenye kuokoa katika Bwana wetu Yesu Kristo, wanakuwa raia wa ufalme Wake na wageni katika dunia. Petro alilifafanua hili vizuri sana katika 1Petro 2:11, kama ifuatavayo: “Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho”. Waebrania 11 inasimulia habari za watu walioishi kwa imani. Katika Waebrania 11:13 tunaambiwa hivi: “Watu hao wote walikuwa bado wanaishi kwa imani walipokufa … nao walikiri kwamba walikuwa wapitaji na wasafiri hapa duniani” (TLR).

 

Watu wengi wanasema kwamba Mungu anakusudia waipende na kuifurahia dunia hii tunayokaa ndani yake. Je, Neno la Mungu ndivyo linavyosema? Yakobo alituambia hivi, “Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu”  (ktk Yakobo 4:4). Mtume Yohana naye akaongezea hivi: “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake” (ktk 1Yohana 2:15).

 

Kisha, Yohana anaeleza ni kwa nini tusiipende dunia, kama ifuatavyo: “Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havfitokani na Baba bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele” (ktk 1Yohana 2:16-17).

 

Kama wewe ni mchungaji au mwali, unahubiri na kufundisha kitu gani katika kanisa lako? Unajali kiasi gani kuhusu wokovu wa wale waliotiwa chini ya uangalizi wako? Je, mawazo ya mhubiri maarufu aitwaye C.H. Spurgeon, aliyotoa miaka mia moja iliyopita, yanakuhusu?

 

“… Unaweza kuingia katika kanisa la Kikatoliki siku hizi, na kusikia ujumbe mzuri tu kutoka kwa kasisi kama ambao utasikia mara nyingi tu kutoka kwa mchungaji wa KiProtestanti, kwa sababu hagusi maeneo yenye utata, wala kusema kitu muhimu kuhusu dini yetu ya KiProtestanti. Angalia pia kwamba katika vitabu vyetu vingi hakuna mwelekeo sana wa itikadi sahihi! Waandish ni kama wanadhani kwamba ukweli hauna thamani sana kuliko udanganyifu; na kwamba, kwa habari ya itikadi tunazohubiri, si kitu kwamba ni zipi; wakiendelea kushikilia kwamba ‘Yeye ambaye maisha yake yako sawa hawezi kukosea’.

 

“…Oo! Laiti tungekuwa na baadhi ya wale wahubiri wa zamani wa KiSkochi! Hao wahubiri walifanya wafalme kutetemeka. Hawakuwa watumwa wa mtu yeyote. Wao ndiyo walikuwa mabwana popote walipokwenda, kwa sababu kila mmoja alisema, ‘Mungu kanipa ujumbe; na uso wangu ni kama gumegume mbele za watu. Nitasema kile ambacho Mungu kanituma kusema.” Kama Mika, walisema, ‘Kama Bwana Mungu wangu aishivyo, chochote Mungu wangu atakachoniambia, ndicho nitakachosema.’

 

Viongozi wa kanisa hukimbilia kwenye Kanisa la Willow Creek la Bill Hybel, au Kanisa la Saddleback Community la Rich Warren kujifunza mbinu za kisasa za kuuza mambo ili waweze kuwa na makanisa makubwa, lakini wanapuuzia mapenzi ya Mungu yaliyo dhahiri kabisa kwamba wafanye nini ili kujenga kanisa Lake.

 

Hatuna haja ya kubishana kuhusu ukweli kwamba walio wengi katika Ukristo wanaasi dhidi ya Bwana wao kwa kukataa “kuwafundisha kuyatii yote niliyowaamuru”. Kama wewe ni mchungaji wa kanisa, mwalimu au kiongozi, jibu swali hili: Je, unafanya watu kuwa wanafunzi kwa kuwafundisha kuyatii yote ambayo Yesu aliagiza? Kama hapana, kwa nini hufanyi hivyo?

 

Pengine utaona kwamba nimekuwa mgumu sana kwa wachungaji, waalimu, na viongozi wa kanisa. Sivyo. Ninarudia tu kusema yale ambayo Bwana Yesu alifundisha na kuagiza. Kwani huoni mambo hayo? Ukisema “Nayaona!” basi kwa nini huyafanyi? Hukumbuki Yesu akiuliza, “Kwa nini mnaniita ‘Bwana, Bwana’ na hamfanyi yale ninayosema?” (ktk Luka 6:46, TLR)

 

Yesu alisimulia mfano wa mtumishi mwaminifu na mwenye busara, na mtumishi mwingine aliyekuwa mwovu. Ona kwamba wote walikuwa watumishi wa huyo bwana. Akasema hivi:

 

“Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? Heri mtumwa yule ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. Amin nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, ‘Bwana wangu anakawia’; akaanza kuwapiga wajoli wake na kula na kunywa pamoja na walevi; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, atamkata vipande viwili na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno” (ktk Mathayo 24:45-51).

 

Katika mfano huu, mtumwa mwovu ana mamlaka ya kuwasimamia watumwa wale wengine, kama ambavyo mtumwa mwaminifu na mwenye akili alivyo. Yule mwaminifu anaendelea kuwapa chakula wale watumwa wengine kwa wakati uliokubalika. Bwana anampa thawabu.

 

Lakini yule mwovu alichoka kutumika kama bwana wake alivyomwagiza. Akaanza kuwapiga wale watumwa wenzake na kula na kunywa na walevi. Yesu akasema, wakati bwana wake atakaporudi atamkata huyo vipande na kumweke fungu lake pamoja na wanafiki, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. Adhabu inayotajwa hapa ni mbaya kuliko ile inayopatikana katika mafundisho mengine au mifano anayotoa Yesu. Maneno yanayo-ongezeka ni haya: “Atamkata mtumwa huyo vipande vipande.”

 

Je, huyo mtumwa mwovu ni mfano wa wale wachungaji, waalimu na viongozi wa kanisa ambao si waaminifu, walio waasi dhidi ya Bwana Yesu na maneno Yake? Je, mtumwa mwaminifu ni mfano wa wale wachungaji, waalimu na viongozi ambao kwa uaminifu kabisa waliwalisha watumishi wengine chakula chao – yaani maneno, mafundisho na amri za Yesu, Bwana wao?

 

Kama mchungaji, kiongozi wa kanisa au mzee, sehemu hii inaweza isiwe na maana sana kwako kama inavyopaswa kwa sababu unaweza kuwa umeleweshwa kabisa Ukanisa kiasi cha kutoweza kutambua hatari ya milele ya uasi wako. Mafundisho mengi ya uongo yametokea kwa sababu ya kutokujua mafundisho ya Yesu na amri Zake, yanayodai kwamba Wakristo hawafungwi na sheria iwayo yote. Je, wachungaji, waalimu, na viongozi wa kanisa watahukumiwa kwa ajili ya uasi wao? Hicho ndicho tunachotaka kutazama sasa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sura Ya Nne

(Chapter 4)

 

Je, Viongozi Wa Kanisa Watahukumiwa?

(Will Church Leaders Be Condemned?)

 

Wachungaji, waalimu na wazee wako mahali pagumu. Wengi wao wamekuzwa katika utamaduni wa Kikristo ambao haukuwa na mafundisho kuhusu haja ya kumtii Yesu kama Bwana. Hata vyuo vikuu vya Kikristo waliohudhuria wale ambao sasa ni wachungaji bila shaka havikufundisha kwamba Yesu ni Bwana, na maana yake katika maisha ya mtu – kwamba ni kuwa mtumishi ambaye kwa uaminifu kabisa anatii kila amri na fundisho la Yesu. Wachungaji wengine pengine hata hawakujifunza kwamba wale wasiotii ni watumishi wasiokuwa waaminifu (yaani, waovu).

 

Ingawa kweli haisikiki hivyo kutokana na maneno ambayo nimetumia, ninawapenda sana wachungaji, tena kipekee sana. Wengi wamekuwa rafiki zangu hata nyakati ambapo hatukukubaliana katika maswala ya itikadi. Wachungaji wengine wamelemewa na kazi nyingi sana, kiasi kwamba hata hawana muda wa kuomba na kujifunza Neno, kama tu wale washirika wao.

 

Pamoja na hayo, huo si utetezi wa kutosha kwao. Kwa kawaida, wachungaji ni watu waliosoma, ambao wamehudhuria vyuo vikuu vya Biblia na kujifunza Maandiko katika lugha za asili. Badala ya utetezi, inakuwa kitu kisichoeleweka kuwa na uwezo wa kuifahamu kweli kwa njia ya elimu ya mtu na taaluma yake, halafu kuipuuza au kuepuka kwa sababu za kibinafsi au za kikazi. Haishangazi kwamba wapo wengi wanaopinga kwa nguvu zote na kwa sauti kubwa ukweli kwamba Yesu ni Bwana. Shetani mwenye anachukia sana kwamba Yesu ni Bwana. Inasikitisha pia kwamba baadhi ya viongozi wa kanisa wanakubaliana na watu kama hao, badala ya kuinuka na kumtetea Bwana wao na Mkuu wao.

 

Kwa kutumia Maandiko tu, unaweza kufikia uamuzi wako binafsi juu ya mwisho wa milele wa viongozi wengi wa kanisa. Kwanza, hebu tutambue kwamba wachungaji na waalimu watahukumiwa kwa ukali zaidi (Yakobo 3:1). Hiyo ni sawa kwa sababu, wale wanaowahubiria na kuwafundisha wanaamini kwamba mchungaji wao hujifunza Neno la Mungu kwa bidii sana na kwa ukamilifu kabisa kuliko wao wanavyoweza kufanya. Basi, hiyo huwafanya kuamini sana anachokisema. Tena, wachungaji wengi huonyesha ujuzi wao katika Kiyunani na Kiebrania ili kujaribu kuonyesha kwamba wanatoa maana sahihi zaidi na ya uhakika ya andiko husika.

 

Katika miaka kumi na tano iliyopita nimeona ongezeko la matumizi ya neno Bwana kwa habari ya Yesu, lakini sijaona ongezeko lolote katika juhudi za kufafanua maana yake katika maisha ya aaminiye, au kuhusu hitaji la kumpokea Yesu kama Bwana katika maisha ya mtu ili apate wokovu.

 

Yesu alisema, tusipoamini kuwa Yeye ndiye tutakufa katika dhambi zetu (Yohana 8:24). Je, alisema Yeye ni nani? Yesu alisema, “Mnaniita ‘Mwalimu’ na ‘Bwana’, na ni sawa maana ndivyo nilivyo” (ktk Yohana 13:13,TLR).

 

Jina “Bwana” linapotumiwa kwa Yesu linamtaja kama Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana (Ufunuo 19:16), ambaye ana mamlaka yote mbinguni na duniani (Mathayo 28:18). Itikio sahihi tu kwa Bwana Yesu ni kumtii. Ni kituko kudai kwamba Yesu ni Bwana, halafu kuacha kumtii. Bwana Yesu ana haki ya kutazamia na kudai utii kutoka kwa wanaodai kuwa wafuasi Wake, na hasa kutoka kwa wale wanaodai kwamba wanahubiri na kufundisha katika jina Lake.

 

Je, Yesu alitazamia utii? Kabisa kabisa! Katika Luka 6:46 aliuliza, “Kwa nini mnaniita ‘Bwana, Bwana’ na hamfanyi ninayosema?” (TLR). Hata wakati akiwepo katikati yao, bila shaka kuna walioamua kumwita Yesu Bwana kuliko kumpokea kama Bwana wa maisha yao.

 

Je, kumtii Yesu kama Bwana ni swala la wokovu? Kabisa! Inabidi tutazame tena Mathayo 7:21, ambapo Yesu alisema hivi: “Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.” Wachungaji wanaweza kutamka maneno “Bwana, Bwana” lakini hawataingia mbinguni mpaka watende mapenzi ya Baba yake Yesu, aliye mbinguni.

 

Nini mapenzi ya Mungu kwa ajili ya waaminio wa Agano Jipya? Yesu alisema kwamba kila kitu alichofanya na kusema akiwa hapa duniani alikuwa ameambiwa na Baba Yake aseme na kufanya (ktk Yohana 8:28; 12:49-50; 14:10; 14:24; 14:31). Kwa hiyo, kila kitu ambacho Yesu alisema na kufanya kilikuwa mapenzi ya Mungu. Je, unashangaa kwamba Yeye ndiye mwanzo wa wokovu kwa wote wanaomtii? (Ona Waebrania 5:9.)

 

Narudia tena kukumbushia amri moja ya Bwana Yesu ambao inaonekana kupuuzwa kabisa katika Ukanisa. Ni ile amri ambayo Yesu alitoa kwa wafuasi Wake waliotakiwa kulijenga kanisa Lake. Katika Mathayo 28:19-20, Yesu alisema, “Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi.”

 

Yesu alitupa mafundisho na amri mia nyingi sana. Katika somo langu la Biblia juu ya mafundisho na amri za Yesu, kuna mada 382 tofauti. Kila moja Yesu alipewa na Baba Yake. Kila fundisho na amri ni mapenzi ya Mungu. Kulingana na Mathayo 7:21, hakuna yeyote kati yetu atakayeingia katika ufalme wa mbinguni bila ya kufanya mapenzi ya Mungu.

 

Kila mtu anayehudhuria kanisa la Kikristo anapaswa kusikia akiambiwa kutii mafundisho na amri za Yesu, huku kila amri ikitajwa na kufafanuliwa vizuri. Je, hayo yanafanyika? Kama wewe ni mchungaji au mwalimu, umewahi kufanya hivyo? Je, katika mahubiri yako, hiyo ndiyo mada, kama Yesu alivyoagiza? Je, wakati wote unatambua kwamba wale walio kanisani mwako wasiojua na wasiotii amri za Yesu hawataingia kamwe katika ufalme wa Mungu?

Na kama wewe ni mlei (au mshirika wa kawaida), umewahi kufundishwa mafundisho na amri za Yesu? Je, unafahamu vema amri za Yesu kiasi cha kuteka mateka kila fikra na kuitiisha kwa Kristo? (Ona 2Wakor. 10:5). Kama hujafundishwa hivyo kanisani kwako, lazima ujifunze na kujipatia maarifa hayo wewe mwenyewe. Jifunze vitabu vya Injili. Kila amri na fundisho la Yesu hukufundisha jinsi ya kuishi kama sehemu ya ufalme wa Yesu ili uweze kuwa tayari kuishi katika ufalme wa mbinguni. Hizi ndizo habari njema za Injili – kwamba, Mungu kwa njia ya Yesu alitufunulia sisi mapenzi Yake ili tuweze kupatanishwa Naye na kuishi pamoja Naye mbinguni, milele yote. Ona Wakolosai 1:21-23.

 

Kitatokea kitu gani kwa wale wasiojua na wasiotii? Paulo alituambia katika 2Wathes. 1:8-9 kwamba, “Yeye [Mungu] atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu. Wataadhibiwa kwa uharibifu wa milele na kufungiwa nje ya uwepo wa Bwana na utukufu wa uwezo Wake …” Yaani, ni mambo makubwa hayo, tena ya milele.

 

Vipi kuhusu wale ambao ni wachungaji wetu na waalimu, wanaoshindwa (au kukataa) kuwafundisha washirika wao kutii kila kitu alichoamuru Yesu? Katika sheria, kupuuza kitu bila kujali ni sawa na tendo la makusudi. Basi, maneno ya Waebrania 10:26 yanapaswa kuleta hofu katika mioyo ya wale ambao kwa makusudi kabisa wanakataa (au kupuuza) kutii amri ya Yesu ya kuwafundisha watu kutii yote aliyoamuru. Yanasema hivi: “Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi, bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.” Ni dhambi kushindwa au kukataa kufanya watu kuwa wanafunzi kwa “kuwafundisha kutii yote niliyowaamuru ninyi” (ktk Mathayo 28:20, TLR).

 

Wachungaji wengi kwa haraka watapinga yote niliyosema wakitoa hoja hii: “Mimi si adui wa Mungu!”

 

Kujitetea kwako si kitu sana. Unachotakiwa kujali ni hiki: Mungu anafikiri nini juu yako? Si jinsi wewe unavyojifikiria mwenyewe. Katika Mathayo 7:22-23 kuna lugha ya kutisha sana. “Wengi wataniambia siku ile: ‘Bwana, Bwana! Hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?’ Ndio nitawaambia dhahiri: ‘Sikuwajua ninyi kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu’!”

 

Je, yawezekana kwamba Yesu alikuwa anasema kuhusu wachungaji na viongozi wa kanisa hapa? Hawa walikuwa watu walio-onekana kuwa na upako maalum sana: walitabiri, walitoa pepo na hata kufanya miujiza mingi sana. Je, Bwana Yesu alipendezwa nao? Hapana. Anasema Yeye hakuwajua kamwe, na anawaita watenda maovu (au, wanaopinga kushika sheria).

 

Je, kuna mchungaji yoyote au mwalimu anayeweza kudai kutokujua amri ya Yesu? Je, hawafanyi dhambi ya makusudi kwa kukataa kwao kuwafundisha wale waliowekwa chini ya uangalizi wao kutii yote ambayo Yesu aliwaagiza wanafunzi Wake? Je, wachungaji wanaokataa kutii amri hiyo na wanaoendelea kushindwa kufanya hivyo si watenda dhambi wa makusudi kabisa, kama inavyosemekana katika Waebrania 10:26?

 

Je, wachungaji wengi leo hawafanani na Mafarisayo na waalimu wa Torati wa siku za Yesu? Yesu aliwaonya sana. “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akisha kufanyika, mnamnfanya kuwa mwana wa Jehanamu mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.” Mafarisayo walikuwa na shauku kwa ajili ya Torati ya Musa. Lakini Yesu aliwaita wana wa Jehanamu na kusema kwamba wafuasi wao wangekuwa wana wa Jehanamu mara mbili kuliko wao.

 

Je, hiyo ni lawama isiyostahili kwa wachungaji wa siku hizi? Vipi kuhusu wale wenye kufundisha itikadi za uongo na kushindwa kutii amri ya Yesu kuhusu kinachowapasa kufundisha?

 

Ndugu Roger Oakland aliandika “Ziara Yangu Kwenye Kongamano la Kufikiri Tena” hivi karibuni, kutokana na mambo aliyopata na kuona baada ya kuhudhuria Kongamano liitwalo Rethink: New Perspectives From Global Influences lililofanyika Januari 17 hadi 19 mwaka huu wa 2008, lililoandaliwa na Erwin McManus na Robert Schuller. Ukitaka kujisomea mwenyewe makala yake kamili, tazama kwenye tovuti yake, www.understandthetimes.org. Ndugu Roger aliandika kwamba, wasemaji walisisitiza kwamba Ukristo lazima utazamwe upya na kupangwa upya kama jina la Yesu Kristo litaendelea kudumu hapa duniani kwa kuwa sasa tumeingia karne ya ishirini na moja. Roger anasema, Robert Schuller alitoa maelezo kwa kifupi kuhusu mafanikio yake. Schuller alieleza jinsi alivyofurahi kupata nafasi ya kutazama nyuma na kuona viongozi wa hali ya juu sana ambao amewalea, akiwemo Bill Hybels, mchungaji mwanzilishi wa kanisa la Willow Creek, kanisa linalojisifia kuwa ‘rafiki wa watafutaji’, Askofu Charles Blake wa kanisa liitwalo Church of God in Christ lenye washirika milioni sita, na mchungaji Rick Warren ambaye ni mwanzilishi wa kanisa linalo-ongozwa na kusudi, na maisha yanayo-ongozwa na kusudi (The Purpose Driven Church, The Purpose Driven Life).

 

Kana kwamba alikuwa anatazama mbele katika karne zifuatazo, Yesu aliuliza hivi: “Je, Mwana wa Adamu atakaporudi, ataikuta imani duniani?” (ktk Luka 18:8, TLR). Unapotafakari kuhusu Kongamano la Rethink na kuhusu mambo yatakayosemwa katika sura zinazofuata, pengine hata wewe utaanza kushangaa kama imani yenye kuokoa haijaanza kukosekana hapa duniani.

 

Yesu alisema hivi, “Nawaambia kweli, hakuna mtumwa aliye mkuu kuliko bwana wake, wala mjumbe si mkuu kuliko yeye aliyemtuma. Kwa kuwa mnajua mambo haya sasa, mtabarikiwa kama mtayatenda” (ktk Yohana 13:16-17, TLR). Je, wachungaji wengi si wanajaribu kuwa wakuu kuliko hata Bwana wao? Kama wachungaji ndiyo wajumbe wanaotakiwa kutangaza Injili, je, wameamua kwamba wanahitaji kuboresha ujumbe (Injili yenyewe) kwa sababu haufai katika kile wanachokiona wao kuwa ni mtazamo mpya?

 

Ingawa Yesu alisema, “Yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kamwe” (ktk Marko 10:15, TLR), tunawaona viongozi wengi sana wa kanisa wenye kutangaza injili mpya – nyingine kabisa – wakiamini bila shaka kwamba wao wanajua zaidi ya Bwana Yesu, na kwamba wanahitaji kuboresha mafundisho Yake, mpaka kufikia mahali pa “kuyafikiri upya” na “kuyaunda upya”.

 

Sasa – hebu tutazame Kutokushika Sheria katika kanisa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sura Ya Tano

(Chapter 5)

 

Uasi Dhidi Ya Sheria Ya Kristo

(Rebellion Against the Law Of Christ)

 

Tuliporudi Marekani kutoka New Zealand, Dar na mimi tulianza kuabudu katika kanisa moja kubwa sana mjini Scottsdale, Arizona. Tukakuta kwamba kuna mabadiliko makubwa sana kitheolojia katika miaka ile sita tuliyokuwa hatupo. Kabla ya kuhamia New Zealand, nilijua kwamba mchungaji kiongozi alikuwa anakubaliana na fundisho la uongo kwamba kuna usalama wa wokovu bila masharti yoyote, japo hakuwa anasema. Tuliporudi, mchungaji kiongozi akahubiri Jumapili moja kuhusu Wakristo wazinzi na walawiti, akihakikishia kanisa lote kwamba wokovu wa watu hao haukuwa unaathirika kutokana na matendo yao. Kupinga Sheria kulikuwa kumeteka kanisa na itikadi zake kikamilifu kabisa.

 

Kama tutakavyo-ona, fundisho la Kupinga Sheria limeenea sana, na limezaa watoto wake pia – itikadi nyingi za uongo ambazo zitawavuta mamilioni wengi wasiende mbinguni, bali waende Jehanamu. Tutatazama baadaye baadhi ya itikadi hizo za uongo ambazo ni maarufu kwa sasa.

 

Asili ya na fundisho hili ni maneno mawili ya Kiyunani – “anti” na “nomos”. Maana ya anti ni kuwa kinyume na, kupinga. Maana ya nomos ni sheria, kanuni, kiwango, sheria inayosimamia maisha au mwenendo wa kiadili. Ukiunganisha yote hayo tunapata maana ifuatayo: kutokuwepo na utawala wa sheria; kutokuwepo na sheria, kupinga au kuwa kinyume na sheria za aina yoyote, na viwango na kanuni za kuongoza maadili katika mwenendo.

 

Mafundisho na amri za Yesu ni kuhusu viwango na kanuni za kuongoza maadili. Paulo aliyaita mafundisho ya Yesu na amri Zake kuwa ni “sheria ya Kristo” (ktk 1Wakor. 9:21 na Wagalatia 6:2). Amri nyingi na mafundisho ya Yesu ni maswala muhimu kwa ajili ya wokovu, yaani, mtu lazima afanye, au asifanye, kinachosemwa na amri na maagizo hayo ili apate wokovu. Ni wazi kwamba kwa watu wanaopinga kuwepo kwa sheria zozote, amri hizo ni ngumu kabisa kuzipokea. Wao hutoa hoja kwamba amri za Yesu si kwa ajili ya siku hizi na wakati huu, na kwamba zilikuwa kwa ajili ya Wayahudi tu, au kwamba kwa sasa tuko chini ya neema, si sheria.

 

Kutokea kwa fundisho hilo la kupinga sheria husaidia kueleza sababu ya viongozi wengi wa kanisa, wachungaji na waalimu kupuuza mafundisho na amri za Yesu. Kulingana na imani zao, wao hawako chini ya sheria aina yoyote au kanuni zinazosimamia maadili. Kwa hiyo, kwa nini wasumbuke kufundisha waamini wapya watii mafundisho ya amri za Yesu? Badala yake, wao wanawasisitizia waamini wapya kwamba wanaokolewa kwa neema, na kwamba matendo yao au mwenendo wao binafsi havitaathiri wokovu wao.

 

Miaka mingi iliyopita nilibahatika kuzungumza mada hii na mchungaji mmoja mstaafu, ambaye wakati huo alikuwa anafundisha katika Shule ya Uzamili ya Theologia huko Pasadena, California. Akaniuliza, “Hivi kweli unajaribu kutii mafundisho na amri za Yesu?” Nikajibu, “Naam!” Akaniambia, “Hayo si kwa ajili ya wasiokuwa Wayahudi. Hayo ni kwa ajili ya Wayahudi!” Nikamjibu, “Hebu soma Agizo Kuu. Linasema watu wafanywe kuwa wanafunzi katika mataifa yote. Haisemi chochote kuhusu Wayahudi. Na inasema hao watu wafundishwe kutii yote ambayo Yesu aliamuru.” Hakujibu hilo.

 

Katika sehemu mbalimbali za Maandiko, dhana ya kupinga sheria inaonekana. Mara nyingi inajitokeza kwa maneno kama “uovu”, “kutokuwepo na haki” au “mkosaji”. Katika Mathayo 7:23 Yesu aliwaambia hivi, “Sikuwajua ninyi. Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu!” Yaweza kutafsiriwa kwa usahihi pia hivi: “Ondokeni kwangu, ninyi msiofuata sheria yoyote (au, msiotii sheria)!”

 

Fungu hilo ni la kutisha sana kwa sababu watu wanaozungumza na Yesu wakati wa hukumu wanasema, “Bwana! Bwana! Hatukutabiri kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo na kufanya miujiza mingi?” Bila shaka hawa watu walifikiri wao ni Wakristo wa hali ya juu, wakitabiri, wakitoa pepo na kutenda miujiza. Si ajabu walikuwa wanaamini kwamba wameokoka na kwamba wanakwenda mbinguni. Haikuwa hivyo. Walikuwa wamehukumiwa. Kwa nini? Yesu alikwisha waambia sababu katika Mathayo 7:21 – “Si kila mtu aniambiaye ‘Bwana! Bwana!’ atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye tu atendaye mapenzi ya Baba Yangu aliye mbinguni.” Nimekazia tena na tena hoja hiyo kwamba kila kitu alichofundisha Yesu na kuagiza ni mapenzi ya Mungu. Bila shaka hawa “Wakristo wa hali ya juu” waliotabiri, kufukuza pepo na kufanya miujiza walidai pia kwamba hawako chini ya sheria yoyote, kwamba, wameokolewa kwa neema. Si ajabu walifundishia pia uongo huo maarufu sana kwa wengine waliokuwa chini ya uangalizi wao, wakiendeleza hali hiyo ya kupinga sheria kwa wafuasi wao.

 

Mwandishi maarufu aitwaye A.W. Tozer alifafanua itikadi hiyo ya kupinga sheria katika kitabu chake kiitwacho Paths To Power. Alisema hivi: “Ukristo halisi katika siku zetu umeingiliwa sana na yule adui wa haki wa siku za kale: Kupinga Sheria. Fundisho la Kupinga Sheria linafafanuliwa kirahisi sana hivi: Tunaokolewa kwa neema tu; matendo hayana nafasi katika wokovu; mwenendo ni matendo, basi, hayana umuhimu. Tunachofanya si kitu mradi tunaamini kilicho sahihi. Talaka kati ya fundisho na mwenendo inakamilika. Swala la dhambi limeshughuliwa na msalaba. Mwenendo uko nje ya imani na hauwezi kuja katikati ya aaminiye na Mungu. Kwa ufupi, hilo ndilo fundisho la Kupinga Sheria.

 

Basi, limeingia na kupenya ndani kabisa ya Ukristo halisi wa siku hizi kiasi kwamba unakubalika na wana dini wengi kwamba ndiyo kweli ya Mungu. Kupinga Sheria ni itikadi ya neema inayobebwa na hoja ambayo si sahihi mpaka kufikia upumbavu. Itikadi hii inachukua lile fundisho la kuhesabiwa haki kwa imani na kulipotosha kabisa.”

 

Ndugu Tozer kwa usahihi kabisa anafafanua Kupinga Sheria kuwa ni fundisho lenye kujihusisha tu na kile anachoamini mtu, si matendo yake. Wakati Biblia inaposema habari za hukumu ya Mungu, haiweki kamwe msingi wake kwenye anachoamini mtu. Katika Ufunuo 20:12-13, Yohana alisimulia alichokiona pale kwenye hukumu ya kiti cha enzi cheupe, kama ifuatavyo: “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliokuwao ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.”

 

Akizungumza kuhusu siku za mwisho, Yesu alisema, “Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake” (ktk Mathayo 16:27). Halafu tena alisema hivi, “Tazama naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo” (ktk Ufunuo 22:12).

 

Paulo akasema hivyo hivyo katika Warumi 2:5-6. “Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu, atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.” Katika Warumi 14:12, Paulo aliandika hivi, “Basi ni hivyo. Kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.” Paulo aliandika hivi kwa Wakorintho, “Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya” (ktk 2Wakor. 5:10).

 

Mpaka hapa, hayo yote ni kinyume kabisa na fundisho la Kupinga Sheria, sivyo? Hatuhukumiwi kwa sababu ya tunachoamini, bali kulingana na yale tuliyotenda.

 

Mafundisho mengine mengi katika Maandiko yanaunga mkono hiyo hoja. Katika Yohana 15:1-2, Yesu alisema, “Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangulisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.” Kulingana na mstari huu, Baba atawakatilia mbali wanaopinga Sheria, watoke kwa Bwana Yesu, kwa sababu wao hawazai matunda yoyote.

 

Yesu alisimulia ule mfano wa kondoo na mbuzi katika Mathayo 25:31-46. Kwa mara nyingine tena, mantiki ni wakati wa hukumu. Yesu akaeleza hivi, “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake. Na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi. Atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.”

 

Yesu anasimulia jinsi watu watakavyohukumiwa, kwa maneno yafuatayo: “Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, ‘Njooni mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu. Kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia’.”

 

Wale wenye haki (walioko kuumeni Kwake) wanamwuliza, “ ‘ Bwana! Ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia’?”

 

Ndipo Yesu anapofafanua msingi wa hukumu ile, hivi: “Na Mfalme atajibu akiwaambia, ‘Amin nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi’.”

 

Ni kinyume kwa wale walio upande Wake wa kushoto – mbuzi. “Kisha atawaambia na wale walioko mkono Wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake’.” Halafu anaendelea kusema kwamba wao hawakumtendea kitu chochote, wala hawakuwatendea mmojawapo wa ndugu Zake aliye mdogo. Yesu anamalizia hivi: “Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele, bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.”

 

Kwa maoni yako, ni nani unayedhani hakufanya chochote? Bila shaka ni yule anayepinga Sheria ambaye anatumainia kile anachoamini tu; yeye anafikiri mwenendo wake hauna maana. Anapinga matendo, mara nyingi sana akidai kwamba wale wenye matendo (na ambao ni watii) wanajaribu kupata wokovu kwa matendo. Hapo tena, kinyume chake ndiyo ukweli. Tunachodai kuamini si cha muhimu sana wakati wa hukumu. Tutahukumiwa kulingana na tuliyofanya.

 

Yesu akahusisha mwenendo na na uhusiano Naye. Katika Mathayo 12:46 Yesu alisema, “Kila atendaye mapenzi ya Baba Yangu wa mbinguni ni ndugu yangu na dada yangu na mama yangu” (TLR). Katika Yohana 15:14 alisema, “Ninyi ni rafiki zangu mkitenda ninayowaamuru.” Mweendo wetu unaonyesha tunachoamini. Je, tuna nafasi yoyote ya wokovu kama si rafiki au ndugu au dada au mama yake Bwana Yesu? Hapa tena Yesu aliweka masharti ya kufanya mapenzi ya Mungu na kutenda alichoagiza.

 

Wapinga Sheria mara nyingi hujidhania kwamba ni wafuasi wa Paulo. Lakini, Paulo huyo huyo alifundisha kwamba mwenendo ni muhimu sana. Katika Wagalatia 5:19-21, Paulo alionya hivi: “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya: uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo. Katika hayo nawaambia mapema kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.” Hapa, Paulo anasaema waziwazi kabisa kwamba mwenendo usiofaa utamnyima wokovu mtu atendaye hayo.

 

Vivyo hivyo katika 1Wakor. 6:9-11, Paulo alitoa onyo hili: “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.” Vipi hapo? Umeona kwamba kila kitu kinachotajwa na Paulo ni mwenendo? Mpinga Sheria anawezaje kudai kwamba mwenendo hauna maana? Paulo anasema tena na tena kwamba mwenendo mwovu utamzuia mtu kuwa na urithi katika ufalme wa Mungu. Ona pia Wakolosai 3:5-8 na 1Wathes. 4:3-8.

 

Katika Ufunuo 21:8, Yohana anatumia maneno ya Yesu, hivi: “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.” Yesu aliwahukumu wote wenye mwenendo mwovu, ambao ni pamoja na kutokuamini. Maandiko yanasema mwenendo ni muhimu, na kwamba mwenendo mwovu utawafanya watu kuhukumiwa.

 

Siku zote dhambi huongezeka na kuwa kubwa zaidi. Fundisho hili la Kupinga Sheria limeongezeka na kuwa theolojia ya uongo katika Nchi za Magharibi. Hebu sasa tutazame mpango huo mwovu.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sura Ya Sita

(Chapter 6)

 

Mtoto Wa Kupinga Sheria: Usalama Milele Usio Na Masharti

(A Child Of Antinomianism: Unconditional Eternal Security)

 

Paulo alipewa kuona siku za baadaye alipoandika hivi: “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo” (ktk 2Timotheo 4:3-4).

 

Ni kitu gani kinachoweza kuvutia zaidi kuliko kufundishwa kwamba unaweza kupata uzima wa milele mbinguni kwa kuamini tu kwamba kitu fulani ni kweli, bila hicho kuathiri mwenendo wako binafsi? Unaweza kuishi unavyotaka, lakini uamini tu kwamba kitu fulani ni kweli, nawe utakuwa njiani kuelekea mbinguni. Ndivyo ilivyo katika fundisho hili la kupinga sheria.

 

Bila shaka Shetani ndiye mwanzilishi wa tafsiri “iliyoboreshwa” ya fundisho hili la kupinga Sheria, ijulikanayo kama Usalama wa Milele Usio Na Masharti, au kwa jina lake maarufu, Ukisha Okoka, Umeokoka Milele. Hii nakala mpya ya Kupinga Sheria inaondoa wasiwasi wowote wa kutokuwa na uhakika wa wokovu unaoweza kuwepo kwa wale ambao wanaonekana hawaamini tena. Unawahakikishia wafuasi wake kwamba kama waliwahi kuamini, wokovu wao ni hakika, milele.

 

Kwa mara nyingine tena, wafuasi wa hili fundisho la uongo kwa kawaida wanajiita wafuasi wa Paulo. Tena, wanasisitiza kwamba wokovu wao ni kwa neema tu, na aina yyote ya matendo ni juhudi za kufanya kazi ili kupata wokovu. Mara nyingi wanahesabu kwamba utii ni aina fulani ya kufanya kazi ili kupata wokovu.

 

Ili kufafanua imani yao kwa usahihi, nitatumia sana maneno ya Dkt. Charles Stanley, mwalimu maarufu wa Usalama wa Milele wa Wokovu bila Masharti, ambaye ameandika kitabu kinachoitwa Eternal Security: Can You Be Sure?[1] – yaani, Usalama wa Milele: Je, Unaweza Kuwa Na Uhakika? Dkt Stanley anafafanua usalama wa milele bila masharti hivi:  “usalama wa milele ni kazi ya Mungu ambayo kwa hiyo anahakikisha kwamba zawadi ya wokovu ikishapokelewa ni kitu cha milele, wala haiwezi kupotezwa au kupotea.”[2]

 

Katika sehemu iliyopita kuhusu Kupinga Sheria, tulisoma kwamba Paulo na Yesu waliorodhesha dhambi mbalimbali na kusema kwamba hao wafanyao hizo dhambi hawataurithi ufalme wa Mungu, na watatupwa katika ziwa liwakalo moto na kiberiti. Dkt. Stanley anasema hivi, kinyume kabisa:

“Uongo, udanganyifu, kuiba, kubaka, kuua, au kutokuwa mwaminifu si vitu vinavyopeleka watu Jehanamu.”[3]

 

Ni ajabu kwamba Maandiko tuliyotazama yanasema kinyume kabisa, sivyo? Mwandishi wa Waebrania alisema, Mungu atamhukumu mwasherati. Hakuna andiko hata moja katika yale tuliyosoma, lililoonyesha kwamba kwa wale wanaodai kwamba waliwahi kupokea zawadi ya wokovu, mambo yatakuwa tofauti. Hata onyo la Paulo kwa Waefeso halisemi hivyo kabisa.

 

“Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wowote wala kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi. Hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru. Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati, wala mchafu, wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu. Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi” (ktk Waefeso 5:3-6).

 

Ona onyo la Paulo mwishoni kabisa. Mtu yeyote asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana. Paulo anasema, kwa sababu ya dhambi hizo – uchafu, uasherati, au tamaa – hasira ya Mungu huwajia wale wasiotii. Dkt. Stanley pamoja na itikadi ya uongo ya usalama wa wokovu bila masharti, wanawadanganya watu kwa maneno matupu, kama Paulo alivyowaonya wasomaji wake. Uhakikisho anaotoa Dkt. Stanley ni kinyume kabisa na maonyo yanayorudiwa tena na tena katika Maandiko.

 

Kama wanaosema juu ya usalama wa milele wako sahihi, kwa nini Yesu alitoa onyo hili?

 

“Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe. Kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika Jehanamu. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe. Kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee, wala mwili wako mzima usitupwe katika Jehanamu” (Mathayo 5:29-30).

 

Yesu anasema, mwenendo mbaya – dhambi – utokanao na jicho lako au mkono wako hakika utasababisha mwili wako wote utupe Jehanamu. Yesu alisema ni afadhali kukata au kung’oa kiungo kinachokwaza katika mwili kuliko kutupwa mzima katika Jehanamu.

 

Lakini, Dkt. Stanley anaandika hivi:

 

“Ila, kama mwanamume au mwanamke aliyekwisha okolewa mara moja kutoka hali ya kutokusamehe, asiwe na wasiwasi. Kwa sababu, baada ya asilimia 100 ya dhambi za mwanamume au mwanamke kusamehewa, uwezo wa kutokusamehewa umeondolewa. Hakuna tishio tena. Hakuna mioto mingine ya zaidi ambayo mwamini anahitaji kuokolewa nayo.”[4]

 

Kama unavyoona kutokana na maneno yaliyopita, wale wenye kukubaliana na itikadi ya usalama wa milele wa wokovu watakuhakikishia kwamba hakuna kitu chochote utakachofanya baada ya kupata imani hapo kwanza kitakachoathiri wokovu wako, kama una hakika kwamba uliwahi kuokolewa kutoka hali ya kutokusamehewa. Kulingana na Dkt. Stanley, hakuna dhambi zinazoweza kuathiri wokovu wako, pamoja na yote ambayo Maandiko yamesema, na bila kujali maonyo ya Paulo kwa Wakorintho na Wagalatia kuhusu dhambi ambazo zingewazuia wanaozifanya kurithi ufalme wa Mungu, na bila kujali yale ambayo Yesu alimwambia Mtume Yohana kuhusu dhambi ambazo zingefanya watu kuhukumiwa kuingia Jehanamu. Kulingana na Dkt. Stanley, hakuna hata moja katika Maandiko hayo linalowahusu wale wenye kukubali itikadi ya usalama wa wokovu wa milele kama waliwahi kumwamini Yesu ili awasamehe dhambi na wakapokea zawadi ya wokovu.

 

Labda kosa la msingi la Dkt. Stanley ni kwamba, yeye anadai kwamba kama mtu ametubu dhambi zake na kusamehewa, msamaha huo ni pamoja na dhambi zote zitakazotendwa siku za baadaye. Petro anasema kinyume cha hayo: “ … kutakaswa dhambi zake za zamani” (ktk 2Petro 1:9).

 

Dkt. Stanley anaendelea zaidi. Aliandika hivi:

 

“Biblia inafundisha dhahiri kabisa kwamba upendo wa Mungu kwa watu Wake ni mkubwa sana kiasi kwamba hata wale wanao-ondoka kwenye imani hawana nafasi hata kidogo ya kutoka katika mkono Wake.”[5]  Akafundisha wakati mwingine hivi, “Hata kama mwamini atafanyika asiyeamini kwa namna yoyote ile, wokovu wake hauko hatarini”[6]  na tena “… waaminio wenye kupoteza au kuacha imani yao, wokovu wao unabaki …”[7]

 

Uliona jinsi fungu hilo la maneno linavyoanza? Dkt. Stanley anasema, “Biblia inafundisha dhahiri kabisa …” Maneno kama hayo yanaweza kukubaliwa tu na wale wasioijua Biblia yao, au wasiojifunza. Maneno hayo ni kwa ajili ya wale wasiojua Maandiko, wenye kutumainia waalimu kama Dkt. Stanley kupata lishe yao ya kiroho. Inasikitisha sana kwamba wanasalitiwa na watu kama Dkt. Stanley, ambao ni waasi dhidi ya Mungu na Bwana Yesu na mafundisho na maagizo Yake.

 

Sasa, watu wenye kukubaliana na fundisho la usalama wa wokovu bila masharti, wafanye uamuzi gani? Je, uasherati ni tatizo? Hapana. Na dhambi nyingine yoyote ile? Haiwezekani. Kulingana na Dkt. Stanley, kama mtu aliwahi kupokea zawadi ya wokovu na akasamehewa asilimia 100 ya dhambi zake, basi dhambi zake zote za wakati ujao zimesamehewa pia, na hawezi kupoteza wokovu wake.

 

Ndiyo maana kuachana na talaka vimeshika kasi sana katika makanisa yenye kufundisha hii itikadi ya usalama wa wokovu wa milele bila masharti! Hakuna sababu iwayo yote ya kukubali mafundisho ya Yesu kuhusu swala la talaka kwa sababu, wenye kufundisha juu ya usalama wa wokovu wa milele wanawahakikishia wahusika kwamba hakuna dhambi zitakazopeleka watu Jehanamu kama waliwahi kumwamini Yesu ili wasamehewe dhambi zao. Si kitu kama wataishi katika uzinzi endelevu. Kulingana na wanaofundisha usalama wa milele wa wokovu, maonyo kuhusu kutourithi ufalme wa Mungu na kuhukumiwa kutupwa Jehanamu hayahusiani na dhambi wanazotenda.[8]

 

Dkt. Stanley pia anadai kwamba:

           

“… Mungu hahitaji mtu awe na hali ya kudumu ya imani ili aokolewe – anachohitaji ni tendo la imani tu.”[9]  Anaendelea, “Hiyo [yaani, imani yenye kuokoa] ni tukio moja tu katika wakati ambapo tunachukua kile kilichotolewa na Mungu.”[10]  Akaandika tena hivi: “Awe mwaminifu au asiwe, kila mtu ambaye amewahi kuwa na imani yenye kuokoa wakati wowote ni sehemu ya kudumu ya mwili wa Kristo.”[11]

 

Lakini, Maandiko yana ujumbe tofauti kabisa, wenye kusisitiza kwamba ni imani inayoendelea na uaminifu unaoendelea vinavyoleta tofauti. Wazo kwamba kujitoa kwa mara moja tu kunaokoa milele ni la uongo. Fikiri kuhusu onyo analotoa Paulo kwa Wakorintho.

 

“Basi ndugu zangu, nataka kuwakumbusha ile Injili niliyowahubiri, mliyopokea na kusimama katika hiyo. Kwa Injili hii mnaokolewa, ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri. La sivyo, mliamini bure” (1Wakor. 15, 1-2, TLR).

 

Huu mstari ni muhimu sana. Paulo anakiri kwamba Wakorintho walipokea Injili, wakasimama katika hiyo, na wanaokolewa ikiwa wanaishika sana. Vipi kama hawaishiki sana? Paulo anawaonya kwamba, watakuwa waliamini bure.

 

Vivyo hivyo, onyo la Paulo kwa Wakolosai ni muhimu, na lina mantiki.

 

“Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarakishwa, tena adui katika nia zenu kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa katika mwili wa nyama yake kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama; mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake” (Wakolosai 1:21-23. Ona pia Yakobo 1:12).

 

Huo hapo ni muhtasari anaotoa Paulo wa Injili, ambayo yeye alikuwa mhudumu wake. Habari njema yote ya Injili inapatikana, mradi tu – kama – utaendelea katika imani yako, ukiwa thabiti na imara, bila kuyumbishwa utoke kwenye tumaini linalotajwa katika Injili. Mungu anataka mengi sana kutoka kwa wale anaowakomboa kutoka ufalme wa giza kuingia katika nuru Yake ya ajabu, yenye utukufu. Thawabu yao ni urithi katika ufalme wa Mungu badala ya kutupwa katika ziwa liwakalo moto na kiberiti.

 

Yesu alisisitiza kuhusu hitaji la kuvumilia,  hivi: “Watu wote watawachukia kwa sababu Yangu, lakini yeye atakayesimama imara hadi mwisho ataokoka” (ktk Mathayo 10:22, TLR). Pia alisema hivi, “Kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka” (Mathayo 24:12-13).

 

Dkt. Stanley pia anadai kwamba, “… tunaonyeshwa Mkristo ambaye hakuna wakati wowote katika maisha yake alipozaa matunda ya milele. Lakini, wokovu wake hauko hatarini kamwe”.[12] Halafu anasema, “… kuna Wakristo wasio-onyesha aina yoyote ya ushahidi wa Ukristo wao pia.”[13]

 

Yesu alikanusha madai kama hayo katika Yohana 15:1-6, kama ifuatavyo:

 

“Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa …

 

“Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote. Mtu asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi na kunyakuka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakatekea” (ktk Yohana 15:1-2; 5-6. Ona pia Luka 13:6-7).

 

Hilo tawi lililokatwa lilikuwa wapi? Lilikuwa katika mzabibu – ndani ya Yesu! Hii inasema juu ya watu walioanza ndani ya Kristo lakini hawakuzaa matunda. Matawi yasiyozaa matunda hukatwa na Mungu Baba na kuondolewa kwa Kristo. Nini hufanywa kwa matawi yale yasiyozaa matunda? Hutupwa na kunyauka, kisha yanaokotwa na kutupwa motoni ili yachomwe.

 

Hayo si mafundisho pekee ya Yesu kuhusu mada ya umuhimu wa kuzaa matunda mema. Katika Mathayo 7:17-19, Yesu alisema hivi: “Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri, na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.” Hapo tena sharti ni kuzaa matunda mazuri au kukatwa na kutupwa motoni.

 

Yesu alisimulia mfano mwingine tena wenye kufafanua hoja hiyo hiyo. “Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate. Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, ‘Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu. Uukate, mbona unaiharibu hata nchi?’ [Yule mtunzaji shamba] Akajibu akamwambia, ‘Bwana! Uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; nao ukizaa matunda baadaye, vema! La usipozaa, ndipo uukate’.” (Luka 13:6-9, Nyongeza kwa ajili ya kuweka wazi zaidi)

 

Hapa tena, swala ni kuzaa matunda. Katika kisa hiki, hayakuwepo matunda hata kidogo, basi Mungu akamwambia Yesu aukate mti huo. Yesu akasihi na kuomba muda zaidi, lakini akakubali kwamba kama mti usingezaa matunda mwaka uliofuata, basi ungefaa kukatwa.

 

Bwana Yesu alitoa fundisho linalofanana na hilo katika mfano wa talanta (ktk Mathayo 25:14-30). Kila mtumishi aliachiwa kiasi tofauti cha talanta ili afanyie biashara kabla ya bwana kuondoka kwenda safarini. Wengi walifanya vizuri, wakiongeza mara mbili kiasi walichokuwa wamekabidhiwa.

 

Mtumishi mmoja hakufanya hivyo. Yeye alipewa talanta moja, akaizika udongoni, kisha akamrudishia bwana wake hiyo hiyo moja wakati aliporudi. Katika mfano kuhusu mzabibu na matawi yake, tawi (yaani, mwamini) lilipewa yale maji yenye kuleta uhai kutoka kwa mzabibu shina, lakini halikuyatumia kuzaa matunda. Katika mifano yote miwili, mtumishi husika hakufanya chochote na kile alichokuwa amepewa.

 

Mwisho unafanana katika kila mfano. Yesu alisema hivi kuhusu mtumishi aliyechezea talanta yake: “Mtupeni huyo mtumishi asiyefaa huko nje katika giza, mahali ambapo kutakuwa na kilio na kusaga meno” (Mathayo 25:30, TLR).

 

Hii mifano inaonyesha adhabu na laana kwa kutokuzaa matunda, kwa kutokutumia tulichopewa na Mungu ili kuleta faida kwa ajili ya Ufalme. Je, pengine hiyo ndiyo maana ya Paulo anaposema, “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu tutende mambo  mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo”? (Waefeso 2:10) Kama ndivyo, itakuwa ni kutokutii kama tutakataa (au tutashindwa) kufanya hayo matendo mema ambayo Mungu alikwisha yaandaa kabla ili sisi tuyafanye.

 

Ushahidi zaidi unapatikana katika mfano wa mwenye kupanda mbegu (ktk Mathayo 13:3-8; Marko 4:3-8; na Luka 8:5-8). Mbegu zilipandwa katika udongo wa namna nne. Ni mmoja tu ndiyo ulitoa mavuno. Kuhusu huo udongo, Yesu alifafanua hivi: “Naye aliyepokea mbegu iliyoangukia penye udongo mzuri, ndiye alisikiaye lile neno na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini” (Mathayo 13:23). Mwamini wa kweli huvumilia na kuzaa matunda, au mazao, kulingana na kile ambacho Mungu amempa atende.

 

Vipi kuhusu zile aina tatu nyingine za udongo? Mbili kati yake ndizo zinazotufaa katika somo hili. Ule wa kwanza hautufai. Yesu alisema juu yake, kwamba, mbegu inayopandwa njiani ni kama mtu mwenye kusikia ujumbe lakini hauelewi. Yule mwovu huja na kunyakua kilichopandwa moyoni mwake (Mathayo 13:19). Aina ya pili – mbegu iliyopandwa kwenye udongo wenye miamba – ni mfano wa mtu mwenye kulisikia Neno na kulipokea kwa furaha. Anakuwa mwamini. Lakini kwa kuwa hana mizizi, anadumu kwa muda mfupi tu. Dhiki au mateso vinapomjia kwa sababu ya Neno, anaanguka upesi (Mathayo 13:20-21). Hakuweza kuvumilia. Aina ya tatu ni mbegu kupandwa katikati ya miiba. Huyo naye husikia Neno, lakini masumbufu ya maisha haya na udanganyifu wa mali huzibana kiasi cha kuzifanya zisizae (Mathayo 13:22).

 

Katika zile aina nne za udongo zilizopokea mbegu, ni moja tu ilivumilia na kuzaa matunda. Aina ya pili na ya tatu japo zilipokea mbegu – kusikia na kulikubali Neno – zilishindwa kuvumilia.

 

Kutokana na Maandiko hayo yaliyotangulia, tunaona kwamba kuzaa matunda kwa ajili ya ufalme ni kitu muhimu sana. Tunaweza kupoteza wokovu wetu kama tutakataa au kushindwa kufanya yale matendo mema ambayo Mungu aliyaandaa tangu mwanzo ili sisi tuyafanye. Hiyo ni aina ya uasi dhidi ya Mungu.

 

Dkt. Stanley anasema, “Tunaonyeshwa Mkristo ambaye hakuna wakati wowote katika maisha yake alipozaa matunda ya milele. Lakini, wokovu wake hauko hatarini kamwe”. Je, hivyo ndivyo wewe ulivyoelewa Maandiko yaliyopita? Katika Maandiko hayo YOTE yaliyotajwa hapo nyuma, kwa sababu hakukuwa na matunda (au, matunda yalikuwa mabaya, au talanta ilifukiwa chini), kukosekana kwa matunda kulisababisha kukatiliwa mbali, au mti kukatwa, au tawi kukatwa kwenye mzabibu na kutupwa motoni ili kuchomwa, au mtumishi mzembe alihukumiwa. Hii mifano yote inaonyesha hukumu kwa wale ambao hawazai matunda.

 

Wanaotetea hoja ya usalama wa wokovu milele wanasema hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kama dhambi zako ziliwahi kusamehe kwa sababu ya kumwamini Kristo. Lakini, Maandiko nayo yanasema hivi:

 

“Naye [Yesu] … akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii” (Waebrania 5:9).

 

Je, Yesu pia ndiye sababu ya wokovu kwa wale wasiomtii? Hilo ni kinyume cha mstari huu, sivyo? Ni muhimu kuona kwamba neno “kutii” katika Waebrania 5:9 liko katika hali ya kuendelea – hivyo basi, kwa wote wanaoendelea kumtii.

 

Je, mtu anaye-endelea kutotii anao wokovu? Hebu fikiri juu ya mafundisho ya Mtume Yohana:

 

“Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye ‘Nimemjua’ wala hazishiki amri zake ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake” (1Yohana 2:3-4).

 

Hapo tena, neno “kutii” liko katika hali endelevu, yaani, “ikiwa [tutaendelea] kutii amri zake.”

 

Hebu tuwe na marudio kidogo. Yesu ndiye aliyesema, “Si kila mtu aniitaye ‘Bwana, Bwana’ atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye tu afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (ktk Mathayo 7:21, TLR). Yesu alisema kwamba kila alichofanya na kila alichosema ni vile Baba Yake alivyomwambia kusema na kufanya (ktk Yohana 8:28; 12:49-50; 14:10; 14:24; 14:31). Basi, kila kitu ambacho Yesu alisema na kufanya kilikuwa mapenzi ya Mungu. Je, ni ajabu kwamba Yeye ndiye asili ya wokovu kwa wote wanaomtii? (Waebrania 5:9). Au kwamba alimalizia agizo Lake kuu kwa amri kwamba wanafunzi wapya wafundishwe kuyatii yote ambayo Yeye amewaagiza? (ktk Mathayo 28:20).

 

Maandiko yanaonyesha kwamba watu wanaofikiri kwamba wanaweza kuishi dhambini na bado wawe na wokovu wamedanganyika. Mtume Yohana alisema kuhusu jambo hilo pia, hivi:

 

“Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi. Kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. … Atendaye dhambi ni wa Ibilisi … Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi …” (1Yohana 3:6, 8, 9).

 

Kama tuonavyo kutoka Maandiko mengi sana, kuna hitaji kubwa kabisa la kutii mafundisho na amri za Yesu unaoambatana na imani ya KiBiblia na wokovu. Nini kinatokea kwa wale wanaoendelea katika dhambi kwa makusudi, wakiwa na uhakika kwamba matendo yao hayataathiri wokovu wao? Tunasomaje katika Waebrania 10:26-27?

 

“Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao”.

 

Watetezi wa usalama wa wokovu milele wanaohubiri kwamba dhambi zote zikishasamehewa mara moja basi ni kwamba dhambi zote za baadaye zimesamehewa pia na kwamba zawadi ya wokovu ikishapokelewa haiwezi kupotea au kupotezwa kamwe wanafundisha injili ya uongo ambayo iko kinyume na Maandiko.

 

Petro aliwaambia waamini kuhusu sifa fulani ambazo wanapaswa kufanya kila juhudi kuziongezea kwenye imani yao. Halafu akaonya hivi:

 

“Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani” (2Petro 1:9).

 

Dhambi za zamani? Ndiyo. Tunapofikia kwenye imani yenye kuokoa na kutubu dhambi zetu, zinazosamehewa asilimia 100 ni zile dhambi zetu za zamani. Katika barua Yake kwa yale makanisa saba katika Ufunuo sura ya 2 na ya 3, Yesu aliyaagiza makanisa matano katika saba yatubu. Kwa nini yawe na haja ya kutubu kama dhambi zote za baadaye zilikwisha samehewa? Wasingehitaji kufanya hivyo. Injili ya uongo ndiyo yenye kufundisha kwamba dhambi za baadaye zimesahemewa, wakati ukweli ni kwamba dhambi za mtu za zamani ndiyo zimesamehewa.

 

Ndiiyo maana Maandiko yanafundisha kwamba, “utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka” (ktk Wafilipi 2:12). Pia yanasema, “Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa” (ktk 2Wakor. 13:5). Wakristo wanapaswa kuwa na nia ya Kristo (1Wakor. 2:16).

 

Mungu ni mwenye upendo, neema na ni mwema. Lakini pia ni mtakatifu na mwenye haki. Tunapaswa kumhofu Yeye kwa habari ya ghadhabu Yake na hukumu Yake ya haki juu ya wale wanaokataa kumtii – wale wanaoendelea katika kumwasi Yeye.

 

Katika sura ya kwanza tuliona kwamba uasi wa kwanza ni kinyume cha Yesu kama Bwana. Katika maandishi ya Dkt. Stanley, jina “Bwana” halionekani kabisa. Anazungumza juu ya Yesu kama Mwokozi, lakini si Bwana. Huyu mtetezi wa usalama wa wokovu milele bila masharti anaonekana kupata matatizo sana kumkiri Yesu kama Bwana, kwa sababu kufanya hivyo kunaambatana na wajibu wa kumtii. Kumpokea Yesu kama Bwana na kukataa mafundisho na amri Zake, kunaangamiza hilo fundisho la uongo la usalama wa wokovu milele bila masharti, pamoja na fundisho la Kupinga Sheria.

 

Kumtii Yesu kama Bwana hakuendani kabisa, tena ni kinyume na itikadi hizo za uongo.

 

Petro vile vile alipiga vibaya sana itikadi ya usalama wa wokovu milele bila masharti. Katika 2Petro 2:20-22 aliandika kama ifuatavyo:

 

“Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa,  hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa. Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli: ‘Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaagaa matopeni’.”

 

Petro alikuwa anasema juu ya watu waliokuwa wamemjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Lakini hao wakanaswa tena katika uharibifu wa dunia na kushindwa. Petro anasema watu hao wako katika hali mbaya zaidi mwishoni kuliko mwanzoni. Kwani mwanzoni ingekuwaje? Wangehukumiwa kuingia Jehanamu kwa kutokuwa na imani yenye kuokoa. Na mwishoni ingekuwaje? Yesu alituambia. “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana. Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo” (Luka 12:47-48). Tukisha jua ukweli na kurudi tena duniani, adhabu yetu itakuwa kali zaidi.

 

Hapa tena tunaonywa na Petro kwamba hakuna kitu kinachoitwa usalama wa wokovu milele bila masharti.

 

Katika 2Petro 3:17, anamalizia barua yake kwa kutoa onyo lingine moja, hivi:

 

“Basi wapenzi, mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu, mkaanguka na kuuacha uthibitisho wenu.”[14]

 

Petro anatambua kwamba nafasi yetu ndani ya Kristo ni salama. Lakini anasema, tunaweza kuanguka kutoka kwenye hiyo nafasi yetu salama, kitu ambacho kinakubaliana kabisa na Maandiko yaliyotangulia. Anatuonya kwamba, tuwe macho. Anajua kwamba tunaweza kuchukuliwa na makosa ya watu wasiofuata sheria – wahalifu. Inavutia kuona kwamba Petro alitumia neno “wahalifu” ambalo maana yake nyingine ni wasioshika sheria. Kama unavyojua, wale wanaoeneza itikadi ya usalama wa wokovu milele bila masharti ni watu wasioshika sheria.

 

Mwandishi wa Waebrania naye aliandika mistari mingi sana kuhusu kudumu katika imani. Katika Waebrania 6:4-6 anaeleza kuhusu mwamini ambaye alipokea na kupata kila kitu ambacho Mungu anampa aaminiye.

 

“Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafasi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.

 

Kiini cha usalama wa wokovu milele bila masharti ni kwamba, hakuna yeyote aliyewahi kusamehewa anayeweza kupotea kamwe. Maandiko hayo hapo juu yanapinga kabisa fundisho hili la uongo. Watu waliotajwa hapa walikuwa na kila kitu ambacho Mungu anatoa. Mwandishi anaeleza kinachotokea na kisichoweza kutokea, kama mtu wa aina hiyo ataanguka. Andiko hili linasema kwamba mtu anayeanguka hawezi tena kuirudia imani. Wakati mwingine pekee ni pale Yesu alipofundisha kwamba kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu haitasamehewa (ktk Mathayo 12:31). Mtu kama huyo hawezi kuokoka.

 

Mwandishi anaonya tena katika Waebrania 10:26-27, kama ifuatavyo:

 

“Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu kwenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.”

Katika Waebrania 6:4-6 mwandishi alizungumza juu ya wengine. Sasa hapa anajiweka na yeye pia. Anasema, “kama tuki …” Hakuna shaka kwamba anazungumza na waaminio. Tunaweza pia kudhani kwamba yeye ni mwamini. Anazungumza juu ya mtu aliyepokea maarifa ya ukweli – si kusikia tu au kupata habari zake. Hapana – anasema kuhusu mtu ambaye ameipokea – yaani, aaminiye.

 

Hapa, mwandishi anachofanya ni kutilia mkazo hitaji la maisha yaliyobadilika kwa wale ambao ni waamini – ni lazima waachane na maisha ya dhambi na kuwa watakatifu. Kama wakikataa makusudi na waendelee kufanya dhambi, basi wanakabiliwa na hukumu tu na moto mkali sana.

 

Mwandishi anaweka wazi pia kwamba hii si ile nidhamu itolewayo kwa “wana” ambayo anaifafanua baadaye katika Waebrania 12. Hapana – hii ni adhabu – hukumu na moto mkali uwakao – utakaowateketeza maadui wa Mungu. Hakuna mwamini anayeweza kupitia hapo, na hakuna mwamini ambaye ni adui wa Mungu.

 

Je, hayo si kinyume kabisa na mambo ambayo Dkt. Stanley amedai tena na tena? Yeye alidai kwamba, “Ila, kama mwanamume au mwanamke aliyekwisha okolewa mara moja kutoka hali ya kutokusamehe, asiwe na wasiwasi. Kwa sababu, baada ya asilimia 100 ya dhambi za mwanamume au mwanamke kusamehewa, uwezo wa kutokusamehewa umeondolewa. Hakuna tishio tena. Hakuna mioto mingine ya zaidi ambayo mwamini anahitaji kuokolewa nayo.”[15]

 

Kweli? Huyo mtu wa Dkt. Stanley hajizuii katika mwenendo wake. Yeye anaamini anaweza kufanya chochote (pamoja na dhambi) na kusiwe na athari yoyote kwa wokovu wake. Mwandishi wa Waebrania anasema yeyote – hata yeye mwandishi – atakaye-endelea katika dhambi kwa makusudi atarajie tu hukumu ya kutisha na moto mkali, utakaowateketeza adui wa Mungu.

 

Mwandishi anaendelea kusisitiza fundisho hilo mwishoni mwa sura, anaposema juu ya wenye haki kama ifuatavyo:

 

“ ‘Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; naye akisitasita, roho yangu haina furaha naye.’

Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.”

 

Hapa anataja kanuni tunayojua kuwa ya kweli. Wenye haki wataishi kwa imani. Lakini itakuwaje kama wenye haki hawaishi tena kwa imani? Mwandishi anaendelea kwa kutoa itikio au jibu la Mungu kwa hali hiyo: “Naye akisitasita, roho yangu haina furaha naye.”

 

Ndipo mwandishi anapowalinganisha wale wanaositasita na wale wenye kuamini. Wanaositasita na kurudi nyuma wanaangamizwa; wale wanaoamini wanaokolewa.

 

Yule aliyerudi nyuma hakuwa asiyeamini siku zote, bali alikuwa mmoja ambaye Mungu alimwita “mwenye haki wangu”. Cha kusikitisha ni kwamba, hata mwenye haki anayerudi nyuma ataangamizwa. Hapa tena, hii ni kinyume kabisa na madai ya fundisho la usalama wa wokovu milele bila masharti, kithibitisho kwa mara  nyingine tena kwamba ni ya uongo!

 

Hapa tena, ona kufanana kwake na mafundisho ya Yesu katika Mathayo 24:45-51, mahali ambapo Yesu anawalinganisha watumishi wawili – mmoja aliye mwaminifu na mwenye kuvumilia, na mwingine anayechoka na kuanguka.

 

“Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?  Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. Amin nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote.

 

“Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, ‘Bwana wangu anakawia;’ akaanza kuwapiga wajoli wake na kula na kunywa pamoja na walevi; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua. Atamkata vipande viwili na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki. Ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.”

 

Ni kwamba wote walianza kumtumikia Bwana. Wote ni watumishi wenye nafasi zenye majukumu – kuwasimamia wenzao.

 

Yesu anamsifu yule wa kwanza na kumhakikishia kwamba atapewa thawabu kwa ajili ya uaminifu wake. Sivyo kwa yule wa pili. Haikuwa kitu kwamba aliwahi kuwa mtumishi mwaminifu mpaka akapandishwa cheo na kupewa nafasi yenye majukumu. Kilichokuwa muhimu ni kwamba wakati bwana wake aliporudi, tumishi huyo hakuwa anatekeleza kazi alizopangiwa. Badala yake, alikuwa anawanyanyasa wale waliokuwa chini ya mamlaka yake na kuishi maisha ya anasa.

 

Ona ukali wa adhabu. Ni kali kuliko adhabu nyingine yoyote inayotajwa katika mifano iliyosimuliwa na Yesu. Je, ni kwa sababu alikuwa mwangalizi wa wengine? “Alikatwa vipande” na kupelekwa Jehanamu pamoja na wanafiki.

 

Hapa tena tunaona mfano wa mtu ambaye alianza vizuri, lakini akamaliza vibaya. Alihukumiwa kwenda Jehanamu pamoja na adhabu kali kuliko zinazoelezwa katika mifano ile mingine.

 

Hebu tudhani tu kwamba “chakula” alichopaswa kuwapa watumishi wale wengine ni mafundisho na amri za Yesu, kama ambavyo Yesu aliagiza katika Mathayo 28:20. Hebu fikiri viongozi wote wa kanisa siku hizi wanaokataa kuwapa watu walio chini ya uangalizi wao chakula chao – mafundisho na amri za Yesu, vinavyotoa uzima wa milele. Je, hao viongozi wa kanisa siyo watumishi wasiokuwa waaminifu, ambao wanamwasi mkuu wa kanisa, Bwana Yesu?

 

Wokovu una masharti! Mtu asipokuwa na imani yenye kuokoa, hawezi kuokoka. Sharti moja la wokovu (ambalo lina mengine mengi ndani yake) ni kwamba mtu lazima awe na imani yenye kuokoa. Ukitaka maelezo kamilifu kuhusu imani yenye kuokoa, unaweza kusoma kitabu changu kiitwacho Imani Yenye Kuokoa [katika Kiswahili] kwenye tovuti hii: www.bereanpublishers.com |tafuta Book: Saving Faith.

 

Tazama maneno mengine yenye kutoa masharti. Yohana 15:10 – Kama mtatii amri zangu, mtadumu katika pendo langu, kama na mimi nilivyotii amri za Baba Yangu na kukaa katika pendo lake. Yohana 15:14 – Ninyi ni rafiki zangu kama mtafanya ninayoamuru. Waebrania 3:14 – Tumefika mahali pa kumshiriki Kristo ikiwa tutashika kwa uthabiti ujasiri wetu tuliokuwa nao tangu mwanzo. (TLR)

 

Katika Maandiko yaliyotazamwa hapo nyuma, Paulo pia aliweka sharti la wokovu kwamba ni uvumilivu. “Mmeokolewa kwa injili hii kama mkishika sana neno nililowahubiri. Vinginevyo, mmeamini bure tu” (1Wakor. 15:1-2, TLR). Pia, “Lakini sasa yeye amewapatanisha ninyi kwa mwili wa Kristo kwa njia ya kifo ili awafikishe mbele Yake mkiwa watakatifu, bila doa na bila mashtaka, kama mtaendelea katika imani yenu, mkithibitishwa na kuwa imara, bila ya kuyumbishwa kutoka kwenye tumaini lipatikanalo katika Injili” (Wakolosai 1:22-23, TLR).

 

Kuna mengi sana ya kusema kuhusu mada ya itikadi ya uongo ya usalama wa wokovu milele bila masharti kuliko tunavyoweza kusema katika nafasi hii. Ona maelezo kamili ya vithibitisho vingi sana kinyume cha fundisho hili la uongo kwenye tovuti hii: www.bereanpublishers.com | tafuta False Doctrines | halafu tafuta Is The Believer Eternally Secure?

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sura Ya Saba

(Chapter 7)

 

Mtoto Mwingine Wa Kupinga Sheria: Ulaghai Katika Kuhubiri Injili

(Another Child Of Antinomianism: Fraud In The Presentation Of The Gospel)

 

Wafuasi wa mafundisho ya uongo ya Kupinga Sheria na usalama wa wokovu milele bila masharti hubadilisha, kufasiri vibaya au kupuuza Maandiko mengi yenye kuthibitisha kwamba wao wanadanganya. Matokeo yake ni kwamba wanapohubiri “injili” yao ya uongo, inakuwa imechafuliwa na uongo na ulaghai.

 

Ulaghai maana yake kueleza kitu isivyo kwa makusudi kabisa (au, kutokujali ukweli kwa makusudi) ili kumfanya mtu atende kwa kutegemea maelezo hayo ya uongo, na kupelekea yeye kuumia. Ninajua tafsiri yake vizuri sana kutokana na mafunzo yangu kama mwanasheria.

 

Nina mashaka kwamba wachache sana katika wale wenye hatia ya ulaghai katika kuhubiri injili hupotosha ukweli kwa makusudi. Yawezekana karibu wote huhubiri uongo wao huo kwa makusudi, pasipo kujali ukweli

 

Katika Sura ya Kwanza, nilisema kwamba uasi wa kwanza – kule kukana kwamba Yesu lazima awe Bwana wa wote watakao-okolewa – unahusu Nafsi ya Yesu Kristo. Vivyo hivyo, ulaghai wa kwanza unaoendelezwa na viongozi wa kanisa unahusu jinsi wanavyompeleka Yesu kwa watu wao.

 

Mkazo wa siku hizi katika kanisa la Kikristo unaonekana kuwa Yesu Kristo ni Mwokozi. Miito itolewayo madhabahuni kwa kawaida inasema hivi: “Mkubali yesu kama Mwokozi wako, nawe utapata uzima wa milele!” Wakati mwingine kuna tofauti kidogo, inayosema hivi: “Kama unaamini kwamba Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zako, utapata uzima wa milele.” Je, maneno hayo yote ni sahihi KiBiblia?

 

Hakuna popote katika Maandiko penye kusema wala kupendekeza kwamba kumwamini, kumkubali au kumpokea Yesu kama Mwokozi kunaweza kutuokoa. Ni dhahiri kutokana na Maandiko kwamba Yesu lazima we Mwokozi wetu kama tunataka kuwa na uzima wa milele. Tangazo la kwanza kuhusu kuzaliwa Kwake lilisema, “Mwokozi amezaliwa kwa ajili yenu” (ktk Luka 2:11, TLR). Utamaduni wa Kikristo umedhani – bila ya kujali kabisa – kwamba, kwa kuwa Yesu lazima awe Mwokozi wetu, basi tunachohitaji kufanya ni kumkubali Yeye tu kama Mwokozi.

 

Vivyo hivyo, hakuna mahali popote katika Maandiko tunapoambiwa kwamba tunaweza kupata uzima wa milele kwa kuamini katika kitu ambacho Yesu alifanya. Maandiko yote yanayosema juu ya wokovu yanatushauri kumwamini Yeye – Yesu (ona ktk Yohana 2:11; 3:15, 16, 18; 6:40; 7:39; 8:30; pia Warumi 4:24; 1Petro 1:8).

 

Basi, kama hatutakiwi kuamini, kukubali au kumpokea Yesu kama Mwokozi (au kuamini katika kitu fulani alichofanya) ili Yeye aweze kuwa Mwokozi wetu na tupate uzima wa milele, nini basi tunachotakiwa kufanya? Hebu tufanye mapitio mafupi ya baadhi ya Maandiko tuliyotazama hapo nyuma kidogo yenye kujibu swali hilo.

 

Je, Yesu alisema nini? Yesu aliwaambia wanafunzi Wake hivi: “Ninyi mnaniita mimi ‘Mwalimu’ na ‘Bwana’. Sawa kabisa kwa sababu, ndivyo nilivyo” (Yohana 13:13, TLR). Yesu alisema tena, “Niliwaambia kwamba mtakufa katika dhambi zenu. Kama hamwamini kwamba Mimi ndiye, hakika mtakufa katika dhambi zenu” (Yohana 8:24, TLR). Akaeleza mamlaka Yake kuwa ni Bwana wakati aliposema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani” (Mathayo 28:18).

 

Maandiko yanatamka kwamba tunatakiwa kumwamini na kumpokea Yesu kama BWANA wetu! Andiko maarufu sana la wokovu ni Warumi 10:9. “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.” Vivyo hivyo, Paulo alimwambia yule askari magereza wa Filipi hivi: “Mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka, na watu wote wa nyumbani mwako” (Matendo 16:31, TLR). Huo ndiyo ulikuwa ujumbe wa kanisa la kwanza – kanisa lililovumilia mateso makali sana! Wao walimpokea Yesu kama Bwana (Wakolosai 2:6). Paulo akasema, kwa mshangao kabisa: “Sisi hatujihubiri wenyewe, bali tunamhubiri Yesu Kristo kama Bwana!” (2Wakor. 4:5, TLR). Andiko lenye kushawishi kabisa ni majumuisho anayofanya Paulo kuhusu huduma yake kwa Waefeso. “Nimewatangazia Wayahudi na Wayunani pia kwamba, lazima wamgeukie Mungu katika toba, na kuwa na imani katika Bwana wetu Yesu” (Matendo 20:21, TLR). Aliwafundisha Wathesalonike hayo hayo, kama ifuatavyo: “Mungu hakutuchagua sisi tupitie hasira, bali alituchagua tupokee wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo” (1Wathes. 5:9, TLR). Na kwa Warumi alisema hivi: “Malipo ya dhambi ni kifo, lakini zawadi ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23, TLR. Ona pia Warumi 5:21).

 

Petro alithibitisha mafundisho ya Paulo. Siku ya Pentekoste alihubiri hivi: “Kila atakayeliitia jina la Bwana ataokoka” (Matendo 2:21). Akamalizia mahubiri yake hivi: “Mungu amemfanya huyu Yesu, ambaye ninyi mlimsulubisha, kuwa Bwana na Kristo” (Matendo 2:36, TLR). Halafu baadaye akafundisha na kusema, “Katika mioyo yetu mtengeni Kristo kama Bwana” (1Petro 3:15, TLR).

 

Nini maana ya Yesu kuwa Bwana wetu? Ni lazima awe mkuu wetu, Mfalme wetu, mtawala wetu, mwenye mamlaka yote na ya mwisho juu ya maisha yetu. Kwa lugha niliyotumia kumwelewesha mjukuu wangu, “Lazima awe bosi wako”.

 

Tukisikiliza kinachohubiriwa katika makanisa yetu mengi, hakika tutatamka kwamba ujumbe mkuu wa Maandiko ni kwamba, Yesu ni Mwokozi wetu. Lakini je, huo ndiyo ujumbe wa msingi wa Maandiko? Hapana. Katika Agano Jipya, Yesu anaitwa Mwokozi mara kumi na tano tu. Mungu Baba anatajwa kuwa Mwokozi mara tisa tu. Yesu anaitwa Bwana mara mia sita kumi na nane (618), zaidi ya mara arobaini ya anavyoitwa Mwokozi. Kwangu mimi ni kitu cha kuzingatia sana kwamba kiasi cha mbili ya tatu ya vitabu vya Agano Jipya – kumi na nane – havitaji jina Mwokozi. Injili mbili kati ya zile nne hazitaji jina Mwokozi, wala Warumi, Wakolosai, Wakorintho wa Kwanza na wa Pili, Wathesalonike wa Kwanza na wa Pili, Timotheo wa Kwanza, Wagalatia, Filemoni, Waebrania, Yakobo, Petro wa Kwanza, Yohana wa Pili na wa Tatu, Yuda, na hata Ufunuo.

 

Je, tofauti kati ya Mwokozi na Bwana ni ya maana? Je, ni muhimu kwamba tumwamini Yesu kama Bwana wetu? Jibu letu huamua kama tuna uzima wa milele au hatuna. Ushahidi hupatikana katika andiko ambalo si la kawaida. Paulo alifundisha hivi:

 

“Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia” (Warumi 14:9).

 

Hayo yanawezekanaje? Kwani Maandiko hayafundishi kwamba Yesu alikufa na kufufuka ili kufanya malipizi kwa ajili ya dhambi zetu, kutukomboa, ili tuweze kuhesabiwa haki mbele za Mungu, ili tuweze kupatanishwa na Mungu na kufikishwa mbele Zake tukiwa watakatifu, bila mawaa na tukiwa huru pasipo mashtaka yoyote? Naam, inafundisha hivyo. Sasa, Warumi 14:9 inawezaje kuunganishwa na makusudi hayo ya ukombozi ambayo kwayo Yesu alikufa na kufufuka? Kwa kutambua kwamba hayo makusudi yote ya ukombozi ni halali tu kwa wale ambao Yesu ni Bwana kwao! Sababu ya Yesu kufa na kufufuka tena ilikuwa aweze kuwa Bwana wa wote, akijua kwamba anaweza kuwa Mwokozi kwa ajili ya wale tu ambao Yeye ni Bwana kwao.

 

Wakati mwingine Ukristo unasemekana kuwa ni mahusiano, si dini. Tofauti katika mahusiano ni muhimu tunapozitazama zile ambazo zingetokana na kumpokea Yesu kama Mwokozi, na kumpokea Yesu kama Bwana. Kama Yeye ni Mwokozi wetu tu, basi uhusiano ungekuwa ni kati ya Mwokozi na aliyeokolewa. Wakati Yesu anapokuwa Bwana wetu, uhusiano unakuwa kati ya Bwana na mtumishi.

 

Je, Agano Jipya linafundisha uhusiano gani? Tunafundishwa tena na tena kwamba mwamini ni mtumishi, au hata mtumwa, wa Bwana Yesu. Maandiko yanafundisha hivi: “Ninyi si mali yenu wenyewe. Mlinunuliwa kwa bei kubwa” (1Wakor. 6:19, TLR). Kwani, mtumwa si anaelezwa kwa lugha hiyo – kwamba ni mtu asiyekuwa huru, bali anamilikiwa na bwana?

 

Tafsiri ya Kiingereza ya New American Standard inafafanua vizuri mahusiano yetu na Bwana Yesu kwamba ni watumwa wa upendo. Mtumwa wa aina hii alikuwa mtumishi wa kipekee sana, ambaye baada ya miaka saba – wakati alipotakiwa kuwekwa huru – yeye alichagua mwenyewe kubaki na bwana wake. Utaratibu wa kufanyika mtumwa wa upendo (au wa hiari) unapatikana katika Kutoka 21:5-6. “Lakini huyo mtumwa akisema waziwazi, ‘Mimi nampenda bwana wangu, na mke wangu na watoto wangu; sitaki mimi kutoka niwe huru,’ ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango, na bwana wake atalitoboa sikio lake kwa uma; ndipo atamtumikia sikuzote.” Huyu anaweza kuwa mtu ambaye alijiuza kwa hiari yake mwenyewe kuwa mtumwa ili alipe deni fulani, lakini akakuta kwamba hali yake kama mtumwa ni bora zaidi kuliko ile aliyokuwa nayo kwanza. Basi, anaamua kukaa na bwana wake kama mtumwa wa upendo. Mara nyingi bwana alimtunukia herein ya dhahabu kama ishara ya nafasi yake maalum kama mtumwa wa upendo.

 

Kanuni za utumwa wa upendo ni hizi: (1) Ni kitu cha hiari, (2) hutamkwa hadharani, (3) kutokana na upendo kwa bwana wake, (4) ni utumwa – kuacha kila kitu, na (5) ni kwa maisha yote. Hayo ndiyo masharti pia kwa ajili ya watakaomfuata Yesu na kumpokea kama Bwana wao.

 

Waandishi wa Agano Jipya walijitangaza kuwa ni watumwa wa upendo. Paulo (Warumi 1:1); Yakobo (Yakobo 1:1); Petro (2Petro 1:1); Yuda (Yuda 1:1) na Yohana (Ufunuo 1:1). Tena, Maandiko yanawataja waamini wote wa kweli kuwa ni watumwa wa upendo, kama ifuatavyo: “Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa Wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana …” (Ufunuo 1:1).

 

Sawa na jinsi uhusiano wetu na Yesu ulivyo wa kitofauti sana anapokuwa Bwana wetu, ndivyo na itikio letu linavyotakiwa kuwa. Kama Yesu angekuwa Mwokozi wetu tu, basi itikio letu Kwake lingekuwa shukrani kwa ajili ya kutuokoa kutokana na hasira ya Mungu. Wakati Yesu anapokuwa Bwana wetu nasi ni watumwa wake, itikio letu la msingi sana Kwake ni kumtii kwa sababu ya upendo.

 

Hebu tutazame Maandiko yenye kuthibitisha kwamba utii ndiyo itikio sahihi kutoka kwetu kumwelekea Bwana wetu Yesu. Tunasoma katika 1Yohana 5:3 kwamba kumpenda Mungu ni kuzitii amri Zake. Yesu alisema, “Kama mnanipenda Mimi, mtatii ninayoamuru” (Yohana 14:15, TLR). Mwandishi wa Waebrania anaunganisha wokovu na utii, hivi: “Yeye (Yesu) alifanyika chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wale wanaomtii” (Waebrania 5:9, TLR). Yesu alitazamia utii kutoka kwa wafuasi Wake. Aliwauliza wale waliodai kumfuata kama Bwana bila kumtii swali hili: “Kwa nini mnaniita ‘Bwana, Bwana’ na hamfanyi ninayosema?” (Luka 6:46, TLR). Yesu alisema hakuna wokovu bila utii:”Si kila mtu aniambiaye ‘Bwana, Bwana’ atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali yeye tu afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 7:21, TLR).

 

Kama watumishi Wake, utii ndiyo itikio la kawaida, linalotazamiwa, kwa Bwana wetu Yesu. Pia, ni ushahidi kwamba Yesu kweli ni Bwana wetu. Isitushangaze kwamba Yesu aliweka utii kama sehemu ya maagizo Yake ya mwisho kwa kanisa Lake. Kwanza alitamka nafasi yake kama Bwana: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani” (Mathayo 28:18). Halafu akawaambia wafuasi Wake alichotazamia wao kufanya akiwa hayupo. “Nendeni duniani kote na kufanya watu kuwa wanafunzi katika mataifa yote” (Mathayo 28:19, TLR). Akawaambia mambo mawili ya kufanya katika utaratibu wa kufanya watu kuwa wanafunzi: “Wabatizeni katika jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kutii yote ambayo nimewaagiza” (Mathayo 28:19, 20, TLR).

 

Ningekuwa mahakamani nikilishtaki kanisa kwa ulaghai kwa jinsi linavyohubiri Injili, naamini viongozi wa makanisa mengi wangepatikana na hatia. Je, kanisa lako na wewe, mnamhubiri Yesu Kristo kama Bwana? Je, kanisa lako na wewe mnaweka wazi kabisa kwamba hakuna wokovu bila Yesu kuwa Bwana? Je, kanisa lako na wewe mwenyewe mnafundisha kwamba utii wa mtu kwa maagizo ya Yesu ni ushahidi kwa Mungu kwamba Yesu ni Bwana wa mtu? Mwisho – Je, wewe na kanisa lako mnatii agizo la mwisho la Yesu la kuwafundisha waongofu wapya kutii kila kitu ambacho Yesu aliamuru?

 

Wale wanaosema wokovu ni kumpokea Yesu tu kama Mwokozi, mara zote wanashindwa – au wanakataa – kufundisha kwamba kutii mafundisho na amri za Yesu ni lazima kwa wokovu. Kuna wanaoshika msimamo huu kwa sababu ndiyo maoni ya kawaida katika utamaduni huu wa Kikristo. Na, Wapinga Sheria na wale wenye kufuata itikadi ya usalama wa wokovu milele bila masharti hushindwa na kukataa kufundisha utii kwa Sheria ya Kristo kwa sababu wao wanaamini kwamba hawako chini ya sheria bali chini ya neema, na kwamba mwenendo si kitu muhimu kwa wokovu.

 

Hayo mafundisho mawili potofu yanapelekea kwenye tatizo lingine tena la kukana wokovu, linalohusiana na Roho Mtakatifu.

 

Ni sahihi kabisa kusema kwamba waamini wote wa kweli wanaye Roho Mtakatifu akikaa ndani yao. Maandiko yanafundisha kwamba ni muhimu kuwa na Roho Mtakatifu, kama tunataka kuwa na wokovu: “Na yeyote asiyekuwa na Roho wa Kristo, huyo si mali ya Kristo” (Warumi 8:9, TLR). Tunajua kwamba lazima tuwe watu wa Kristo ili tuokolewe, maana Yesu alisema, “Mimi ndiye njia, kweli na uzima. Hakuna anayekuja kwa Baba bila ya kupitia kwangu” (Yohana 14:6, TLR). Waamini wa kweli wamenunuliwa kwa bei kubwa – wao ni watumwa wa hiari na upendo wa Bwana Yesu. Ni mali yake. Ona 1Wakor. 6:20 na 7:23.

 

Nadhani viongozi wengi wa kanisa wanaamini kwamba Roho Mtakatifu hukaa ndani ya wale “wanaomkubali Yesu kama Mwokozi”. Lakini je, ndivyo Maandiko yanavyosema?

 

Yesu alituambia jinsi na masharti ya Roho Mtakatifu kutolewa, kama ifuatavyo: “Mkinipenda, mtatii ninayoamuru. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Mshauri mwingine awe nanyi milele – Roho wa kweli” (Yohana 14:15-17, TLR). Sharti ni kwamba lazima tujitolee kumtii Yesu kwa upendo. Ndipo atamwomba Baba ambaye atatupa Roho Mtakatifu. Maandiko yanathibitisha fundisho hilo katika Matendo 5:32, mahali ambapo Petro anawatetea wanafunzi mbele ya Baraza Kuu La Wayahudi (Sanhedrin). Akizungumza juu ya Roho Mtakatifu, Petro alisema hivi: “… Roho Mtakatifu, ambaye Mungu amewapa wale wanaomtii” (TLR).

 

Yesu alieleza mahusiano yatokanayo na utii kwa amri Zake.

 

“Yeyote mwenye amri Zangu na kuzitii, huyo ndiye anipendaye. Yeye anipendaye mimi atapendwa na Baba yangu, na mimi pia nitampenda na kujionyesha kwake” (Yohana 14:21, TLR).

 

Akarudia tena kusema, “Mtu yeyote akinipenda, atatii mafundisho yangu. Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kufanya makao yetu pamoja naye. Yeye asiyenipenda hatatii mafundisho yangu. Haya maneno mnayosikia si yangu; ni ya Baba aliyenituma” (Yohana 14:22-23, TLR).

 

Ni wale wanaompenda Yesu na kushika amri Zake ndiyo wanapendwa na Mungu Baba, na Yesu. Yesu na Baba watakuja na kufanya makao pamoja na wale wanaompenda na kumtii Yesu.

 

Wale wasiofundishwa kumwamini na kumpokea Yesu kama Bwana wao, bila shaka hawafundishwi hata kumtii. Wale wasiojitolea kumtii Yesu hawatampokea Roho Mtakatifu. Wale wasiompokea Roho Mtakatifu si mali ya Bwana Yesu. Basi, kuhubiriwa Injili kwa ulaghai mwanzoni kabisa – kwamba si lazima Yesu awe Bwana – kumepelekea kuwepo sababu tatu tofauti kwa nini watu kama hao watanyimwa wokovu.

 

Hebu fikiri tena onyo la Yesu la kutisha sana. “Wengi wataniambia siku ile, ‘Bwana! Bwana! Hatukutabiri kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo na kufanya miujiza mingi?’ Ndipo mimi nitakapowaambia waziwazi kabisa, ‘Sikuwajua ninyi kamwe. Tokeni mbele yangu, ninyi watenda maovu!’ [yaani, msiofuata sheria]” (Mathayo 7:22-23, TLR). Ni watu gani hao ambao Yesu hakuwajua kamwe? Ni wale ambao hawakumpokea Yeye kama Bwana, hawakumtii, wala hawakupokea Roho Mtakatifu. Lakini, si walitabiri kwa jina Lake, wakatoa pepo na kufanya miujiza mingi kwa jina Lake? Ndiyo, kabisa. Hiyo ndiyo sehemu ya udanganyifu wenyewe, ambao hata sasa uko kanisani. Kwani, Yesu hakutoa onyo? “Kwa sababu, maKristo wengi wa uongo na manabii wengi wa uongo watatokea na kufanya ishara kubwa na miujiza ili kuwadanganya hata wateule – ikiwezekana” (ktk Mathayo 24:24, TLR). Watadanganya kwa kufanya mambo haya katika jina la Yesu.

 

Kanisa lenye kukosa mafundisho kuhusu haja ya kutii, na ambalo haliwezeshwi na nguvu za Roho Mtakatifu limedanganywa na mahubiri ya kilaghai ya Injili. Ni sehemu ya utamaduni wa Kikristo unaoweza kuitwa UKanisa. Hauna nguvu wala uwezo wa kupambanua. Umepoa; washirika wake huwezi kuwatofautisha na watu wa dunia, na si ajabu linabadilisha imani za msingi mara nyingi. Mwishowe litafika mahali pa kuwa na maswali kuhusu Maandiko kutokuwa na makosa, kwamba Yesu ni Mungu, na ukweli kuhusu ufufuo. Pengine linaruhusu dhambi waziwazi katika kanisa na madhabahuni kwa kukubali uzinzi, uasherati, watu walawiti na mashoga na kwa kuwaingiza katika huduma wachungaji ambao ni walawiti na mashoga. Makanisa kama hayo yanaweza pia kufukuzia madhihirisho mbalimbali yanayodhaniwa kuwa ni ya Roho lakini yasiwe na uwezo wa kupambanua kama madhihirisho hayo kweli ni ya Roho Mtakatifu.

 

Je, maelezo hayo yanasema juu ya baadhi ya makansia gani leo? Naogopa kwamba makanisa yetu mengi ni sehemu ya UKanisa. Hayajatia nanga imara juu ya mwamba usiobadilika, usiosogezwa – Bwana Yesu na maneno Yake.

 

Katika mahakama, ulaghai ni kitu kinachoweza kushughulikiwa. Mikataba inaweza kubatilishwa kama ulaghai utatumika kumlazimisha mtu kuingia katika mkataba. Viongozi wa makanisa mengi hutoa matamshi ya kilaghai yanayowalazimisha watu kufanya maamuzi yatakayobadilisha maisha yao. Maamuzi haya yana matokeo mazito sana. Wale wenye kuamini na kukubali matamshi hayo ambayo ni ya kilaghai pengine huhakikishiwa kwamba wamekwisha fanya kila kinachohitajika ili kupata uzima wa milele. Watatoa fedha kwa kanisa lao na wakati mwingine watatumika katika wadhifa fulani. Wanatumia muda wao, wakati mwingine kwa kujitolea kabisa, na kuacha mambo mengine. Wakishawishiwa kufanya maamuzi kutokana na ulaghai, matokeo yanaweza kusababisha uharibifu usiopimika. Hao watu hawatakosa imani yenye kuokoa tu na kwa hali hiyo wasiwe na wokovu, bali wanaweza pia kuvurugikiwa kabisa kiasi cha kutokuwa tayari kufanya uamuzi wa kujitoa kwa Bwana Yesu.

 

Miaka mingi iliyopita nilianza kuwa na mashaka kwamba mojawapo kati ya ushahidi wa ulaghai katika kutangazwa kwa injili ni ile idadi kubwa ya watu ambao wanaliacha kanisa haraka sana baada ya “kujitoa”.

 

Kitabu cha Ray Comfort kiitwacho The Way of the Master (kitolewacho na Bridge-logos) kikathibitisha mashaka yangu. Ndugu Ray alitaja takwimu za dhehebu kubwa sana la Marekani ambalo lilitangaza kwamba watu 294, 784 waliamua kumfuata Kristo mwaka wa 1990. Lakini, mwaka wa 1991, dhehebu hili lilifanikiwa kupata watu 14, 337 tu katika ushirika wa Kikristo. Wale wengine 280, 447 waliofanya uamuzi hawakujulikana wako wapi. Uongozi haukuwa na habari kwa nini hayo yalitokea, na jibu la mwisho walilotoa ni kwamba, “Kuna kitu ambacho hakiko sawa!” Mambo yakaendelea. Mwezi Agosti mwaka wa 1996, dhehebu lingine kubwa la Marekani likadhihirisha kwamba mwaka wa 1995 lilifanikiwa kupata watu 384,057 walioamua kumfuata Yesu, lakini waliobakia katika ushirika ni 22,983 tu. Halikuwa na la kusema kuhusu wale wengine 361,074 waliodhaniwa kuwa wamekata shauri. Ray akaeleza juu ya mkutano mwingine wa Injili ambao ulipata watu 600 waliokata shauri, bila shaka kukiwa na shangwe kubwa sana. Lakini baada ya siku 90, watenda kazi wafuatiliaji hawakuweza kumpata hata mtu moja aliyekuwa anaendelea katika imani. Mwaka wa 1991 huko Cleveland jimbo la Ohio, watu 400 walikata shauri katika mahubiri ya kuwafikia watu mjini, lakini tena, hakuna hata mtu mmoja aliyepatikana ambaye aliendelea na imani.

 

Ndugu Ray akamkariri Ndugu Mchungaji Charles E. Hackett, Mkurugenzi Kitaifa wa Idara ya Utume wa Ndani wa Assemblies of God ya Marekani, hivi: “Roho ya mtu madhabahuni haisababishi msisimiko sana katika maeneo mengine kwa sababu tunatambua kwamba kiasi cha watu 95 katika kila watu 100 hawataingia kanisani. Ukweli ni kwamba, wengi wao hata hawatarudi mara ya pili.”

 

Hiki si kitu cha Marekani tu. Kulingana na Ndugu Ray, mchungaji mmoja wa mjini Boulder jimboni Colorado alituma timu ya watu kwenda Urusi mwaka wa 1991, na watu 2,500 wakakata shauri. Mwaka uliofuata waliporudi walikuta watu 30 tu wakiendelea na imani. Huko mjini Leeds Uingereza, mhubiri mgeni kutoka Marekani alifanikiwa kupata watu 400 kufanya uamuzi kwa ajili ya kanisa la mahali. Lakini, baada ya majuma sita, ni wawili tu waliokuwa wanaendelea, nao wakaanguka baadaye. Mchungaji aliyesafiri kwenda India kila mwaka tangu mwaka wa 1980 alimwambia Ndugu Ray kwamba aliona kadi 80 elfu za wakata shauri zikiwa zimepangwa katika kibanda fulani mjini Rajamundry, “matokeo” ya mikutano ya uinjilisti iliyopita. Lakini akataja kwamba mtu angekuwa na bahati sana kama angepata hata Wakristo 80 katika mji huo. Kiwango hicho ni moja ya kumi ya asilimia moja.

 

Ndugu Ray pia anataja takwimu za kituo cha utafiti cha Barna, zilizoonyesha kwamba asilimia 62 ya WaMarekani wanasema wao wana uhusiano wenye maana na Yesu Kristo. Lakini, utafiti uliofanywa na Gallup wakati kama huo huo ulidhihirisha kitu cha ajabu kuhusu kundi maalum la asilimia 6 hadi 10 la WaMarekani wanaosema ni Wakristo. Anasema hivi Bwana Gallup kuwahusu hao:

 

“Watu hawa ni watu wa kipekee sana … wanawavumilia watu kutoka mazingira tofauti. Wanahusika katika shughuli za kusaidia watu. Wanahusika katika Ukristo wa vitendo. Tena, wamejitoa kikamilifu kabisa kwa maombi.”

 

Ndugu Neil Anderson katika kitabu kiitwacho The Bondage Breaker, ukurasa wa 107, anataja takwimu inayofanana, hivi: “Kwa maoni yangu, hakuna zaidi ya asilimia 15 ya jamii ya Kikristo yenye kuamini Injili ambo wako huru na utuma wa Shetani.” Ingawa Neil anazungumza kwa ukarimu sana juu ya waliobaki kwamba ni Wakristo, kutokana na jinsi anavyowaelezea, wanazo tabia za wale waliotajwa katika Wagalatia, Waefeso na Ufunuo, ambao (kama Maandiko yanavyosema) hawana urithi katika Ufalme wa mbinguni.

 

Mkazo wa Ndugu Ray Comfort ni kwamba hatusemi ukweli – hapo tena, ulaghai na udanganyifu – tunapowaleta watu kwa Kristo. Kwa hiyo, mbegu inaangukia kwenye udongo wenye miamba, na hata ingawa inapokelewa kwa furaha, mtu mwenye anaanguka upesi katika nyakati ngumu au za mateso.

 

Kabla ya kutazama swala la udanganyifu katika uenezwaji wa Injili, inabidi tutazame mfano ufuatao wa ulaghai ambao upo mara nyingi, na ambao hupelekea kwenye udanganyifu tutakaotazama katika sura inayofuata.

 

Wokovu ni zawadi. Maandiko yanasema hivyo katika Warumi 6:23. “Kwa sababu, malipo ya dhambi ni kifo, lakini zawadi ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (TLR). (Ona pia Waefeso 2:8-10) Ulaghai ni jinsi zawadi hiyo inavyoelezwa. Mara nyingi mchungaji, mwalimu au mwinjilisti atasema, “Wokovu ni zawadi ITOLEWAYO BURE! Haikugharimu chochote!”

 

Je, ni bure? Kama kuna gharama, ni zipi? Hapo tu ndipo mtu anaweza kuamua kama yuko tayari kulipa gharama inayotakiwa. Yesu alifundisha kwamba mtu yeyote anayeamua kumfuata lazima ajue gharama kwanza. La sivyo, anaweza kushindwa kumalizia, naye atadhihakiwa. Ona Luka 14:28-30.

 

Pengine unajikuna kichwa katika akili zako ukifikiri, “Mimi nilidhani wokovu ni bure, na kwamba Yesu alilipa gharama yote pale Kalvari.” Kama ilivyo kwa ulaghai mwingi na udanganyifu, sehemu ya jibu hilo ni sahihi. Wokovu si bure, lakini Yesu alilipa gharama yote kwa ajili ya msamaha wa dhambi zetu pale Kalvari. Yesu alifanya iwezekane sisi kuokolewa kwa kuimwaga damu Yake na kufa kwa ajili yetu. Damu Yake iliyomwagika ilituruhusu sisi kusamehewa dhambi zetu; kwa kifo Chake alifanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu na kufanya iwezekane sisi kupatanishwa na Mungu. Hiyo ndiyo zawadi ambayo kwa neema (upendeleo tusiostahili) ilitolea kabla sisi hatujajua kuiomba. Lakini, wakati mwingine inasemekana hivi, na ni sahihi kabisa, “Wokovu ndiyo zawadi iliyo ghali kuliko yoyote unayoweza kupokea. Inagharimu kila kitu ulicho nacho!”

 

Gharama za wokovu na msamaha wa dhambi hazimaanishi kwamba vitu hivyo vinapatikana kwa kufanya chochote. Hakuna tunachoweza kulipa au kufanya ili tupate wokovu. Lakini Yesu alituambia kuhusu gharama (au masharti basi) ambazo ni lazima ili tustahili kupokea zawadi ya wokovu na uzima wa milele. Wengine wanaziita “masharti ambayo lazima yatoshelezwe” ili kupokea uzima wa milele. Mimi wakati mwingine ninaziita “Maswala ya wokovu”.

 

Labda nifafanue masharti hayo kwa njia hii. Tuseme kwamba umenunua gari jipya miezi kadhaa iliyopita na mwuzaji akakutumia taarifa kwamba watu wote walionunua aina hiyo ya gari na mwaka huo kutoka kwa mnunuzi wana fursa ya kubadilishwa mafuta ya injini bure. Hili ni toleo la kubadilishiwa mafuta ya injili kwa watu kikundi kidogo – wale watakaotimiza masharti hayo. Masharti ni kwamba uwe ulinunua aina hiyo ya gari na iwe ya mwaka huo, kutoka kwa huyo mwuzaji. Ukienda kwa mwuzaji huyo kutafuta kubadilishiwa mafuta ya injili na huna gari aina hiyo, huwezi kupata huduma hiyo. Ukienda na uwe na gari la zamani zaidi kuliko ule mwaka uliotajwa, huwezi kupata huduma hiyo. Na ukinunua gari aina inayotakiwa na mwaka unaotakiwa kutoka kwa mwuzaji mwingine, huwezi kupata huduma hiyo. Inabidi utimize masharti. Ukiyatimiza, kubadilishwa mafuta ya injili hakutakugharimu chochote. Ni bure kwa kila atakayetimiza masharti husika.

 

Vivyo hivyo, Mungu kwa neema ametoa zawadi ya wokovu kwa wote wanaotimiza masharti.

 

Hebu sasa tutazame masharti (au gharama) ambayo Yesu alisema ni ya lazima ili mtu apate wokovu. Hebu tuyatathmini tuone kama watafutaji – yaani, watu wanaofikiri kuwa wafuasi wa Bwana Yesu – wanapaswa kuambiwa masharti haya kabla ya kufanya uamuzi wa kumfuata Yesu. Masharti hayo yote yanapatikana katika mafundisho na amri za Yesu. Wewe na mimi tunaweza kuyatimiza yote  kwa kutii mafundisho na amri za Yesu.

Sura Ya Nane

(Chapter 8)

 

Mtoto Mwingine Wa Kupinga Sheria: Udanganyifu Katika Kuhubiri Injili

(Another Child Of Antinomianism: Deceit In The Presentation Of The Gospel)

 

Hebu tutofautishe udanganyifu na ulaghai. Ulaghai unahusisha kusema au kuonyesha kitu cha uongo kwa kusudi la kuwafanya wengine waamini kitu hicho au maneno hayo kwa hasara yao. Udanganyifu ni kuondoa kweli muhimu kwa kusudi la kumfanya mtu atende kitu kwa hasara yake. Katika yote mawili, sharti la kuwa makusudi pia hutoshelezwa kwa kutokujali ukweli. Ukweli uko dhahiri na wazi kabisa kutokana na Neno la Mungu, kama tunavyoweza kuona hapa. Wakati “injili nyingine” inapotajwa ambayo iko tofauti na Neno la Mungu, ni ulaghai kama ni maelezo ya uongo, au ni udanganyifu kama kuna kuondolewa au kupunguzwa kwa kweli muhimu, ambazo zinaweza kumfanya mtu kutenda kwa hasara yake. Kupinga Sheria na usalama wa wokovu milele bila masharti huhusisha ulaghai na udanganyifu pia.

 

Kuunganika kwa ulaghai na udanganyifu pengine ndiyo sababu inayofanya asilimia 95 au zaidi ya watu “wanaokata shauri” kuanguka haraka tu. Mambo ni makubwa sana maana ulaghai na udanganyifu katika kutangaza Injili huwagharimu mamilioni ya watu wokovu wao. Kwa kujua au kutokujua, wachungaji wengi na waalimu wanamwasi Bwana Yesu na Neno Lake. Kwa makusudi au vinginevyo, wanafuata mafundisho ya wanadamu badala ya mafundisho na amri za Bwana Yesu. Wanafuata na kueneza itikadi za uongo. Sura hii inashughulikia uasi kwa njia ya udanganyifu.

 

Hebu tutumie mfano halisi wa kutusaidia kuelewa udanganyifu. Tuseme unakwenda kununua gari lililotumika, na sheria inamtaka mwuzaji kuwaambia wanunuzi watarajiwa kila kitu kilicho kibaya katika hilo gari – hasa vile ambavyo haviwezi kuonekana kwa kulitazama tu. Tuseme umekwenda kwenye eneo wanalouza magari yaliyotumika, ukaona gari ambalo ndilo ungetaka, na bei yake unaiweza. Mwuzaji akutembeze ulitazame gari, akikuonyesha vitu mbalimbali vya gari, lakini asiseme chochote kuhusu matatizo ya gari lenyewe. Halafu unalinunua.

 

Baada ya muda unagundua kwamba kuna kitu kisichokuwa sawa na breki za gari. Fundi magari mmoja anakwambia kwamba zimekwisha kabisa. Halafu moshi mweusi unaanza kuonekana. Ukichunguza zaidi unagundua kwamba injini ina tatizo, itahitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa. Halafu gia zinaanza kusumbua. Itabidi kutengeneza, lakini ni kwa gharama kubwa sana.

 

Nini kimetokea? Je, mwuzaji amekulaghai kwa kukudanganya? Hapana, tatizo liko kwenye kile ambacho hakusema – udanganyifu wake. Hakusema kwamba alijua (au alipaswa kujua) kilichoharibika katika gari, ingawa sheria inamtaka akwambie mambo hayo yote. Kwa sababu ya udanganyifu wake, utakuwa na haki ya kumfungulia mashtaka ili kubatilisha biashara mliyofanya na fedha yako irudishwe.

 

Mfano huu unahusikaje katika kuhubiri Injili kwa asiyeamini? Yesu alituambia kwamba tunapaswa kumwambia asiyeamini gharama ambazo ni za msingi kuhusiana na uamuzi wake wa kumfuata Yesu. Yesu alitumia mfano ili kufundisha juu ya kupewa habari zote – kujua gharama – kabla ya kufanya uamuzi wa kumfuata.

 

“Au tuseme kwamba mmoja wenu anataka kujenga mnara. Hataketi kwanza chini na kukadiria gharama ili aone kama ana fedha ya kutosha kumaliza ujenzi wake? Kwa sababu, kama ataweka msingi na ashindwe kumaliza, kila mtu atakayeuona atamdhihaki na kusema, ‘Huyu mtu alianza kujenga, akashindwa kumaliza’.” (ktk Luka 14:28-30, TLR).

 

Takwimu za wanaofanya maamuzi ya kumfuata Kristo zinaonyesha kwamba asilimia 95 hawakuweza kumaliza, au hawakutaka kumaliza. Kwa nini? Sababu moja inaweza kuwa ulihakikishiwa kwamba hakuna gharama – uliambiwa wokovu ni zawadi itolewayo bure, lakini baadaye unakuta kwamba kuna gharama nyingi. Basi hapo unajua kwamba umedanganywa. Au, kama ulihakikishwa kwamba baada ya kufanya uamuzi huo wewe umeokoka milele na huwezi kupotea, basi ni kwa nini kuhangaika na kuendelea kanisani? Tayari una kinga ya maisha yako mpaka milele.

 

Zipo gharama katika kumfuata Yesu. Hizo “gharama” pia zinaweza kuitwa “masharti” au “sifa” – kitu ambacho lazima tufanye ili kustahili kupata wokovu. Ingawa nitatumia maneno hayo kwa kubadilishana hapa na pale, maana yake ni ile ile. Sura hii itataja masharti mengi ambayo lazima tuyatimize ili tuweze kustahili kupata wokovu.

 

Je, kanisa mara nyingi linadanganya linapowashawishi watu kumfuata Yesu? Wewe utaamua baada ya kupitia baadhi ya gharama, masharti au sifa ambazo Yesu alizungumzia.

 

Sharti la kwanza na ambalo ni maarufu sana, linapatikana katika Yohana 3:16.

 

“Kwa maana, Mungu aliipenda dunia sana hata akamtoa Mwanawe pekee, ili yeyote atakayemwamini asipotee bali awe na uzima wa milele” (TLR).

 

Je, mstari huu unasema kila mtu ataokolewa? Hapana. Ahadi (na sharti) ni “yeyote atakayemwamini Yeye hatapotea bali atakuwa na uzima wa milele.” Vipi kuhusu wale wasioamini? Yesu aliendelea. “Yeyote amwaminiye Yeye hahukumiwi, lakini yeyote asiyeamini amekwisha kuhukumiwa kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu” (Yohana 3:18, TLR). Yesu anathibitisha hilo katika Yohana 3:36. “Yeyote amwaminiye Mwana anao uzima wa milele, lakini yeyote anayemkataa Mwana hatauona uzima, kwa sababu hasira ya Mungu inabakia juu yake” (TLR).

 

Nadhani sasa ume-elewa maana ya “kustahili”. Zawadi ya uzima wa milele inapatikana kwa wote. Kustahili kupata uzima wa milele, mtu lazima “amwamini Yeye”, yaani, awe na imani yenye kuokoa. Hapo ndipo makanisa mengine hutenda udanganyifu. Yanashindwa kueleza kwa ukweli kile kinachohitajika ili mtu awe na imani yenye kuokoa. Wanashindwa hata kueleza nini maana ya kumwamini Yesu kweli. Utapata maelezo marefu na sahihi kabisa kuhusu mada hii kwenye tovuti hii: www.bereanpblishers.com |tafuta Book: Imani Yenye Kuokoa | halafu tafuta Sura ya Kwanza: Mwamini Yeye.

 

Mara nyingi imani hufafanuliwa kama dhana yenye upande mmoja, kana kwamba kukubali kiakili tu kunatosha. Imani yenye kuokoa, kama inavyofafanuliwa na Yesu katika Maandiko, ni kama almasi yenye sura mbalimbali. Kwa mbali, almasi inaonekana kama kitu kimoja tu, sawa tu na imani. Lakini, unapoitazama kwa ukaribu sana utaona sura zake mbalimbali – kila moja iking’aa sana kuonyesha mwanga, sawa na zile aina tofauti za imani yenye kuokoa.

 

Ufuatao ni mfano kutoka katika fani ya sheria, wa kusaidia kufafanua jambo hili, kwamba imani ina sehemu nyingi au sura nyingi. Tafsiri ya Sheria ya Kawaida kuhusu wizi ni kwamba, ni tendo la kuvunja na kuingia katika nyumba wanamoishi watu usiku ili kufanya uhalifu. Mambo hayo yote lazima yawepo ili wizi uwe umefanyika. Kama haikufanyika usiku, si wizi. Kama si nyumba ya kuishi, si wizi. Kama tendo la kuvunja na kuingia halikufanyika, huo si wizi. Kama si kwa kusudi la kufanya uhalifu, huo si wizi. Yaani, sehemu  hizo zote lazima ziwepo ili hatia hiyo ikamilike kisheria.

 

Vivyo hivyo, kama sehemu yoyote muhimu katika imani yenye kuokoa haipo, si imani yenye kuokoa hiyo, na mhusika huyo hatapata uzima wa milele. Kama hatuelewi kwamba imani yenye kuokoa ina sehemu mbalimbali, tutaifafanua isivyo na kufanya udanganyifu katika kuieleza Injili. Sehemu muhimu ya imani yenye kuokoa inaweza mara moja kutambulika kwa sababu Yesu alisema kwamba bila hiyo huwezi kuokolewa. Mifano ya masharti ya wokovu ni kama ifuatavyo: bila hiyo huwezi kuwa mwanafunzi wake, hutaingia katika ufalme wa mbinguni, huwezi kusamehewa dhambi zako, atakukana mbele za Baba, utakatiliwa mbali na kuchomwa, na umeamini bure.

 

Dkt. John R. Armstrong aliandika hivi: “Hakika, hapa ndipo penye kitu kinachokosekana kabisa katika mahubiri karibu yote ya ki-injili ya siku zetu. Tumeifanya imani kuwa ni kitu cha kukubali tu, kama ni uamuzi, au kama ni kitu cha kutambua tu. Lakini, imani kwa maana yake halisi inalingana na utii.”

 

Utii ndiyo sehemu muhimu zaidi katika imani yenye kuokoa. Ndicho kitu kilicho juu ya vyote, na ndani yake kuna hivyo vingine ambavyo ni kama sehemu zake ndogo. Tunaona haya kutokana na maneno ya Yesu katika Mathayo 7:21, kwamba:

 

“Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana’ atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye tu afanyaye mapenzi ya Baba Yangu aliye mbinguni” (Mathayo 7:21, TLR).

 

Ni wale tu wenye kutii – wanaofanya “mapenzi ya Baba yangu” – ndiyo watakaoingia katika ufalme wa mbinguni. Hapo basi tunapata kuona kwamba kutii mapenzi ya Mungu ni sehemu muhimu na nyeti kabisa ya imani yenye kuokoa. Bila hiyo huwezi kuokoka na kwenda mbinguni. Mwandishi wa Waebrania naye anasema hayo hayo, kama ifuatavyo: “Yeye [Yesu] alifanyika chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii” (Waebrania 5:9, TLR).

 

Yesu alisema kwamba kila alichosema na kufanya wakati akiwa hapa duniani kilikuwa ambacho Baba Yake alimwambia kusema na kufanya (Yohana 8:28; 12:49-50; 14:10; 14:24 na 14:31). Basi, kila kitu alichosema Yesu na kufanya kilikuwa mapenzi ya Mungu. Basi, haishangazi kwamba Yeye ndiye chanzo au asili ya wokovu kwa ajili ya wote wanaomtii. Wala si ajabu kwamba alimalizia agizo lake kuu kwa kutoa amri kwamba wanafunzi wapya wafundishwe kutii yote ambayo Yeye aliwaamuru (Mathayo 28:20).

 

Kutii mafundisho ya Yesu na amri Zake ni muhimu ili kupata wokovu. Mara moja utaona kwamba kutii sehemu hizo za imani yenye kuokoa ni kitu kisichokubaliana na zile itikadi za uongo za Kupinga Sheria na usalama wa wokovu milele bila masharti. Kila sehemu ni mafundisho au amri ya Yesu – ni sehemu ya “Sheria ya Kristo”. Haya mafundisho ya uongo yanadai kwamba kutii sheria yoyote si kitu kinachotakiwa kwa ajili ya wokovu. Wanadai kwamba wokovu unategemea unachoamini na kwamba mwenendo hauna maana yoyote.

 

Sasa tutarudia baadhi ya sehemu imani yenye kuokoa kutoka katika mafundisho na amri za Yesu. Kinyume na mafundisho ya Kupinga Sheria na usalama wa wokovu milele bila masharti, utaona kwamba amri baada ya amri inasema kwamba huwezi kupata wokovu (au hutaingia ufalme wa mbinguni) usipofanya inavyosema. Sasa utaelewa kwa nini kuna bonde kubwa kati ya wokovu wa KiBiblia na ule wokovu bandia, wa kufikirika tu, unaohubiriwa na Wapinga Sheria na wale wanaodai kwamba kuna usalama wa wokovu milele bila masharti.

 

Nimeanza kila amri kwa maneno haya – “Yesu alisema” ili kusisitiza katika akili yako kwamba kila moja ya mafundisho haya na amri hizi zilitoka kwa Yesu moja kwa moja, na basi ilitoka kwa Mungu moja kwa moja. Nataka pia kusisitiza umuhimu wa kufundisha wengine kutii mafundisho na amri za Yesu, kama alivyotuagiza kufanya.

 

            Ni lazima tutubu. Yesu alisema hivi: “Lakini msipotubu, ninyi pia mtaangamia wote” (Luka 13:3, 5, TLR). Amri ya kwanza ya Yesu ilikuwa, “Tubuni, kwa sababu ufalme wa mbinguni uko karibu” (Mathayo 4:17, TLR). Hakika Yesu hakuwa anazungumza juu ya kifo cha kawaida (maana wasikilizaji wake wote wangepitia kifo siku moja). Badala yake, alikuwa anawaonya kuhusu kuangamia kiroho kama wasingetubu.

 

            Ni lazima tuzaliwe mara ya pili. Yesu alimwambia Nikodemu hivi, “Kweli nakwambia, hakuna mtu anayeweza kuuona ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili” (Yohana 3:3, TLR). Wale wenye imani yenye kuokoa wamezaliwa mara ya pili. Imani yenye kuokoa (na kuzaliwa mara ya pili) ni pamoja na kujitolea kutii amri za Yesu (Yohana 14:15-17). Je, mtu anaweza kuuona ufalme wa Mungu bila ya kuzaliwa mara ya pili? Hapana. Yesu alisema, ni sharti muhimu kabisa.

 

            Ni lazima tuwe wenye haki kuliko Mafarisayo. Yesu alisema, “Nawaambia hivi, haki yenu isipozidi ile ya Mafarisayo na waalimu wa Torati, hakika hamtaingia katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 5:20, TLR). Yesu alisema hivi kuhusu Mafarisayo na waalimu wa Torati, “Lakini, msifanye wanayofanya, kwa sababu wao hawatendi kulingana na mahubiri yao” (TLR). Sisi kama wafuasi wa Yesu lazima tuwe watendaji, si wasikiaji tu.

 

Kama alivyosema Yakobo, “Msisikilize neno tu, na kwa njia hiyo kujidanganya wenyewe. Fanyeni linachosema” (Yakobo 1:22, TLR).

 

            Tusifanye uovu. Yesu alisema, “Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao wataondoa katika ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi, na wote watendao maovu”. Ona Mathayo 13:40-43.

 

            Tusiwe watu waovu. Yesu alisema hivi: “Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia. Malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” Ona Mathayo 13:47-50.

 

            Ni lazima tusamehe. Yesu alifundisha hivi: “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu wa mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu” (Mathayo 6:14-15). Yesu alifafanua hayo katika mfano aliosimulia katika Mathayo 18:21-35. Mfalme aliyekuwa amemsamehe mtumishi wake deni kubwa alilirudisha lile deni wakati mtumishi alipokataa kumsamehe mtumishi mwenzake. Yesu akasema: “Kwa hasira, bwana wake akamkabidhi kwa askari magereza ili ateswe, mpaka atakapolipa kila kitu alichokuwa anadai” (Mathayo 18:34, TLR). Sehemu ya kutisha katika kisa hicho inapatikana katika mstari unaofuata. Yesu alisema, “Hivyo ndivyo Baba Yangu wa mbinguni atakavyowafanyia kila mmoja wenu, msipowasamehe ndugu zenu kutoka moyoni” (Mathayo 18:35, TLR). Wale wanaokataa kusamehye watapokea adhabu ya wasioamini – mateso milele Jehanamu – kwa sababu hakuna yeyote kati yetu anayeweza kulipa deni la dhambi zetu yeye mwenyewe.

 

            Ni lazima tumpende Yesu kuliko mtu mwingine yeyote, na kuliko maisha yetu. Yesu alisema hivi: “Mtu yeyote akija kwangu naye hamchukii baba yake na mama yake, mke wake na watoto, ndugu zake na dada zake – naam, hata maisha yake mwenyewe – hawezi kuwa mwanafunzi wangu” (Luka 14:26, TLR).  Amri yetu ya kusonga mbele ni “kufanya watu kuwa wanafunzi katika mataifa yote” (Mathayo 28:19, TLR). Kweli, hakuna mtu anayeweza kusema kwamba tunaweza kuokoka kama sisi si wanafunzi wa Yesu.

 

            Ni lazima tujikane wenyewe, tujitwike msalaba wetu na kumfuata Yesu. Yesu alisema, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, lazima ajikane mwenyewe na kubeba msalaba wake, na kunifuata” (Mathayo 16:24, TLR). Tusipomfuata Yesu hatuwezi kuwa na uzima wa milele.

 

            Hatupaswi kumkataa au kumkana Yesu. Yesu alisema, “Yeyote anayenikiri mbele ya watu, hata Mimi nitamkiri mbele za Baba yangu wa mbinguni. Lakini, yeyote anikataaye mbele za watu, hata Mimi nitamkataa mbele za Baba Yangu wa mbinguni” (Mathayo 10:32-33, TLR).

 

            Ni lazima tudumu katika imani. Yesu alionya hivi: “Watu wote watawachukia kwa sababu Yangu, lakini, yeye atakayesimama imara mpaka mwisho, ataokoka” (Mathayo 10:22, TLR). Paulo alithibitisha kweli hiyo, hivi: “Basi ndugu zangu, nawaqarifu ile Injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, na kwa hiyo mnaokolewa, ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri, isipokuwa mliamini bure” (1Wakor. 15:1-2).

 

            Ni lazima tuzae matunda. Yesu alionya hivi: “Kila tawi ndani yangu lisilozaa  [Yeye Mungu] huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa” (Yohana 15:2). Matawi ndani ya Yesu yalikatwa kwa sababu hayakuzaa matunda yoyote.

 

            Lazima tukae na kudumu ndani ya Yesu. Yesu alisema hivi: “Mtu asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea” (Yohana 15:6).

 

            Lazima tuwe wanyenyekevu kama mtoto mdogo. Yesu alisema hivi: “Kweli nawaambia, yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kamwe” (Luka 18:17, TLR). Ona pia Mathayo 18:3, kwamba, “… msipobadilika na kuwa kama watoto wadogo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.” (TLR)

 

            Lazima tufanye mapenzi ya Mungu. Yesu alisema hivi: “Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.” Amri hii inahusu kila kitu ambacho Yesu alifundisha na kuagiza. Kila kitu alichosema Yesu ni mapenzi ya Mungu.

 

            Tusiwafanye watoto kutenda dhambi. Yesu alisema hivi: “Bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa katika kilindi cha bahari. Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha, lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!” (Mathayo 18:6-7)

 

            Tusiendelee kufanya dhambi. Yesu alisema, “Basi mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe. Ni afadhali kuingia katika uzima hali umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele. Na jicho lako likikukosesha, ling’oe ukalitupe mbali nawe. Ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili na kutupwa katika Jehanamu ya moto” (Mathayo 18:8-9). Yesu hakubali mwenendo wa dhambi.

            Tusitamani. Yesu alisema, “Mmesikia kwamba imenenwa, ‘Usizini’. Lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake” (Mathayo 5:27-28). Wayahudi walijua kwamba wazinzi wote wamehukumiwa –walitakiwa kuwapiga mawe mpaka kufa. Paulo ndiye aliyeunganisha uzinzi na hukumu ya Mungu moja kwa moja, hivi: “Msidanganyike: waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi” (1Wakor. 6:9-10). Hayo yote ni mwenendo.

 

            Hatupaswi kuachana katika ndoa, isipokuwa kwa sababu ya kutokuwepo na uaminifu katika ndoa. Yesu alisema hivi: “Mimi nawaambia kwamba, yeyote amwachaye mke wake, isipokuwa kwa sababu ya kutokuwa mwaminifu katika ndoa, anamfanya kuwa mwasherati, na yeyote amwoaye huyo mwanamke aliyeachwa anafanya uasherati” (Mathayo 5:31-32, TLR).

 

            Hatupaswi kuwa na ndoa nyingine kama tumeachwa isivyostahili. Yesu alisema hivi: “Mimi nawaambia, yeyote amwachaye mke wake, isipokuwa kwa sababu ya kutokuwa mwaminifu katika ndoa, na kuoa mwanamke mwingine, anafanya uasherati” (Mathayo 19:9).

 

            Hatupaswi kuwa watenda maovu (au, wasiofuata sheria yoyote). Yesu alisema, “Siku ile wengi wataniambia, ‘Bwana! Bwana! Hatukutabiri katika jina lako, na kwa jina lako tukatoa pepo na kufanya miujiza mingi?’ Ndipo mimi nitakapowaambia wazi wazi kabisa, ‘Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu’!” (Mathayo 7:22-23, TLR). Neno “watenda maovu” linaweza kufasiriwa hapa kama wapinga sheria au wasiofuata sheria yoyote – wale wale watu ambao wanamwasi Bwana Yesu na maneno yake.

 

            Tusitumie maneno bila ya kujali. Yesu alisema, “Mimi nawaambia kwamba, watu watatakiwa kujieleza siku ya hukumu kwa ajili ya kila neno walilosema bila kujali. Maana, kwa maneno yako utawekwa huru, na kwa maneno yako utahukumiwa.” (Mathayo 16:25, TLR).

 

            Tusitake kuyaokoa maisha yetu. Yesu alisema, “Kwa maana, kila anayetaka kuokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata” (Mathayo 16:25, TLR).

 

            Lazima tufanye mambo kwa kufuata njia ya Mungu. Yule mgeni aliyealikwa arusini hakuwa amevaa mavazi ya arusi. Yesu akasema hivi juu ya hilo: “Ndipo mfalme akawaambia wahudumu, ‘Mfungeni mikono na miguu mkamtupe nje katika giza, ambako kutakuwepo kulia na kusaga meno” (Mathayo 22:13, TLR). Ni dhahiri kwamba mwenendo mzuri – mavazi ya arusi – ni kitu kilichotakiwa, sawa tu na utii kwa mafundisho na amri za Yesu – Sheria ya Kristo – unavyotakiwa kwa wale watakao-okolewa. Pamoja na hayo, wale wapinga sheria na wale wenye kuamini kwamba kuna usalama wa wokovu milele bila masharti yoyote wanadai kinyume chake – kwamba, mwenendo hauna maana.

            Lazima tuwe watumishi waaminifu. Yesu anasema kwanza juu ya yule mtumishi mwaminifu ambaye alituzwa na bwana wake. Halafu Yesu akasema, “Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, ‘Bwana wangu anakawia;’ akaanza kuwapiga wajoli wake na kula na kunywa pamoja na walevi; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki. Ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” Ona Mathayo 24:45-52. Katika mfano huu, bwana hakuuliza mtumishi wake alikuwa anaamini nini. Yeye alitazama kazi aliyofanya. Bwana alikuwa ametoa kazi za kufanywa na mtumishi wake. Mmoja alikuwa mwaminifu; mwingine hakuwa. Zilikuwepo sheria na amri ambazo yule mtumishi alipaswa kuzifuata. Mtumishi mwovu alishindwa kufuata sheria zilizokuwa zimewekwa na bwana wake. Mwenendo wake ulikuwa na maana; akahukumiwa.

 

            Lazima tuwe tayari kwa ajili ya kuja kwa Bwana. Yesu alifundisha mfano wa wanawali kumi. Wengine walikuwa na mafuta ya ziada kwa ajili ya taa zao, wengine hawakuwa nayo. Wakati bwana arusi alipokaribia, wale waliokuwa wamejiandaa na kuwa na mafuta ya ziada kwa ajili ya taa zao waliingia pamoja na bwana arusi wakati wale wenzao walipokuwa wamekwenda kutafuta taa. Yesu alisema, “Baadaye, wale wengine nao wakaja. Wakasema, ‘Bwana mkubwa! Tufungulie mlango!’ Lakini yeye akajibu, ‘Kweli nawaambia, siwajui ninyi.’ Kwa hiyo, chungeni, kwa sababu hamjui siku wala saa.” (TLR) Ona Mathayo 25:10-13.

 

            Lazima tutumie talanta zetu vizuri. Katika mfano wa talanta, bwana alitoa talanta za viwango tofauti kwa watumishi watatu. Aliporudi, wawili walikuwa wameziongeza mara mbili. Mmoja alificha yak wake. Yeye akamrudishia bwana wake ile yake moja. Yesu akasema, “… mtupeni huyo mtumishi asiyefaa nje katika giza, ambako kutakuwepo kilio na kusaga meno” (Ona Mathayo 25:26-30, TLR).  Yote hayo yanahusiana na mwenendo. Mtumishi aliyehukumiwa hakuamini kwamba mwenendo wake ni kitu chenye maana.

 

            Tutahukumiwa kulingana na tuliyofanya. Hii inatoka katika mfano wa Yesu kuhusu kondoo na mbuzi. Yesu aliwatenganisha kondoo na mbuzi, akiwaweka kondoo mkono Wake wa kuume, na mbuzi mkono Wake wa kushoto. Akawasifu kondoo kwa kuwajali wale walio ndugu Zake. Halafu anaendelea  hivi: “Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake. Kwa maana nalikuwa na njaa msinipe chakula; nalikuwa na kiu msininyweshe; nalikuwa mgeni msinikaribishe; nalikuwa uchi msinivike; nalikuwa mgonjwa na kifungoni, msije kunitazama.’ … Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.” Ona Mathayo 25:41-43, 46.

 

            Huu mfano ni kisu kikali kabisa moyoni mwa wapinga sheria na wale wenye kuamini kuhusu usalama wa wokovu milele bila masharti. Ingawa wanadai kwamba mwenendo si kitu, mfano huu unahusu mwenendo kabisa. Mwenendo ni kitu cha maana! Cha kusikitisha sana ni kwamba, wengi wanaodai kwamba mwenendo si kitu cha maana watakuwa miongoni mwa wale mbuzi ambao Yesu alisema juu yao kwamba, “watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele.

            Hatupaswi kumwonea Yesu aibu, wala maneno Yake. Yesu alisema, “Kama mtu yeyote atanionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, basi Mwana wa Adamu naye atamwonea aibu atakapoingia katika utukufu wa Baba yake, na malaika wale watakatifu” (Marko 8:38, TLR). Hakutakuwa na wokovu kwa wale wanaomwonea Yesu aibu. Vipi kuhusu wale wasiohubiri kwamba Yesu ni Bwana kwa sababu wanawaogopa wale wanaopinga kwamba Yesu ni Bwana? Je, wanamwonea aibu? Vipi kuhusu wale wanaoshindwa na kukataa kufundisha amri za Yesu kama Yesu alivyowaagiza? Je, wanamwonea Yesu aibu, na maneno Yake?

 

            Lazima tuamini. Yesu alisema, “Nendeni katika dunia yote na kuhubiri habari njema kwa uumbaji wote. Yeyote atakayeamini na kubatizwa ataokoka, lakini yeyote asiyeamini atahukumiwa” (Marko 16:15-16, TLR). Je, Yesu alitazamia kuikuta imani duniani wakati atakaporudi? Yeye Mwenyewe aliuliza hivi: “Wakati Mwana wa Adamu atakapokuja, ataikuta imani duniani?” (Luka 18:8, TLR). Neno “kuamini” ni kitendo, ila “imani” ni jina. Hapa, “kuamini” ni pan asana, kama ambavyo imani yenye kuokoa ilivyo na mengi.

 

            Tusibweteke. Yesu alisema hivi: “Lakini, Ole wenu ninyi mlio na mali, kwa kuwa faraja yenu mmekwisha kuipata. Ole wenu ninyi ambao mmeshiba sasa, kwa kuwa mtaona njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia. Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo” (Luka 6:24-26). Yesu hakutuita kuishi maisha ya starehe, bali ya utumishi na kujitoa.

 

            Lazima tumtii Yesu kama Bwana wetu. Yesu aliuliza, “Mbona mnaniita ‘Bwana, Bwana,’ lakini hamtendi ninayosema?” (Luka 6:46, TLR). Bila shaka Yesu anatutazamia tumtii. Tunaelewa uzito wa utii kwa Yesu tunaposoma onyo la Paulo katika 2Wathesalonike 1:8-10. “Yeye atawaadhibu wale wote wasiomjua Mungu na wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu. Wataadhibiwa kwa kuharibiwa milele na kufungiwa nje ya uwepo wa Bwana, na nje ya enzi ya nguvu Zake …” (TLR)

 

            Wale wasiotii kwa makusudi wataadhibiwa vikali. Yesu alionya hivi: “Mtumishi yule ajuaye mapenzi ya bwana wake, lakini hawi tayari wala hajui bwana wake anataka nini, atapigwa sana” (Luka 12:47-48, TLR). Vipi kuhusu wale wanaojua kwamba amri ya Yesu kwa wafuasi Wake ni kuwafundisha waongofu wapya kutii yote ambayo amewaamuru Yeye, lakini wanakataa kufanya hivyo? Vipi kuhusu kukataa na kutokujali mafundisho na amri za Yesu kunakofanywa na Wapinga Sheria na wale wenye kuamini kuhusu usalama wa wokovu milele bila masharti? Hilo linawahusuje wao? Ona pia Waebrania 10:26, kwamba, “Kama tukiendelea kufanya dhambi kwa makusudi baada ya kupokea ujuzi wa kweli, hakuna dhabihu iliyobakia kwa ajili ya dhambi, bali kuna kutarajia kwa hofu sana hukumu na moto mkali utakaowateketeza maadui wa Mungu” (TLR).

 

            Lazima tupatanishwe na Mungu. Yesu alionya kama ifuatavyo: “Unapokwenda na adui yako mahakamani,  jaribu sana kupatana naye  mkiwa njiani, la sivyo atakuburuza kwa hakimu, na hakimu atakukabidhi kwa askari magereza, naye atakutupa gerezani. Nakwambia, hutatoka mpaka ulipe senti ya mwisho” (Luka 12:58-59, TLR). Hii ni sawa kabisa na lile onyo litolewalo na Yesu kuhusu kutokusamehe katika Mathayo 18:34-35, hivi: “Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji hata atakapoilipa deni ile yote. Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa moyo yenu kila mtu ndugu yake.” Tunajua kwamba hatuwezi kulipa gharama ya kutosha kwa ajili ya dhambi zetu; lazima tupatanishwe na Mungu kwa njia ya Bwana Yesu. Ona Wakolosai 1:21-23.

 

            Ni lazima tufanye kila juhudi kuingia kupitia mlango ule mwembamba. Yesu alisema, “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia  ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.” Wakati walioko nje watakapoomba waruhusiwe kuingia, mwenye nyumba atawajibu, “Siwajui ninyi, wala mtokako.” Wale walioko nje watasema, “Tulikula na kunywa pamoja nawe, na ulifundisha katika mitaa yetu.” Jibu la kutisha litatoka kwa Yesu: “Nawaambia: Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu!” (Ona Luka 13:22-27). Hapa tena, Bwana kuwakataa hao watu hakukutokana na mafundisho yasiyo sahihi, bali uovu wao. Aliwaita watenda maovu. Mwenendo wao mwovu ndiyo uliwahukumu.

 

            Lazima tuachane na kila kitu tulicho nacho ili tuwe wanafunzi wa Yesu. Yesu alisema, ”Yeyote kati yenu asiyeacha kila kitu alicho nacho hawezi kuwa mwanafunzi wangu” (Luka 14:31-33, TLR). Kwani ni ajabu kwamba wapinga sheria wanakataa kukubali mafundisho ya Yesu? Je, hayo mafundisho na amri ni magumu sana kwa makanisa yanayojiita marafiki wa watafutaji kuwaeleza wanaoabudu katika makanisa yao? Kama ni hivyo, bila shaka wanamwonea Yesu aibu na maneno Yake, sivyo?

 

            Lazima tuwe wenye kuaminika. Yesu alisema, “Yeyote anayeweza kuaminiwa na kitu kidogo sana anaweza pia kuaminiwa na vitu vingi, na asiyekuwa mwaminifu kwa vichache hatakuwa mwaminifu pia kwa vingi. Basi, kama hujaweza kuaminika unaposhughulika na mali ya dunia, nani atakayekuamini na mali ya kweli? Na kama hujawa mwaminifu kwa mali ya mtu mwingine, nani atakayekupa wewe mali yako?” (Luka 16:10-12, TLR). Hapa tena mkazo uko kwenye mwenendo! Swala la wokovu ni dhahiri linapofafanuliwa kupitia ule mfano wa talanta.Walikuwepo wale watumishi wawili waliokuwa wanaaminika, na walipata zaidi maana waliwekwa juu ya vitu vingi. Lakini yule mtumishi asiyefaa, aliyefukia talanta yake, alitupwa nje katika giza, mahali penye kulia na kusaga meno. Angalia Mathayo 25:14-30. Ona pia mfano kama huo katika Luka 19:12-26. Katika huu, mtumishi yule asiyefaa aliyeficha fedha yake aliitwa mwovu.

 

            Tunapaswa kuwa waangalifu sana kuhusu hatari za utajiri. Yesu alisimulia hadithi ya tajiri na Lazaro. Akasema hivi: “Alikuwepo mtu tajiri aliyevaa nguo za zambarau na kitani safi, na kuishi kwa starehe kila siku.” Lazaro maskini na yule mtu tajiri wote wakafa. Lazaro akaenda kifuani kwa Ibrahimu, yule tajiri akaenda jehanamu. Ibrahimu akamwambia yule tajiri, “Mwanangu! Kumbuka kwamba katika maisha yako ulipokea vitu vizuri vya kwako, wakati Lazaro alipokea vitu vibaya. Sasa amefarijiwa hapa, nawe uko katika mateso” (TLR). Katika Luka 6:24-26, Yesu alisema hivi: “Ole wenu ninyi mlio na mali, kwa kuwa faraja yenu mmekwisha kuipata.” Yesu pia alionya hivi: “Na wengine, kama zile mbegu katikati ya miiba, hulisikia neno, lakini masumbufu ya maisha haya, udanganyifu wa mali na tamaa ya vitu vingine huja na kulinyonga ile Neno, na kulifanya lisizae matunda!” (TLR) Ona pia Ufunuo 3:15-18. Hapa tena, onyo la kuhukumiwa ni kwa sababu ya mwenendo.

 

            Lazima tuwe waangalifu – makini – tuwe macho wakati wote! Yesu alionya hivi: “Basi jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya, siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo. Kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika hayo yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu” (Luka 21:34-36).

 

            Lazima tumwamini Yeye. Yesu alisema, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika Yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu” (Yohana 3:16-18).

 

            Lazima tumwamini Mungu Baba. Yesu alisema, “Amin amin nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumu bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani” (Yohana 5:24). Kumwamini Baba ni kuamini kila neno alilolisema Yesu, kwa sababu alisema yale tu ambayo Baba Yake alimwambia aseme (Yohana 8:28; 12:49-50; 14:10; 14:24; na 14:31). Kumwamini Baba ni kumtii Mwana.

 

            Lazima tumwamini Mwana – Bwana Yesu. Yesu alisema hivi, “Mimi nina ushuhuda wenye uzito kuliko ule wa Yohana. Kwa sababu, kazi ile ambayo Baba amenipa ili niimalize na ambayo ninaifanya, inashuhudia kwamba Baba amenituma. Naye Baba aliyenituma mwenyewe ameshuhudia juu yangu. Ninyi hamjawahi kuisikia sauti yake wala kuona umbo lake, wala neno lake halikai ndani yenu kwa sababu, hamumwamini aliyetumwa na Yeye. Mnajifunza Maandiko kwa bidii sana kwa sababu mnafikiri kwa njia hiyo mnao uzima wa milele. Hayo ndiyo Maandiko yenye kunishuhudia mimi, lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima” (Yohana 5:36-40). Katika siku zetu, hiyo ni kweli yenye kusikitisha sana. Wachungaji katika mamilioni ya makanisa wanahubiri kutoka Biblia, lakini ni wachache sana wanaothubutu kufundisha maneno ya Yesu ambayo kwa hayo, wasikilizaji wao watapata uzima wa milele.

 

            Ni lazima tuamini kwamba Yesu ndiye, kama alivyosema. Yesu alisema hivi: “Niliwaambia mtakufa katika dhambi zenu. Kama hamtaamini kwamba mimi ndiye, hakika mtakufa katika dhambi zenu” (Yohana 8:24, TLR). Katika Yohana 13:13, Yesu alisema hivi: “Mnaniita ‘Mwalimu’ na ‘Bwana’, na ni sawa maana ndivyo nilivyo.” Alipokamatwa na Wayahudi, kuhani mkuu alimwambia Yesu, “Nakuapisha kwa Mungu aliye hai utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu. Yesu akamwambia, ‘Wewe umesema. Lakini nawaambieni: Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni’.” (Ona Mathayo 26:63-64). Katika hii mistari michache tu, Yesu alidai kuwa Mwalimu, Bwana, Kristo, Mwana wa Mungu, na Mwana wa Adamu.

 

            Lazima tushike mafundisho ya Yesu. Aliwaambia hivi wale Wayahudi waliokuwa wamemwamini, “Mkishika mafundisho yangu, kweli ninyi ni wanafunzi Wangu. Halafu, mtaifahamu kweli, na kweli hiyo itawaweka huru” (Yohana 8:31-32, TLR). Mara nyingi mstari wa 32 husemwa, lakini ni sharti linalotegemea mstari wa 31 kufanyika. Ili kuwa mwanafunzi wa Bwana Yesu lazima tuvumilie na kutii – tushike mafundisho Yake. Wanafunzi wa Yesu tu ndiyo watakao-okolewa.

 

            Lazima tulishike Neno la Yesu. Yesu alisema hivi, “Nawaambia kweli kwamba, kama mtu yeyote atalishika neno langu, hataona kifo kamwe” (Yohana 8:51, TLR). Neno “kulishika” ni mchanganyiko wa kuvumilia, kujua na kuthamini, na kutii neno la Yesu.

 

            Lazima tumkubali Yesu na maneno Yake. Yesu alisema, “Yupo hakimu kwa yule mwenye kunikataa na asiyekubali maneno yangu. Neno lile lile nililosema litamhukumu siku ya mwisho” (Yohana 12:48).

 

            Lazima tuje kwa Baba kwa njia ya Yesu, tena, Yeye tu. Yesu alisema, “Mimi ndiye njia na kweli na uzima. Hakuna mtu anayekuja kwa Baba bila kupitia kwangu. Kama kweli mngenijua, mngemjua na Baba yangu vile vile. Kuanzia sasa, mnamjua, na mmemwona” (Yohana 14:6-7, TLR).

 

            Ni lazima tumpende Yesu na kuyatii mafundisho Yake. Yesu alisema, “Mtu yeyote akinipenda, atatii mafundisho yangu. Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kufanya makao pamoja naye. Yeye asiyenipenda hatatii mafundisho yangu” (Yohana 14:23-24, TLR). Tunaambiwa katika Waebrania 5:9 kwamba Yesu alifanyika asili ya wokovu wa milele kwa wale wote wenye kumtii. Ni muhimu kwamba tumpende Yesu na kumtii, kama tunataka wokovu.

 

            Ni lazima tudumu katika mzabibu na kuzaa matunda sana. Yesu alisema, “Mimi ndiyo mzabibu, ninyi ni matawi. Kama mtu akikaa ndani yangu nami ndani yake, atazaa matunda mengi, na bila mimi ninyi hamwezi kufanya lolote. Mtu asipokaa ndani yangu, yeye ni kama tawi linalotupwa na kunyauka. Matawi kama hayo huokotwa na kutupwa motoni, na kuchomwa” (Yohana 15:5-8, TLR).

 

            Ni lazima tubakie na ladha yetu kama chumvi. Yesu alisema, “Ninyi ni chumvi ya dunia. Lakini, kama chumvi ikipoteza ladha yake, inawezaje kufanywa kuwa chumvi tena? Haifai tena kwa lolote isipokuwa kutupwa nje na kukanyagwa na watu” (Mathayo 5:13, TLR). Andiko hilo linaonekana kama lenye kusema kwamba, ile ladha ikiisha potea haiwezi tena kurudishwa. Katika Waebrania 6:4-6 tunakuta andiko lenye kufanana na hilo. “Haiwezekani kwa wale waliokuwa wamepewa nuru hapo kwanza, waliokwisha onja zawadi ya mbinguni, waliokwisha shiriki Roho Mtakatifu, waliokwisha onja uzuri wa Neno la Mungu na nguvu za wakati ujao, kurudishwa kwenye toba kama wataanguka, kwa sababu, kwa hasara yao, wanamsulubisha Mwana wa Mungu tena, na kumwaibisha mbele ya watu” (TLR).

Hizo amri zinahusiana na mwenendo na zinakubaliana na Maandiko mengi sana yenye kusema kwamba tutahukumiwa kulingana na tulichofanya – yaani, mwenendo wetu. Lakini Maandiko pia yanasema tunaokolewa kwa imani. Maneno hayo yanayo-onekana kama yanapingana yanakubaliana kwa sababu, utii hutokana na imani. Ona Warumi 1:5. Imani husababisha utii ambao unaamuru mwenendo wetu. Kutii amri za Yesu ni sawa na kufanya mapenzi ya Baba yetu wa mbinguni. Tusipotenda mapenzi ya Mungu, hatuwezi kuingia katika ufalme wa mbinguni. Ona Mathayo 7:21.

 

Ili tusiwe na hatia ya kudanganya, lazima tuwafundishe wanaotafuta na waongofu wapya masharti husika – sehemu za imani yenye kuokoa – ambayo lazima yatimizwe ili wokovu upatikane.

 

Je, kweli ni lazima kueleza kila sharti? Kulingana na Yesu, tunapaswa kuhesabu gharama kabla ya kuanza. Sehemu hizo zote zilizotajwa hapo juu ni za imani yenye kuokoa. Lakini je, kuna kiasi kidogo kinachotakiwa kumwambia mtu anayetafuta ili kuepukana na hatia ya kudanganya? Nadhani kipo.

 

Kuna kweli mbili ambazo hazina mjadala, ambazo lazima zikubaliwe na yeyote anayetaka kuokoka. Kwanza – Yesu ni lazima awe Bwana wa wote wanaotaka kuokoka. Na pili – kama Yesu ni Bwana, lazima kumtii. Ni kituko kudai kwamba Yesu ni Bwana na kuacha kumtii.

 

Ili tusiwe na hatia ya kudanganya, ni muhimu pia kuhakikisha kwamba mtafutaji anaelewa kwamba wale wanaomfuata Bwana Yesu lazima waache kila kitu (Luka 14:33). “Gharama” zingine zote zimehusishwa katika hii gharama kubwa. Wale wanaojifunza tangu mwanzo kwamba lazima wampende Yesu kuliko wake zao, watoto na wana-familia wengine, na kwamba lazima wajitwike msalaba wao na kumfuata, hawatashangaa baadaye kwa sababu tayari walijua gharama ya kumfuata Bwana Yesu.

 

Mungu aliongoza safari yangu kuelekea kwenye imani yenye kuokoa kwa njia ambayo  inaonyesha baadhi ya matatizo tunayozungumzia hapa. Baada ya kusoma Biblia kwa miezi kadhaa, nakumbuka kushuka ngazi asubuhi moja nikiamini kwamba Biblia ni kweli. Niliamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zangu, kwamba Yeye ni Mwana wa Mungu, na kweli zingine za msingi kuhusu imani, ambazo sikuwa nimeziamini usiku uliopita. Kanisa likaamini kwamba mimi ni mwongofu mpya, na mimi pia nikaamini hivyo. Ingawa nilibadilisha marafiki zangu tuliokuwa tunafanya mambo nao na kuwa na marafiki wa kanisa, na ingawa niliacha kutumia lugha chafu, maisha yangu hayakubadilishwa kabisa. Nilikuwa nakwenda kanisani nikiwa nimebeba Biblia yangu, badala ya kuisoma.

 

Baada ya miezi michache nikachoka na kujiuliza kama kweli Ukristo ni hayo tu. Neema niliyokuwa nayo mimi ni kwamba Bwana alinivuta nirudie Neno Lake tena. Safari hii, kila mahali nilipotazama niliona neno “Bwana, Bwana” na “tii, tii”. Nikajifunza swala la Yesu kuwa Bwana na haja ya kumtii yeye kwa sababu, kwa kumbukumbu zangu, sikuwahi kusikia mahubiri kuhusu haja ya Yesu kuwa Bwana katika maisha yangu, au kwamba nilihitaji kumtii. Kibaya zaidi, nilipowauliza rafiki zangu wa kanisani kuhusu kumtii Bwana, walisema hatuwezi kumtii kwa sababu tunatenda dhambi mara mia nyingi kila siku.

 

Siku moja nikamwendea Bwana katika maombi na kusema, “Bwana Yesu, kwa kadiri ninavyoona katika Neno Lako, unatakiwa kuwa Bwana katika maisha yangu, nami ninatakiwa kukutii. Kama unataka hivyo, niko tayari kufanya hivyo. Naomba uwe Bwana maishani mwangu, nami nitakutii kiasi niwezavyo katika maisha yangu yote.” Hapo ndipo maisha yangu yalipobadilika. Mara nikawa na upendo, furaha na amani moyoni mwangu ambavyo sikuwahi kuwa navyo. Hata sikujua yaliyonitokea mpaka niliposoma Yohana 14:15-17 na kugundua kwamba ukiri wangu kumwamini Yesu kama Bwana wangu na ahadi yangu kumtii kulimfanya Yesu amwombe Baba anipe Roho Mtakatifu. Nilipokuja kusoma Wagalatia sura ya 5, niligundua kwamba ule upendo, furaha na amani nilivyokuwa nimepata vilikuwa tunda la Roho Mtakatifu.

 

Watafutaji wenye kumpokea Yesu kama Bwana na kuahidi kumtii Yeye kwa moyo wote watazaliwa mara ya pili wakati Baba atakapowapa Roho Mtakatifu (Yohana 14:15-16). Kabla na baada ya uamuzi wao, watafutaji pamoja na waamini wapya wanapaswa kuelekezwa kwenye Injili na mafundisho na amri za Bwana Yesu. Watafutaji watapata ufahamu mkubwa zaidi kuhusu maana ya kumfuata Yesu. Waamini wapya watajifunza jinsi ya kuishi katika ufalme wa Bwana wao (Mathayo 28:20). Ushahidi mmoja wa kuongoka kweli ni kwamba, mtoto aliyezaliwa mara ya pili katika Kristo atatafuta kwa njaa sana maziwa ya Injili, mara nyingi akitumia masaa mengi sana kujifunza Maandiko. Vivyo hivyo, ushahidi wa kudumu katika imani unaonyeshw kwa kuendelea kila siku katika Neno la Mungu ili kupata mkate wa kiroho wa kila siku.

 

Wakati mwamini mpya anaposoma Maandiko sana, atajifunza haraka sana kuhusu masharti kwa ajili ya wale wanaotaka kumfuata Bwana Yesu. Wale ambao wamepokea Yesu kweli kama Bwana wao wanayapokea maagizo yake kwa furaha na kutafuta kuyafuata maishani mwao. Wale ambao walidanganywa kufanya maamuzi kwa ajili ya Kristo wanaweza kuchanganyikiwa na kuondoka watakapojua kwamba kuna masharti mengi ambayo lazima watimize ili wapate wokovu.

 

Tulipokuwa tunatazama swala la ulaghai hapo mwanzoni mwa sura hii, tulisoma takwimu kutoka kitabu cha Ray Comfort kiitwacho The Way Of The Master (Bridge-logos) zilizotuonyesha kwamba watu 19 kati ya 20 walioamua kumfuata Kristo katika madhehebu makubwa walikuwa wanaondoka kwenye imani upesi sana. Je, ulaghai na udanganyifu katika kuhubiri injili kunawea kuwa sababu za wengi kuanguka haraka hivyo? Nadhani ndiyo. Watu wanaojua kweli wana kawaida ya kusimama imara. Majaribu na dhiki vinapokuja, hawashangai wala kuvunjwa moyo.

 

Kuna wanaomhesabu Charles Finney kuwa mwinjilisti mkuu sana wa KiMarekani. Mtindo wake ulikuwa tofauti na wenzake wengi. Alipokuwa anafanya mkutano wa ki-injilisti katika mji, angehubiri kila jioni kwa masaa matatu au zaidi kwa miezi mingi. Alipoanza mkutano, alikuwa hamruhusu mtu yeyote kufanya uamuzi wa kumfuata Kristo mpaka siku ya nne au ya tano. Alitaka wajue gharama kabla ya kujitolea kumfuata Bwana Yesu. Tafiti zilizofanywa baadaye zilionyesha kwamba asilimia 85 hadi 90 ya watu waliofanya uamuzi wa kumfuata Kristo katika mikutano yake, waliendelea katika Bwana. Miji ilibadilishwa. Uhalifu ulipungua sana.

 

Tokea wakati huo, inaonekana kuna hali ya kutokutaka kabisa kumwambia mtafutaji ukweli wa imani, kwa hofu kwamba habari hizo ni ngumu. Badala yake, kujitolea kwa mtu kumeshushwa hadi “sala ya toba” ambayo, watu wanaambiwa “omba nyuma yangu” sala fupi tu rahisi, mara nyingi ni ya kutubu na kuonyesha kwamba wanamkubali Yesu kama Mwokozi wao (si kama Bwana). Halafu mara nyingi wanahakikishiwa kwamba sasa wameokoka.

 

Niliwahi kumsikia mhubiri mmoja anayeitwa Hal Lindsey akihubiri kwenye kipindi cha redio nilipokuwa Seattle. Alikuwa ametoa nafasi ya ombi kama hilo. Baadaye aliwaahidi wale waliokuwa wameomba pamoja naye kwamba, atawaona mbinguni. Hapo, Hal alifanya ulaghai kwa sababu hakuwaongoza watu hao kwa Yesu kama Bwana. Alifanya udanganyifu kwa sababu hakuwaambia kwamba kuna masharti mengi sana ambayo lazima kila mwamini ayatimize kama anataka kwenda mbinguni, na yote ni sehemu ya imani yenye kuokoa.

 

Kiongozi mmoja wa vijana anayeitwa Dave De Roles alisema kwamba, mara nyingi Injili inaelezwa kwa njia ambayo karibu vijana wote watafurahia kupokea mwaliko huo. Anasema, hilo linaleta matatizo sana. Hakuna aina yoyote ya matunda yanayo-onyesha kwamba kweli wamekuwa Wakristo, na inaonekana ni kama wamepewa kinga dhidi ya kupokea ukweli baadaye.

 

Basi, haishangazi kwamba 19 kati ya 20 wameanguka na kuacha imani. Je, tunaogopa kufanya kama Yesu alivyofanya? Tunapaswa kuwa na shauku ya kufanya chochote ambacho Bwana wetu anasema, kwa njia Yake. Tukifanya mambo kama Yeye, tuna uhakika kwamba Yeye atabariki na kuitia nguvu kazi Yake.

 

Mwinjilisti aitwaye Graham Ashby aliandika hivi: “Kama mtu yeyote aliyewahi kufanya huduma mimbarani anavyojua, ‘sisi tunaweza’ kuwafanya watu wafanye chochote tunachotaka – ni udanganyifu mkubwa huo. Badala yake, tungesubiri Mungu aokoe kuliko kulazimisha watu wafanye maamuzi yasiyokomaa. …. Kuhusu matokeo, sote tunajua kinachosemwa na takwimu.”

 

Pengine sasa tunaweza kuelewa vizuri zaidi uhalisi wa mafundisho ya Yesu kuhusu mlango mwembamba. “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba. Maana mlango ni mpana, na njia ni pana, iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache” (Mathayo 7:13-14).

 

Inasikitisha kwamba wachungaji wengi na waalimu waliopewa wajibu wa kuwaongoza wale wanaowafundisha wafikie wokovu wa milele wanawanyima washirika wao ukweli kwa kuwafundisha injili nyingine – injili ya uongo ambayo inapelekea kwenye kuhukumiwa badala ya kuokoka.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sura Ya Tisa

(Chapter 9)

 

Tafuteni Kwanza … Haki Yake

(Seek First … His Righteousness)

 

Katika Mathayo 6:33, Yesu alifanya haki kuwa kipaumbele cha juu sana alipoagiza hivi: “Tafuteni kwanza ufalme Wake na haki Yake, na haya mambo mengine yote mtapewa vile vile.” (TLR)

 

Katika sura hii tutatazama amri ya Yesu ya kutafuta kwanza haki ya Mungu. Hii amri ndiyo inayovunjwa sana na Wapinga Sheria, wafuasi wa itikadi ya usalama wa wokovu milele bila masharti, na utamaduni wa kanisa ninaouita mimi UKanisa.

 

Yesu aliweka haki kuwa sharti mojawapo la wokovu aliposema hivi:

 

“Kwa maana nawaambia hivi: Haki yenu isipozidi ile ya Mafarisayo na waalimu wa Torati, hakika hamtaingia katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 5:20, TLR).

 

Maneno ya mwisho ya sentensi hii yanaifanya haki kuwa sharti la imani yenye kuokoa. Hatutatokoka kama haki yetu haitazidi ile ya Mafarisayo.

 

Wengi hapa watapiga kelele, “Hatuwezi kuwa wenye haki! Haiwezekani kabisa!” Kweli? Hilo wazo linatokea wapi? Yusufu aliitwa mtu mwenye haki (Mathayo 1:19). Simioni aliitwa mwenye haki na mtauwa (Luka 2:25). Kuwa haki ni swala la kuamua kutenda yaliyo haki – ni jambo la nia ya mtu. Mtume Yohana alisema hivi: “Wala amri Zake si mzigo” (1Yohana 5:3, TLR).

 

Inaonekana Mtume Yohana anasema na watu kama hao katika 1Yohana 3:7. “Watoto wapenzi, msiruhusu mtu yeyote awapotoshe. Kila afanyaye yaliyo sawa ni mwenye haki, kama ambavyo Yeye alivyo mwenye haki.” Je, umeona neno “afanyaye”? Hapo tena mkazo uko kwenye mwenendo! Ni lazima tufanye yaliyo sahihi. Hapo tutakuwa wenye haki. Tukifanya yaliyo ya dhambi, sisi tutakuwa waovu.

 

Je, mtu anaweza kufanya yaliyo dhambi na aokoke? Wengi wanasema, “Ndiyo!” Mtume Yohana anakataa. Yeye alifundisha hivi: “Yule afanyaye yaliyo dhambi ni wa Ibilisi” (1Yohana 3:8, TLR). Tena, “Hivi ndivyo tunawajuavyo watoto wa Mungu ni akina nani, na watoto wa Ibilisi ni akina nani: Yeyote asiyefanya yaliyo sawa (yaani, asiyetenda kwa haki) si mtoto wa Mungu” (1Yohana 3:10, TLR). Kinyume na mawazo ya wengi, Yohana alifundisha kwamba wale wasiokuwa wa haki – yaani, wale wafanyao yaliyo ya dhambi (au, wanaotenda uovu) – ni wa Ibilisi. Hao ni watoto wa Ibilisi.

 

Mtume Paulo naye alithibitisha kwamba kuendelea katika dhambi hakuwezekani katika maisha ya waamini wa kweli. “Kila anayelikiri jina la Bwana lazima ageuke na kuacha uovu” (2Timotheo 2:19, TLR). Wakristo wote wa kweli wanaolikiri jina la Bwana lazima wageuke na kuachana na maovu. Hiyo ndiyo maana halisi ya toba – kuungama dhambi yetu na kuiacha, na kumgeukia Mungu. Tusipotubu (ambalo ni sharti lingine tena la imani yenye kuokoa), hatuwezi kuokoka. Tusipoungama dhambi yetu na kugeuka kuiacha, hatutaokoka.

 

Pengine utauliza, “Unachosema ni kwamba kama nitafanya dhambi mimi ni wa Ibilisi?” Unaweza kuwa, lakini sisemi hivyo, wala sidhani mstari unasema hivyo. Neno “afanyaye” ni kitendo kinachoendelea. Basi, ni halali kabisa kusema maneno ya Yohana kwa njia nyingine, hivi: “Yeye aendeleaye kufanya yaliyo dhambi ni wa Ibilisi”. Na hilo linakubaliana na maneno ya Mtume Yohana mahali pengine, kwamba: “Hakuna mtu anayekaa ndani Yake anaye-endelea kufanya dhambi. Hakuna mtu anaye-endelea kufanya dhambi aliyemwona, wala kumjua Yeye” (1Yohana 3:6, TLR). Mtu anaye-endelea kufanya yaliyo sawa ni mwenye haki. Mtu anaye-endelea kufanya dhambi ni mwovu. Yeye ni wa Ibilisi. Hajawahi kumwona Bwana, wala kumjua.

 

Yesu alisimulia mfano unaofuata wenye kufundisha kiwango ambacho kitatumiwa kuwahukumu watu wakati wa hukumu ya mwisho.

 

“Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Ndipo wenye haki watakapong’aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio na asikie” (Mathayo 13:41-43).

 

Hukumu ya mwisho itategemea tu yale ambayo mtu anasababisha au kufanya maovu. Wale wanaotenda maovu watahukumiwa. Watatupwa katika tanuru la moto. Watahukumiwa kulingana na kama walifanya maovu au walikuwa wenye haki – haitategemea walichoamini.

 

Imani yenye kuokoa inadhihirishwa kupitia haki. Imani ya uongo au bandia (au, isiyokuwepo kabisa basi) inadhihirishwa kwa njia ya uovu na mabaya. Katika mfano huu, Yesu alihakikisha kwamba tunaelewa kwamba kuna hukumu ya moto mkali kwa ajili ya wale watendao uovu, lakini baraka katika ufalme Wake kwa wale ambao ni wenye haki.

 

Hebu tutazame baadhi ya mafundisho ya Yesu yenye kulinganisha haki na uovu – kitu kikubwa katika mafundisho ya Yesu. Mara tu baada ya lile sharti la kufanya mapenzi ya Mungu (ktk Mathayo 7:21), Yesu anatuambia juu ya siku ya hukumu, ambapo wengi watamwambia, “ ‘Bwana, Bwana! Hatukutabiri katika jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo na kutenda miujiza mingi?’ Ndipo nitakapowaambia waziwazi, ‘Sikuwajua ninyi kamwe. Ondokeni kwangu, enyi mtendao maovu’!” Kumbuka kwamba wakati huu, neno linalotafsiriwa “watenda maovu” linaweza kutafsiriwa vizuri kwamba ni “wapinga sheria”.

 

Yesu aliwaita watu hawa watenda maovu. Mbinguni ni kwa ajili ya wale watendao mapenzi ya Mungu. Hukumu ni kwa ajili ya wale watendao uovu. Hapa tena ona kwamba Yesu anazungumza juu ya mwenendo – kutenda maovu. Je, umeona kwamba wale watu ambao Yesu alisema ni waovu walijaribu kumshawishi kwamba wao ni wa mbinguni kwa matendo yao – kutabiri kwa jina lake, kutoa pepo, na kufanya miujiza mingi? Somo kubwa hapa ni kwamba kuwa wenye haki – kufanya mapenzi ya Mungu – huharibu kila unachodai kwamba unafanya kwa ajili ya Mungu. Ni lazima kwanza tuwe kama Yesu kabla ya kuhesabiwa haki kwa ajili ya kufanya mambo kwa ajili ya Yesu.

 

Paulo alifundisha hicho hicho katika 1Wakorinto 13:1-3. “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo hainifaidii kitu.” Bwana Yesu aliamuru kwamba tupendane, kama Yeye alivyotupenda sisi. Paulo alifundisha kwamba dhambi ya kutokumpenda Mungu na kutowapenda wengine kiliharibu matendo mema. Hapa tena, kutokutii pamoja na dhambi vitaadhibiwa. Tumeitwa kuwa wenye haki.

 

Yesu alizungumza mara nyingi sana kuhusu kitakachotokea mwishoni wa wakati. Katika Mathayo 13:44, Yesu alisema, “Malaika watakuja na kuwatenganisha waovu na wema, na kuwatupa waovu katika tanuru la moto, ambako kutakuwa na kulia na kusaga meno.” Waliohukumiwa walitajwa kuwa waovu; mwenendo wao ulikuwa mwovu.

 

Katika Mathayo 18:23-31, Yesu alisimulia hadithi ya mtumishi aliyesamehewa fungu kubwa sana na mfalme, lakini ambaye baadaye alisababisha mtumishi mwenzake kutupwa gerezani kwa kushindwa kumlipa yeye kiasi kidogo sana cha fedha. Yesu alisema, yule mtumishi aliyesamehewa alikuwa mwovu. Wakati mfalme aliposikia juu ya yeye kutomsamehe mwenzake, alirudisha den lake na kumkabidhi kwa askari magereza ili ateswe mpaka alipe kila kitu alichodaiwa. Katika mstari wa 35, Yesu alisisitiza kwamba sisi pia tutahesabiwa waovu kama hatutawasamehe wengine. “Hivyo ndivyo Baba yangu wa mbinguni atakavyowatendea kila mmoja wenu, msipowasamehe ndugu zenu kutoka moyoni.” Hapa tena, swala ni hukumu kwa sababu ya mwenendo mbaya – kukataa kusamehe.

 

Hebu turejee kwenye ile hadithi ya mtumishi mwaminifu na mwenye hekima, na yule asiyekuwa mwaminifu. Wote walikuwa watumishi wa Bwana. Wa kwanza anasifiwa kwa sababu ya uaminifu wake. Ila, Yesu anamwita yule mtumishi ambaye hakudumu katika uaminifu kuwa ni mwovu. Yesu alisema, bwana wa mtumishi huyo “atamkata vipande viwili na kumpangia mahali pamoja na wanafiki, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno” (Mathayo 24:51, TLR). Mtumishi mwovu alishindwa kufanya alichotakiwa kufanya, kisha akawa mwovu – akaanza kuwapiga watumishi wenzake na kula na kunywa na walevi. Mwenendo wake mwovu ukasababisha ahukumiwe.

 

Pia tulitazama hapo nyuma mfano wa talanta ambapo watumishi watatu walipewa talanta za kusimamia, wakati bwana akiwa hayupo. Wawili walifanya vizuri kwa kuzidisha kiasi walichokuwa wamepewa, lakini yule wa tatu alificha talanta yake, kisha akairudisha kama ilivyo kwa bwana wake. Watumishi wale wawili wa kwanza walitajwa kuwa “wema na waaminifu”. Bwana alimwambia yule aliyeficha talanta yake, “Wewe mtumishi mwovu, mvivu!” Je, bwana alitoa amri gani kuhusu mtumishi huyu? Aliamuru hivi: “Mtupeni huyo mtumishi asiyefaa nje katika giza, mahali ambapo kutakuwepo kilio na kusaga meno”. Ona mfano mzima katika Mathayo 25:14-30. Fundisho linalofanana na hili linapatikana katika ule mfano mwingine wa aina hiyo katika Luka 19:12-27.

 

Katika mafundisho haya, Yesu anasema kuhusu mwenendo! Aliwasema watu katika kila mfano kwamba ni waovu kwa sababu hawakufanya yaliyoagizwa na bwana. Wote walihukumiwa kwenda jehanamu – kwenda gizani, mahali ambapo kutakuwepo kilio na kusaga meno.

 

Watu waliosifiwa ni wale waliotenda walichotakiwa kufanya. Waovu na wale waliosifiwa walihukumiwa kwa msingi wa walichotenda.

 

Marekani na mataifa ya Magharibi yanasemekana kuwa ni mataifa ya Kikristo yaliyopita. Badala ya Ukristo kuwa sehemu muhimu ya maisha ya kitaifa, kuna upinzani au chuki ya wazi kabisa dhidi ya imani. Yesu alitabiri juu ya wakati kama huu, hivi:

 

“Wakati huo wengi wataiacha imani na kusalitiana na kuchukiana, na manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya watu wengi sana. Kwa sababu ya kuongezeka kwa maovu, upendo wa walio wengi utapoa, lakini, yeye atakayesimama imara mpaka mwisho ataokoka” (ktk Mathayo 24:10-13, TLR).

 

Tunaona wengi wakiondoka kwenye imani ya Kikristo. Manabii wengi wa uongo wametokea ili kuwadanganya watu wengi sana. Wapinga Sheria na wale wenye kuamini kuhusu usalama wa wokovu milele bila masharti yoyote ni miongoni mwa wanaowadanganya wengi sana. Kwa nini upendo wa walio wengi unapoa? Kwa sababu ya kuongezeka kwa maovu – mambo ambayo ni kinyume cha haki.

 

Bwana Yesu alilaumu uovu na maasi kila mara, pamoja na wale waliokuwa watenda maovu na wafanya mabaya. Inanishangaza mimi sana kwamba wengi wanaodai kuwa Wakristo wanaendelea kutangaza kwamba tabia mbaya na uovu haviathiri wokovu, kwamba, cha maana ni kitu mtu anachoamini tu. Kwa hali hiyo, haishangazi kwamba Yesu aliuliza, “Je, Mwana wa Adamu atakaporudi, atakuta imani duniani?” (Luka 18:8, TLR).

 

Bila shaka unaona wazi jinsi wapinga Sheria watakavyokipata wakati wa hukumu. Dai lao kwamba ukiamini sawa ndicho cha maana tu, na kwamba mwenendo hauathiri wokovu, ni uongo kabisa.

 

Mafundisho yao ya uongo yanasababisha hukumu tu na kupotea kwa wale wanaoendelea katika dhambi, wakiamini kwamba wanao wokovu kwa kuwa tu wameamini kitu sahihi. Lakini, mpinga sheria haamini kilicho sahihi. Anachoamini kimepotoka vibaya sana kwa sababu kinaruhusu na kuendelea maisha katika dhambi na kuachilia nafsi ifanye ipendacho, kitu kinachohakikisha laana na hukumu kwa wote wanaoishi hivyo. Ingawa huyo mpinga sheria anadai ameokoka – kwa uongo lakini – mtume Yohana anasema watu kama hao hawamjui Mungu wala hawajahi kumjua.

 

Imani ya wapinga sheria imeenea sana. Pamoja na imani juu ya usalama wa wokovu milele bila masharti, yawezekana hizo mbili ndizo zilizoenea sana sana katika kanisa la siku hizi la nchi za Magharibi. Takwimu za talaka katika Marekani zinathibitisha jambo hili. Katika sura iliyotangulia tuliona kwamba Yesu aliruhusu talaka wakati tu mwenzi mmoja katika ndoa anapokuwa mwasherati.

 

Kundi la Utafiti la Barna liligundua kwamba wanaodai kuwa Wakristo walikuwa na viwango vya juu kidogo vya talaka kuliko watu wa kawaida, ambao ni pamoja na wasemao kwamba hakuna Mungu na wenye mashaka juu ya Mungu. Ukitazama takwimu hizo kwa ukaribu zaidi, utaona mambo ya kushangaza zaidi. Asilimia 27 ya wale wanaojiita “Wakristo waliozaliwa mara ya pili” wameachana na wenzao zamani au hivi karibuni, ukilinganisha na asilimia 24 ya watu wa kawaida. Lakini katika makanisa ya KiBatisti na ya KiProtestanti yaliyo huru ambayo ndiyo mengi katika ukanda uitwao “Wa Biblia” huko Marekani, asilimia 29 ya WaBatisti na 35 ya hao wengine, wameachana na wenzao, ambacho ni kiwango cha juu kuliko cha dhehebu lingine lolote la Kikristo.

 

Hapa, si kwamba kanisa limekuwa kama dunia. Kanisa limeizidi dunia kwa ubaya. Dunia ya wasioamini haina vizuizi vyovyote vya kidini kuhusu talaka. Lakini, Wakristo, ambao wameamriwa na Bwana Yesu wasiachane, wanafanya hivyo kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko wale ambao hawana vizuizi. Dhehebu la KiBatisti, lenye kiwango cha juu cha talaka kwa asilimia tano kuliko watu wa kawaida, linakubaliana na itikadi ile ya uongo ya usalama wa wokovu milele bila masharti – au, mtoto wa Wapinga Sheria – kama alivyofafanua Charles Stanley.

 

Tumerudia mara kwa mara mafundisho ya Yesu katika Mathayo 7:21 yasemayo kwamba wale tu “wafanyao” mapenzi ya Mungu ndiyo watakaoingia katika ufalme wa m binguni na kwamba, mafundisho na amri za Yesu ni mapenzi ya Mungu. Tumeona katika sura zilizopita kwamba masharti mengi ambayo ni sehemu ya imani yenye kuokoa yanapatikana katika mafundisho na amri za Yesu. Tunapokuwa watiifu kwa mafundisho na amri za Yesu tunatimiza masharti ya Mungu ya imani yenye kuokoa na kutosheleza matakwa ya wokovu kwamba tufanye mapenzi ya Mungu. Kutii amri za Yesu hufanya zaidi. Wale wanaotii amri Zake wanamwonyesha Yesu kwamba wanampenda. Basi, wao nao hupendwa na Baba pamoja na Bwana Yesu (Yohana 14:21, 23). Yesu alisema, “Mkitii amri zangu, mtakaa katika pendo langu, kama mimi nilivyotii amri za Baba yangu na kukaa katika pendo Lake” (Yohana 15:10, TLR). Tena Yesu aliwaambia wanafunzi Wake kwamba, “Ninyi ni rafiki Zangu mkifanya ninayoamuru” (Yohana 15:14, TLR). Tuliona hapo nyuma kwamba kumpokea Roho Mtakatifu hutegemeana na kujitolea kwa mtu kumtii Bwana Yesu (ona Yohana 14:15-17 na Matendo 5:32). Mwisho, wokovu wenyewe ni kwa ajili ya wale wanaomtii Yesu, kama ifuatavyo: “Yeye [Yesu] alifanyika asili ya wokovu wa milele kwa ajili ya wote wanaomtii” (Waebrania 5:9, TLR).

Ukitaka maelezo zaidi kuhusu mada ya haki, ona makala niliyoandika katika tovuti hii: www.bereanpublishers.com | tafuta “Salvation Issues” | halafu tafuta “Must Christians Be Righteous?”

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sura Ya Kumi

(Sura Ya 10)

 

Maneno Yaliyozoeleka, Yanayosemwa Kupinga Haki

(Popular Anti-Righteousness Expressions)

 

Hatuko Chini Ya Sheria …

 

Kwa kuwa wito wa kuwa wenye haki umeenea sana katika mafundisho ya Kristo, kuna jitihada nyingi sana kutoka kwa wenye kueneza itikadi za uongo kufanya batili amri za Yesu. Mara nyingi wanamkariri Paulo, aliposema hivi: “hatuko chini ya Sheria. Tuko chini ya neema!” (Warumi 6:14-15, TLR). Sheria ambayo Paulo alikuwa anaisema hapo ni Torati la Agano la Kale – ile ambayo Wayahudi walipewa na Musa. Tunajua ni ile Torati ya Musa kutokana na mabishano yaliyozuka huko Galatia, mahali ambapo waamini wa Kiyahudi waliotaka kudumu katika dini yao walijaribu kuwalazimisha Wakristo wWagalatia kushika sheria na maagizo ya Agano la Kale, kama vile tohara (ona Wagalatia 2:4-5). Paulo alimkabili Petro akisema, “Wewe ni Myahudi, lakini unaishi kama Asiyekuwa Myahudi. Inakuwaje basi uwalazimishe Wasiokuwa Wayahudi wafuate desturi za Kiyahudi?” (ktk Wagalatia 2:14, TLR).

 

Paulo mwenyewe alisema yuko chini ya sheria. “Mimi siko huru kutokana na sheria ya Mungu bali niko chini ya sheria ya Kristo” (1Wakor. 9:21, TLR. Ona pia Wagalatia 6:2). Kwa kuilinganisha sheria ya Mungu na sheria ya Kristo, Paulo alitambua kwamba mafundisho na amri za Yesu – yaani sheria ya Kristo – vilitoka kwa Mungu. Paulo akafundisha kwamba waamini lazima waitii Injili ya Bwana Yesu (ktk 2Wathes. 1:8-10).

 

Haki Ya Kuhesabiwa

 

Juhudi nyingine ya kupotosha mafundisho na amri za Yesu ni kudai kwamba haki pekee ambayo waamini wanaihitaji ni ile ya kuhesabiwa, iliyo kamili, ya Yesu. Wanasema kwamba, wakiamini ipasavyo, Mungu ataona ndani yao ile haki kamilifu ya Yesu, bila ya kujali mwenendo wao ambao unaweza kuwa mwovu. Wanasimama kwenye Maandiko kama hili: “Basi mwaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria” (ktk Warumi 3:28). Hapa tena wanategemea maneno au tamko linalosema juu ya Torati ya Agano la Kale, si Sheria ya Kristo ambayo imekusanya pamoja mafundisho Yake na amri Zake. Wanadai kwamba Mungu huangalia haki ya Yesu tu na kuwahesabia haki Yake iliyo kamili wale wanaomwamini.

 

Ingawa Paulo alitamka kwamba mtu huhesabiwa haki bila ya kushika au kufuata sheria, Paulo ndiye aliyetuambia juu ya tamko la utume wake katika Warumi 1:5, kama ifuatavyo: “Ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili kuwaita wote Wasiokuwa Wayahudi wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake.” Kulingana na Paulo, utume wake wa msingi haukuwa kuwafundisha watu kitu cha kuamini, bali kuwaita watu kutii kutokana na imani. Kumtii nani? Bwana Yesu. Tunapaswa kutii nini? Kila kitu ambacho Bwana Yesu alikisema katika mafundisho Yake na amri Zake. Basi si ajabu sana kwamba wale wapinga sheria wanathubutu kudai kwamba alichosema Paulo kuwa ni kazi yake maishani, ambayo kwa ajili hiyo alipokea neema na utume, haiwahusu wao?

 

Tumekwisha ona mwenendo ukitajwa sana tangu mwanzo wa kitabu hiki. Karibu mafundisho yote ya Yesu na amri Zake ni kuhusu mwenendo wetu, lakini mwenendo wetu usingekuwa na faida yoyote kama Mungu hataki kitu cha zaidi kwetu isipokuwa haki kamilifu ya Kristo ihesabiwe kwetu.

 

Yohana alifafanua haki aliposema hivi: “Atendaye haki yuna  haki, kama Yeye alivyo na haki. Atendaye dhambi ni wa Ibilisi …” (1Yohana 3:7). Yohana anaturudisha kwenye mwenendo tena, sio kwenye haki ya kuhesabiwa. Vile vile alisema, “Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua Yeye, ikiwa tunashika amri Zake. Yeye asemaye, ‘Nimemjua’ wala hazishiki amri Zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake” (1Yohana 2:3-4). Yohana anasemaje kwa habari ya madai ya wapinga sheria na wengine wenye kueneza hii injili ya uongo kwamba mwenendo si kitu? Anasema wao ni wa Ibilisi, kwamba ni  waongo na kwamba kweli haimo ndani yao. (Ona 1Yohana 2:4 na 3:10).

 

Upendo Wa Mungu Usio Na Masharti

 

Maneno mengine ambayo yamejulikana na kupendwa sana ni “upendo wa Mungu usio na masharti.” Hii nayo ni sehemu ya mafundisho na itikadi kwamba wokovu wa mtu pia hauna masharti yoyote. Fundisho la uongo kwamba “ukisha okoka, umeokoka milele” linafafanuliwa na madai ya Charles Stanley kwamba, mtu kama aliwahi kupata hata dakika moja tu ya imani, basi ameokoka bila masharti yoyote. Tamko la kuunga mkono madai hayo ya uongo ni uongo mwingine kwamba, upendo wa Mungu hauna masharti.

 

Upendo wa Mungu una masharti. Mafundisho ya Maandiko tangu Mwanzo hadi Ufunuo yanadhihirisha upendo wa Mungu wenye masharti. Tutazame kwanza Yohana 14:21 na 23-24 kama mifano ya upendo wa Mungu wenye masharti.

 

“Yeye aliye na amri zangu na kuzishika, yeye ndiye anipendaye, naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake” (Yohana 14:21).

 

“Yesu akajibu akamwambia, ‘Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kufanya makao kwake. Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka” (Yohana 14:23-24).

 

Katika mstari wa 21 hapo juu, Yesu alieleza kwanza kuhusu mtu yule ampendaye kwamba ni yeye mwenye amri Zake, na anayezitii. Kisha anatamka kwamba Yeye na Baba Yake watawapenda wale wampendao Yeye. Hilo ndilo sharti. Katika mstari wa 23, Yesu anasema kwamba Baba Yake atampenda mtu yule anayempenda Yeye (mtu anayetii mafundisho Yake). Sharti la kupendwa na Mungu ni kwamba mtu ampende Yesu na kuonyesha hilo kwa kutii mafundisho Yake. Katika mstari wa 24, Yesu anatangaza kwamba wale wasiompenda hawatatii mafundisho Yake. Halafu anatuhakikishia kwamba maneno hayo si yake mwenyewe, bali ni ya Baba aliyemtuma. Katika mistari hii, upendo wa Baba (na wa Yesu pia) sharti lake ni mtu kumpenda Yesu na kuyatii mafundisho Yake na amri Zake.

 

Bila hata kutazama Maandiko mengine, tayari tunaona kwamba wale wapinga sheria, wanaoshikilia usalama wa wokovu milele bila masharti na wengine wote wanaodai kwamba mwenendo si kitu cha maana katika wokovu, ni watu wasiompenda Bwana Yesu. Tunajuaje hili? Kwa sababu hataki kutii amri Zake, na hawatazitii kamwe. Wanatangaza kwamba wao wako chini ya neema, si chini ya sheria. Bila shaka unasikia kelele za upinzani hapa. “Wewe! Unasemaje? Simpendi Bwana mimi?” Kumpenda Mungu kunafafanuliwa katika Maandiko, kama ifuatavyo: “Huku ndiko kumpenda Mungu: Kuziti amri Zake” (ktk 1Yohana 5:3, TLR). Bwana Yesu alisema vivyo hivyo katika Yohana 14:15, kwamba, “Mkinipenda, mtazitii amri zangu” (TLR). Kulingana na maelezo katika Maandiko, watu kama hao hawampendi Bwana Yesu. Wamemwasi Yeye. Wameunda fundisho la uongo lenye kudai kwamba hawana haja ya kumtii Bwana Yesu, lakini bado wataokolewa tu.

 

Nini kinachotokea kwa wale wasiompenda Bwana na wasiomtii? Angalia tafsiri hii “hai” ya Yohana 3:36.

 

                        “Yeyote amwaminiye Mwana wa Mungu ana uzima wa milele.

                        Yeyote asiyemtii Mwana hataona uzima wa milele bali anabakia chini ya

hukumu ya Mungu ya hasira kali.”

 

Tafsiri zingine zinasema hivi: “… Yeye asiyemtii Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu iko juu yake.” “… hasira ya Mungu inabaki juu yake.” Sasa, huo upendo wa Mungu ambao hauna masharti uko wapi hapa? Hakuna. Kwa wasiomtii Mwana, hasira ya Mungu inabakia juu yao. Ona Waefeso 2:3.

 

Hii mistari ni muhimu sana katika kufunua wazi uongo kamili wa madai ya wapinga Sheria. Wapinga Sheria wanadai kumwamini Mwana wa Mungu na wanasema, kwa sababu wanamwamini, wanao uzima wa milele. Lakini pia wanadai kwamba hawana haja ya kumtii Bwana Yesu kwa sababu hawako chini ya sheria yoyote ile, wakikiri wazi kwamba wao hawafuati sheria yoyote.

 

Zile tafsiri tulizotaja hapo juu zinakubaliana zote kwamba “yeyote asiyemtii Mwana hataona uzima wa milele.” Pengine njia ifaayo ya kuunganisha “kuamini na kupata uzima wa milele” pamoja na “kutotii na kubakia chini ya hasira ya Mungu” ni rahisi sana. Wale wanaoamini watatii. Wale wanaodai kwamba wanaamini lakini hawatii, ni kwamba hawaamini kulingana na tafsiri ya Biblia – ambayo ndiyo muhimu kwa Mungu. Sisi tunajua kwamba hawana imani yenye kuokoa kwa sababu utii hutokana na imani yenye kuokoa. Hata mapepo wanaamini kwamba kuna Mungu (Yakobo 2:19). Imani pasipo matendo imekufa (Yakobo 2:26).

 

Hebu tutazame tafsiri za Biblia na kuzilinganisha na tafsiri za kidunia kutoka kwenye kamusi. Biblia ni kitabu pekee, kilichokamilika na kujitosheleza kabisa. Wakati wanasheria wanapochunguza mkataba, lazima watazame “katika pembe nne za maandishi husika” – ambao ni usemi unaotumiwa sana katika jamii ya sheria. Wanatafuta maana za maneno na maelezo ya vipengele katika mkataba wenyewe. Kama hakuna ushahidi wa maana iliyokusudiwa ya wahusika wote katika mkataba huo, ndipo wanaporuhusiwa kutafuta maana katika sehemu zingine. Kanuni hii hii ni sawa kwa ajili ya Biblia kwa sababu tafsiri zinazotumiwa katika Maandiko si lazima zilingane na tafsiri tutakazopata katika kamusi. Kwa mfano: Wengi wetu tunaelewa kidogo “kupenda” mtu mwingine ni kitu gani, japo yawezekana tafsiri zetu zikatofautiana.  Lakini, kumpenda Mungu ni kitu gani? Je, unaweza kuchukua maana yako ya upendo na kuihusisha na kumpenda Mungu? Kama ndivyo, bila shaka ungekosea kabisa. Maandiko yanatuambia kwamba: “Huku ndiko kumpenda Mungu: Kuzitii amri Zake” (1Yohana 5:3, TLR). Si ajabu hakuna tafsiri yetu hata moja ya kumpenda Mungu ambayo ingefanana na tafsiri ya Biblia. Ndiyo sababu Yesu aliweza kusema, “Kama mnanipenda, mtanitii” (ktk Yohana 14:15, TLR). Yeye alijua kwamba wale wanaomtii ndiyo wanaompenda. Kwa kuyahusisha maelezo ya kumpenda Mungu na Yeye Mwenyewe, Yesu alijitangaza kuwa Mungu.

 

Mambo ni hivyo hivyo kuhusu maana ya “kuamini” na “imani”. Maana ya maneno haya katika Maandiko si kukubali kitu kwa akili – yaani, kuamini tu kwamba kitu ni kweli. Badala yake katika Warumi 1:5 tulijifunza kwamba utii hutokana na imani. Yale masharti tuliyoona mapema, ambayo bila hayo hatuwezi kuokoka, ni maagizo na viwango vya haki kutoka kwa Mungu ambavyo sisi tulipewa na Yesu katika mafundisho na maagizo Yake, na tunapaswa kuyatii yote. Kwa kuwa tunaokolewa kwa neema kwa njia ya imani, nayo si yetu wenyewe bali ni zawadi kutoka kwa Mungu, wala si kwa matendo, mtu yeyote asije kujivuna (ktk Waefeso 2:8-9), tunajua kwamba tunapopata andiko linalosema lazima tutimize sharti fulani ili tuokolewe, sharti hilo bila shaka ni sehemu ya imani! Kweli, imani ina sura mbalimbali – imeundwa na mambo mengi mbalimbali. Maelezo yasiyokuwa ya KiBiblia hayawezi hata kujaribu kuifafanua.

 

Upendo wa Mungu una masharti. Kwa maelezo zaidi, tazama katika tovuti iitwayo www.bereanpublishers.com |tafuta “False Doctrines” | halafu tafuta “Is God’s Love Unconditional?”

 

Mimi Ni Mwenye Dhambi Tu Aliyeokolewa Kwa Neema

 

Mchungaji anaweza kuwaambia washirika wake, “Mimi ni kama ninyi tu. Ni Mwenye dhambi aliyeokolewa kwa neema.” Mwenye dhambi ni mtu atendaye dhambi. Pengine hapo mchungaji anatafuta kitu cha kuwaunganisha yeye na washirika wake. Je, kuna ukweli wa KiBiblia katika maneno hayo? Hakuna hata tone. Katika Agano Jipya lote, hakuna mahali hata pamoja tu ambapo mfuasi wa kweli wa Yesu anaitwa mwenye dhambi. Wala hakuna mfano wa aina yoyote wa mtu ambaye ni mwenye dhambi “aliyeokolewa”. Wafuasi wa Yesu hawatakuwa wenye dhambi; hawataendelea katika dhambi. Hiyo haimaanishi kwamba hawatafanya dhambi kamwe. Unakumbuka maneno ya Mtume Yohana kuhusu kuendelea katika dhambi? Alisema hivi: “Hakuna mtu anayekaa ndani Yake anaye-endelea kutenda dhambi. Hakuna mtu anaye-endelea katika dhambi aliyemwona, wala kumjua” (ktk 1Yohana 3:6, TLR).

 

Mtu anapofikia mahali pa imani katika Bwana Yesu, ni kiumbe kipya huyo. Tangu wakati huo anaitwa ndugu, mtakatifu, mtumishi, mtumwa, mtumishi wa upendo na wa hiari, mtumwa wa upendo na wa hiari, na kadhalika. Kamwe haitwi mwenye dhambi.

 

Lakini, bila shaka utaelewa jinsi maneno hayo yanavyokuwa faraja kwa mpinga sheria anayefikiri kwamba anaweza kutenda dhambi kwa uhuru kabisa kwa sababu ya kuamini kwake kwamba wokovu hauhusiani na mwenendo hata kidogo. Yeye anajua kwamba ni mwenye dhambi. Kwake, neema ya Mungu ndiyo mambo yote. Kweli, Tozer alisema kitu sahihi kabisa, kwamba, “Fundisho la Kupinga Sheria ni itikadi ya neema ikichukuliwa na hoja zisizo sahihi mpaka kufikia upuzi. Linachukua fundisho la kuhesabiwa haki kwa imani na kulipotosha kabisa.”

 

Ukitaka kujua zaidi swala la waamini kutokuwa wenye dhambi, tazama tovuti ya www.bereanpublishers.com |tafuta “Important Issues”| halafu tafuta “Are Christians Sinners or Saints”

 

Mungu Anampenda Mwenye Dhambi, Lakini Anaichukia Dhambi Yake.

 

Tamko lingine ambalo limetokea katika itikadi ya Wapinga Sheria kanisani ni kwamba, “Mungu anampenda mwenye dhambi, lakini anachukia dhambi yake.” Ni muhimu sana kwa Mpinga Sheria na wafuasi wa fundisho la usalama wa wokovu milele bila masharti kwamba, Mungu ampende mwenye dhambi. Wao wanaamini kwamba ni wenye dhambi, na kwamba hakuna juhudi zozote zinazotakiwa ili kuwa huru na dhambi hizo kwa sababu wamekwisha amua kimakosa kwamba mwenendo (yaani dhambi) si muhimu kwao, kama watapata wokovu au hawatapata. Mwenye dhambi ni mtu anaye-endelea katika dhambi.

 

Je, Mungu anampenda mwenye dhambi? Hebu tuone Maandiko yanasema nini. Katika Zaburi 5:4-6, Daudi aliandika hivi: “Maana wewe si Mungu apendezwaye na ubaya; mtu mwovu hatakaa kwako. Wajivunao hawatasimama mbele za macho Yako; unawachukia wote watendao ubatili. Utawaharibu wasemao uongo; BWANA humzira mwuaji na mwenye hila.” Andiko hili linasema wazi kabisa kwamba Mungu huwachukia wote wanaofanya maovu, na kwamba watu waovu hawawezi kukaa Naye. Katika Zaburi 11:5 Daudi aliandika hivi: “Bwana humjaribu mwenye haki; bali nafsi yake humchukia asiye haki na mwenye kupenda udhalimu.” Hosea aliandika hivi, “Kwa sababu ya maovu yao yote pale Gilgali, niliwachukia hapo. Kwa sababu ya matendo yao ya dhambi, nitawafukuza watoke katika nyumba yangu” (Hosea 9:15, TLR. Ona vile vile Yeremia 12:8).

 

Kwa mantiki hiyo, inakuwa rahisi sasa kuelewa Yohana 3:36, mahali ambapo Yesu alisema hasira ya Mungu inabaki juu ya wale wasiomtii Mwana. Mungu anawachukia walio waovu – wale wasiotii mafundisho na amri za Yesu. Je, hao wachungaji na waalimu wanaokataa kutii amri ya Yesu ya “kuwafundisha kuyatii yote niliyowaamuru ninyi” (ktk Mathayo 28:20, TLR) ni waovu?

 

Dhambi Zinazotazamiwa Na Zilizopita Zimesamehewa.

 

Usemi mwingine unaotumiwa na wapinga sheria na wanaofuata itikadi ya usalama wa wokovu milele bila masharti ni huu: “Unapotubu dhambi zako, dhambi zote zitakazotokea pamoja na zilizopita, zinakuwa zimesamehewa.” Je, umeona jinsi neno la Mungu linavyobatilisha mafundisho ya uongo kwa kusema ukweli kabla ya wakati? Kwa sababu Biblia ni ujumbe mmoja uliounganika na wenye kukubaliana kutoka kwa Mungu, Biblia nzima inaweza kutumika kujifafanua yenyewe. Kwa habari ya dhambi zitakazotokea kusamehewa, Mungu alisema juu ya jambo hili wakati Petro alipoandika hivi: “Lakini, mtu yeyote asipokuwa na hayo, haoni mbali na ni kipofu, naye amesahau kwamba alisafishwa kutokana na dhambi zake za zamani” (2Petro 1:9, TLR). Ndiyo. Tunapotubu, tunasafishwa kutokana na dhambi zetu za zamani, yaani, zile ambazo ndiyo tumezitubia.

 

Uthibitisho zaidi unaweza kuonekana katika barua za Bwana Yesu kwa yale makanisa saba ya Ufunuo. Yesu alisema hivi kwa kanisa la Efeso, “Kumbuka umeanguka kutoka kimo gani! Tubu na kufanya yale mambo uliyofanya mwanzoni. Usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa mahali pake” (Ufunuo 2:5, TLR). Hili linaloandikiwa hivyo na Yesu ni kanisa. Kama dhambi zote zinazotarajiwa zilikuwa zimesamehewa, kwa nini Yesu aliagize kanisa kutubu?

 

Kwa kanisa la Pergamo, Yesu alizungumzia wale waliokuwa wanatetea na kuunga mkono uasherati, na wale “wanaoshika mafundisho ya WaNikolai. Basi, tubuni! La sivyo, nitakuja kwenu hivi karibuni na kupigana kinyume na hao kwa upanga wa kinywa changu” (Ufunuo 2:15-16, TLR). Watubu nini kama dhambi zao za wakati ujao zilikwisha samehewa? Wanahitaji kutubu kwa sababu dhambi zao tarajiwa bado hazijasamehewa. Tunahitaji kutubu upesi sana, mara tu tunapogundua kwamba tumetenda dhambi. Ndipo tutakaporejezwa kuwa watakatifu mbele za Mungu – tusio na mawaa, na bila lawama (Wakolosai 1:22).

 

Kama mfano wa mwisho, hebu tutazame maneno ambayo Yesu alisema kwa kanisa la Thiatira.

 

“Lakini nina neno juu  yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. Tazama, nitamtupa juu ya kitanda na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake; nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake” (Ufunuo 2:20-23)

 

Katika Maandiko haya, Yesu anamtaka Yezebeli na wale wazinio pamoja naye watubu. Anaweka wazi kabisa kwamba atawaadhibu wale watakaoendelea katika dhambi, na kumlipa kila mmoja kulingana na matendo yake. Hakuna hata moja hapo ambalo lingekuwa kweli kama toba ingekuwa inahusiana na dhambi tarajiwa. Wito wa toba anaotoa Yesu unathibitisha kwamba mtu anaweza kutubia dhambi za zamani tu – hawezi kutubu dhambi tarajiwa.

 

Bila shaka dai hili la uongo linaweza kutokana na kutokuelewa toba ni kitu gani. Si kujisikia vibaya tu kwa ajili ya dhambi na kumwomba Mungu msamaha. Ni kugeuka na kuacha hiyo dhambi, na kumgeukia Mungu. Wale wanaoendelea katika dhambi hawajatubu, ingawa wanaweza kuwa walitafuta msamaha. Toba ni pamoja na kuiacha dhambi, kugeuka mbali nayo, kufanya kila kinachowezekana ili kutoirudia. Hii haiwezekani na dhambi tarajiwa – maana hata hazijafanywa!

 

Ni rahisi kuona sababu ya msamaha wa dhambi tarajiwa kuwa muhimu sana kwa wapinga sheria na wale wenye kufuata itikadi ya usalama wa wokovu milele bila masharti. Kwa kuwa wanaamini kwamba wanachohitaji tu ni muda mfupi wa kuamini ili waweze kuwa salama milele, waliunda fundisho ambalo litashughulika na dhambi za baadaye. Dkt. Stanley anasema hakuna dhambi ya baadaye itakayoharibu wokovu wa mtu, kama aliwahi kuokoka. Hili fundisho la uongo linawezeshwa kwa kudai kwamba wakati mtu akisha tubu mara moja tu dhambi, za zamani na dhambi tarajiwa zimekwisha samehewa.

 

Bila shaka unaona jinsi ambavyo fundisho moja la uongo linavyoelekea kwenye mengine mengi ya uongo pia.

 

Kutokana na kujua unachojua sasa kuhusu umuhimu wa haki, unaweza kuona jinsi Shetani anavyopata njia za kupinga haki kwa kuingia kanisani na kupenyeza itikadi za uongo zinazofundisha kwamba kuwa na haki si kitu cha lazima, au zaidi, kwamba ni kitu kisichowezekana, au zaidi sana, kwamba haki yetu huja kwa njia ya Yesu tu – nayo ni ya kuhesabiwa, wala haihusiki hata kidogo na haki yetu binafsi. Tafiti zinaonyesha kwamba wengi wanaojiita Wakristo wanaishi kiovu (yaani, pasipo haki) kama tu wale walio duniani, ambao hawasemi wana imani yoyote.

 

Mdanganyifu mkuu siku zote anajaribu kuwadanganya wale wanaotaka kuwa wafuasi wa kweli na wanafunzi wa Bwana Yesu. Anawataka wao kuamini uongo kwamba haki binafsi haiathiri wokovu wa mtu. Anataka wafuate njia za uovu na kutokuwa na haki, ili wawe wafuasi wake – watoto wa Ibilisi. Mara nyingi sana, hayo ndiyo ambayo yametokea.

 

Warumi Sura Ya Saba Kueleweka Vibaya.

 

Miaka mingi iliyopita nilipokuwa mwamini mchanga, baadhi tulikuwa tunakwenda kupata kifungua kinywa baada ya ibada. Nikazusha swala la haja ya haki. Haraka sana niliambiwa hivi: “Sisi hatuwezi kuwa wenye haki. Tunatenda dhambi mara mia nyingi sana kwa siku. Tunachotakiwa kufanya ni kumwomba Mungu atusamehe. Hata Paulo aliendelea kufanya dhambi. Je, sisi ni bora kuliko Paulo?”

 

Nilikuwa najua tayari kuhusu 1Yohana 3:6, kwamba, “Hakuna yeyote akaaye ndani yake anaye-endelea kutenda hambi. Hakuna yeyote anaye-endelea katika dhambi ambaye amemwona wala kumjua” (TLR). Sikukubaliana na itikio hilo. Nikaona kwamba mtu huyo (aliyejibu) hakuelewa vizuri. Yeye alikuwa anasema juu ya Warumi 7:14-24, mahali ambapo Paulo anasema,

 

“Kwa maana twajua ya kuwa Torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi. Maana sijuli nilifanyalo: kwa sababu lile nilipendalo silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. … Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu, halikai neno jema. Kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu” (Warumi 7:14-20)

 

Nikajiuliza kama hiyo ndiyo maana ya Petro alipoandika hivi kuhusu barua za Paulo: “ … barua zake zina mambo magumu kuelewa, ambayo, watu wasio na akili na wasio na msimamo huyapotosha, kama wanavyofanya Maandiko mengine pia, kwa uharibifu wao” (2Petro 3:16, TLR).

 

Nikajua kwamba hilo si ungamo la Paulo, kwamba yeye kama Mkristo alikuwa ameuzwa kuwa mtumwa wa dhambi. Katika Warumi 6:15-18, Paulo alifafanua tofauti kabisa.

 

“Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha! Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki. Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki”.

 

Mbona Maandiko haya ni tofauti kabisa! Hili la mwisho linakubaliana na kila kitu ambacho tumeona kuhusu wito wa Yesu kwa habari ya haki, na hukumu kwa wale walio watumwa wa dhambi. Hapa, Paulo anasema tunapaswa kuwa watumwa kwa kutii, kitu kinachopelekea haki. Halafu anawaambia wale wanaopokea barua yake kwamba, “Ninyi mmewekwa huru na dhambi na kuwa watumwa wa haki.” Si Paulo hapo nyuma alisema kwamba yeye hakuwa mtu wa kiroho, na kwamba alikuwa ameuzwa dhambini kama mtumwa?

 

Tatizo liko kwenye matumizi ya neno kitendo. Katika Andiko la Warumi sura ya saba, Paulo anatumia maneno tendo ya wakati uliopo, yanayoonyesha kana kwamba yuko katika hilo hiyo wakati huo. Hebu tutazame kwa ukaribu zaidi. Katika Fahirisi ya Young’s Literal Translation of the Holy Bible, mfasiri anatuambia kuhusu kanuni tunayopaswa kuelewa juu ya waandishi wa Kiebrania. Anasema hivi:

 

Waebrania wanaposema kuhusu matukio ambayo huenda yakawa ni ya zamani au wakati ujao, walizoea kutumia kanuni ya kujihamisha wenyewe kiakili hadi kipindi na mahali pa tukio husika, na hawakuridhika na kutazama matukio hayo bila ya kujali, kana kwamba ni ya wakati uliokwisha pita au unaokuja baadaye. Ndiyo sababu ya matumizi mengi ya maneno ya wakati uliopo (maneno mepesi ni ili kutilia mkazo).

 

Hivyo ndivyo Paulo alivyofanya. Yeye alitumia maneno tendo ya wakati uliopo ili kueleza hali yake kabla hajamjia Kristo. Kwa kuwa katika utamaduni wetu wa Magharibi hatuandiki wala kuzungumza hivyo, mistari hiyo imeleta vurugu sana. Lakini tukisha tambua hilo, andiko hilo linaeleweka kwa urahisi kabisa. Paulo alikuwa anazungumza juu yake mwenyewe kabla ya kumwamini Kristo. Kabla hajamjua Bwana Yesu, Paulo alisema hivi juu yake: “Ole wangu, maskini mimi! Nani atakayenikomboa na mwili huu wa kifo?” (Warumi 7:24, TLR). Lakini anajibu swali lake mwenyewe katika mstari unaofuata, kwamba: “Ashukuriwe Mungu – kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu!”

 

Katika Warumi 8:1-2, Paulo anatoa ufumbuzi kwa tatizo alilolitaja katika Sura ya Saba, hivi: “Sasa basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu, sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.”

 

Kuna ushahidi wa zaidi kwamba andiko la Warumi sura ya saba lisingekuwa linazungumzia hali ya Paulo akiwa anamfuata Bwana Yesu. Paulo alieleza maisha yake mbele ya waaminio, hivi: Kwamba alikuwa na “dhamiri safi” (2Timotheo 1:3); kwamba “amevipiga vita vile vizuri … amemaliza mwendo … ameitunza imani” (2Timotheo 4:7, TLR). Alisema pia, “Ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa utakatifu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu, si kwa hekima ya mwili bali kwa neema ya Mungu, tulienenda katika dunia, na hasa kwenu ninyi” (2Wakor. 1:12). “… Hatukumdhulumu mtu yeyote, wala kumharibu mtu, wala kumkaramkia mtu” (2Wakor. 7:2).

 

Paulo alijitoa kama mfano wa kufuatwa hata na wengine. “Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo” (Wafilipi 4:9). “Ndugu nawasihi, mwe kama mimi” (Wagalatia 4:12, TLR). “Nawahimiza mniige mimi” (1Wakor. 4:16, TLR). “Uliyoyasikia kwangu yaweke kama mfano wa mafundisho sahihi” (2Timotheo 1:13, TLR). “Ndugu, jiungeni na wengine katika kufuata mfano wangu” (Wafilipi 3:17, TLR). “Mwajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata. Kwa sababu hatukutenda bila utaratibu kwenu, wala hatukula chakula kwa mtu yeyote bure; bali kwa taabu na masumbufu, usiku na mchana tulitenda kazi, ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote. Si kwamba hatuna amri, lakini makusudi tufanye nafsi zetu kuwa kielelezo kwenu, mtufuate” (2Wathes. 3:7-9). Anayoandika Paulo yanakubaliana na tafsiri hizi zote.

 

Basi, haishangazi kwamba wapinga sheria na wale wenye kuamini kuhusu usalama wa wokovu milele bila masharti watajaribu kutafuta faraja katika tafsiri isiyo sahihi ya Maandiko hayo. Wanajua vizuri sana kwamba wanaishi dhambini; wanataka ule uhakikisho kwamba Mtume Paulo pia aliishi dhambi. Kama aliishi, wao bila shaka wako sawa katika maisha yao ya dhambi na katika tafsiri yao potofu ya Maandiko.

 

Kwa maelezo kamili zaidi kuhusu Warumi sura ya Saba, tafadhali soma makala yangu iitwayo “Romans 7 Revisited” katika tovuti ya www.bereanpublishers.com |tafuta “False Doctrines”| halafu tafuta “Misunderstood”| halafu tafuta “Romans 7 Revisited”.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sura Ya Kumi Na Moja

(Chapter 11)

 

Tubu, Badilika, na Ufundishe!

(Repent, Change, and Teach!)

 

Katika makala iitwayo “A Shocking ‘Confession’ from Willow Creek Community Church” (yaani, Ukiri Unaoshtua kutoka Kanisa la Willow Creek Community), ya tarehe 30 Oktoba mwaka 2007, Bob Burney alitaarifu kwamba hilo kanisa kubwa sana lilitoa matokeo ya utafiti uliofanyika katika kipindi cha miaka kadhaa juu ya mafanikio ya mipango yao na falsafa ya huduma. Matokeo ya utafiti huyo yamo katika kitabu kilichotolewa hivi karibuni kinachoitwa “Reveal: Where Are You?” kilichoandikwa kwa ushirikiano wa watu wawili: Cally Parkinson na Greg Hawkins, ambaye ni mchungaji mtendaji wa hilo Kanisa la Willow Creek Community. Mchungaji kiongozi Hybels mwenyewe aliyaita matokeo ya utafiti huo kuwa “yanayotikisa dunia”, na “yanayoshangaza akili”. Wala si ajabu: inaonekana “wataalamu” wao walikuwa na makosa.

 

Taarifa hiyo inadhihirisha kwamba mengi ambayo wamekuwa wakifanya kwa miaka mingi, na mambo ambayo wamefundisha mamilioni ya watu kufanya hayajasababisha wanafunzi imara wa Yesu Kristo. Wanaongeza idadi ya wafuasi wao, lakini si idadi ya wanafunzi. Tena, mambo yanazidi kuharibika. Hybels analalamika hivi:

 

“Baadhi ya mambo ambayo tumetia mamilioni ya dola ndani yake tukifikiri kwamba yangewasaidia watu wetu kweli kweli kukua na kuendelea mbele kiroho, yalipotafitiwa na majibu kurudishwa, imeonekana kwamba hayakuwa yanawasaidia watu kiasi hicho. Mambo mengine ambayo hatukutia fedha nyingi ndani yake, wala kuwa na watenda kazi wengi juu yake, ndiyo mambo ambayo watu wetu wanayalilia na kuyataka.”

 

Ni hivi: Ukitaka kundi kubwa la watu, ule mfumo wa kanisa “lenye kujali watafutaji” huleta matokeo. Lakini, ukitaka wafuasi wa Kristo ambao ni thabiti, wa kweli, waliokomaa, mfumo huo haufai hata kidogo. Katika ukiri mwingine unaoshtua sana, Hybels anasema hivi:

 

“Tulikosea. Tulichotakiwa kufanya wakati watu walipovuka mstari wa imani na kuwa Wakristo ni kwamba, tungeanza kuwaambia watu na kuwafundisha kwamba wanahitaji kuwajibika ili kuwa ‘wanaojilisha wenyewe’. Tungepata watu, tuwafundishe jinsi ya kusoma Biblia zao wakiwa wanasubiri ibada, na jinsi ya kufanya mambo ya kiroho kwa bidii zaidi wao wenyewe.”

 

Cha ajabu ni kwamba, huyo ‘bingwa’ wa kukua kwa kanisa sasa anatuambia kwamba watu wanahitaji kujisomea Biblia zao na kuwajibika kwa ajili ya kukua kiroho kwao.

Tovuti moja iitwayo “Out of Ur” (Kutoka Uri) ilitoa maoni yake kuhusu mambo hayo hayo na kusema hivi:

 

“Maana yake ni kwamba, kukua kwa kiroho hakufanyiki vizuri kwa kutegemea mipango ya hali ya juu sana, bali kwa njia ya mazoezi ya tangu kale ya kiroho, yaani maombi, kusoma Biblia, na mahusiano. Halafu – cha ajabu – hayo mazoezi ya msingi kabisa wala hayahitaji majengo ya gharama kubwa na watumishi mia nyingi kuyasimamia.”

 

Je, huu ni mwanzo wa kumalizika kwa ushawishi wa Kanisa la Willow Creek juu ya mambo ya kiroho Marekani? Hapana. Hawkins anasema hivi:

 

“Ndoto yetu ni kwamba, tubadilishe kabisa msingi wa jinsi tunavyoendesha kanisa. Kwamba tuchukue karatasi safi mpya, na kufikiri upya mawzo yetu ya zamani. Tubadilishe na kuweka mtazamo mpya. Mitazamo hiyo iwe imetafitiwa vizuri na kuwekwa msingi katika Maandiko. Ndoto yetu ni kujaribu kugundua kweli kweli kile ambacho Mungu anafanya, na jinsi anavyotutaka sisi tuibadilishe sayari hii.”

 

Je, ni ajabu kwamba makumi elfu ya dola yaliyotumiwa katika mipango hayasababishi wanafunzi kuwepo? Isiwe ajabu. Yesu alituambia tufanye watu kuwa wanafunzi kwa kuwafundisha kuyatii yote ambayo Yeye aliamuru. Bill Hybels na Kanisa la Willow Creek Community hawajajifunza bado. Sasa wanafikiri kwamba njia waliyopaswa kupitia ni kuwafanya watu wasome Biblia zao wakisubiri ibada na kufundishwa jinsi ya kufanya mazoezi ya kiroho [sijui ni nini hicho] wao wenyewe.

 

Watoa maoni pamoja na Greg Hawkins wameshindwa kuona kitu halisi. Ajabu ni kwamba, baada ya kutumia hekima ya binadamu miaka hiyo yote na kushindwa, wanakusudia kufutilia mbali kila kitu na kufikiri upya mambo waliyoyawaza zamani. Mbona inasikitisha tu? Kwa nini wasisome Mathayo 28:18-20 waone Mkuu wa Kanisa aliwaamuru wafanye nini ili kuwa na wanafunzi?

 

Kama wewe ni mchungaji au mwalimu ambaye ameshindwa au kukataa kufanya watu kuwa wanafunzi kwa kuwafundisha kuyatii yote ambayo Yesu aliamuru, unatakiwa kutubu tabia yako hiyo ya kuasi ambayo ni dhambi. Maandiko yako wazi kabisa juu ya kinachotokea kwa wale wanaoendelea kufanya dhambi kwa makusudi.

 

“Tukiendelea kufanya dhambi makusudi baada ya kupokea maarifa ya kweli, hakuna dhabihu ya dhambi iliyobaki tena, bali kuna kutazamia kwa kutisha sana hukumu na moto mkali ambao utawaangamiza adui wa Mungu” (Waebrania 10:26-27, TLR).

 

Kama ulikuwa hujui ukweli kabla ya hapa, sasa unaujua. Huna cha kujitetea ukiendelea katika tabia hiyo ya uasi.

 

Hakuna swala lingine muhimu kuliko hili sasa hivi katika Ukristo. Watu wanaohudhuria makanisani mwetu wanapitia ukame wa Neno la Mungu. Walikuja kusikia habari za Mungu, jinsi wanavyoweza kumpendeza, na jinsi wanavyoweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Badala yake, mara nyingi sana, wanapewa injili ya uongo ambayo haiwezi na haitawakoa. Kama hujawafundisha wale walio chini ya uangalizi wako kutii mafundisho na amri za Bwana Yesu, umekuwa ukifundisha injili ya uongo. Hakuna Injili nyingine ambayo watu wanapaswa kuitumia ili kuokoka. Paulo alitoa onyo lifuatalo:

 

“Yeye atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na wasioitii injili ya Bwana wetu Yesu. Wataadhibiwa kwa uharibifu wa milele na kwa kufungiwa nje ya uwepo wa Bwana, na utukufu wa uwezo wake” (2Wathes. 1:8-9, TLR).

 

Mungu anataka sisi sote tubadilike na kulitii Neno Lake, kama Bwana Yesu alivyotuambia. Kitabu hiki ni wito kwamba tutii agizo la Yesu la kuwafanya watu kuwa wanafunzi kwa “kuwafundisha kuyatii yote niliyowaamuru ninyi” (Mathayo 28:20, TLR). Unaweza kubadilika, lakini lazima uwe na ujasiri wa kumfuata Mungu, si wanadamu. Wote mara nyingi tumefanya mambo ambayo hayajampendeza Mungu – wakati mwingi hatukuwa tunatambua uzito wa dhambi yetu. Tusipotubu na kubadilika, tutahukumiwa vikali sana (Yakobo 3:1).

 

Moyo wangu unawalilia mamilioni ya watu wanaohudhuria ibada katika makanisa yasiyohubiri Injili ya Bwana wetu Yesu, ambao wanaweza kujitolea sana kwa habari ya muda wao na hazina zao, lakini wanaelekea jehanamu wote kwa sababu hawatii yale mafundisho na amri za Yesu zinazosema kwamba, bila ya wao kufanya kitu fulani (au kuacha kufanya kitu fulani), hawataingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

 

Wakati mafundisho na amri za Yesu zinapofundishwa kama Yesu alivyoagiza, watu wengi humjua Mungu na kwa hiari yao wenyewe hutafuta kuitii Injili ya Bwana wetu Yesu, kama wanafunzi Wake.

 

Sasa – utafanyaje hayo? Kwanza, unaweza kutumia masomo ya Biblia kuhusu Mafundisho na Amri za Yesu ambayo nimeandika na kufundisha katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Yote yanapatikana katika tovuti hii: www.bereanpblishers.com | tafuta “Bible Study”. Jina la masomo hayo ni hili: “KNOWING AND LOVING GOD Through Learning And Obeying The Teachings And Commands Of Jesus.”

 

Kwa mara ya kwanza, niliandika na kufundisha mafundisho na amri za Yesu huko New Zealand. Ilikuwa kazi kiasi. Japo ilikuwa rahisi kwangu kufundisha, kwa wengine ingekuwa shida kidogo. Kwa miaka minne na nusu nilifanikiwa kufika katikati ya Injili ya Luka tu.

 

Tuliporudi Marekani, niliandika upya mafunzo hayo. Nikatilia mkazo kuyafanya kuwa mafunzo ambayo hayakuwa na haja ya mwalimu mjuzi wa Biblia. Hivi karibuni nilifundisha tena toleo hilo jipya la masomo kwa mara ya kwanza. Nilifurahi sana kuona mabadiliko yaliyotokea katika majuma 43 tu ya mafunzo, ukilinganisha na ile miaka minne na nusu niliyofundisha huko New Zealand. Si kwamba masomo yangu ndiyo yanayohusika katika kubadilisha maisha kulikotokea, ni maneno ya Yesu. Maneno Yake kweli ni roho na ni uzima!

 

Pengine sasa unafikiri, “Aha! Sasa tumegundua aliandika hiki kitabu ili kupigia debe masomo yake ya Biblia!” Sikulaumu kama utafikiri hivyo, ukizingatia kwamba Injili siku hizi imekuwa biashara kubwa.

 

Sasa hebu shangaa: haya masomo kwenye tovuti ni ya BURE KABISA! Hakuna gharama yoyote kuyatumia! Utakachohitaji ni kuyatoa mwenyewe kwenye mtandao na kuchapisha kiasi chochote unachotaka.

 

Masomo yenyewe yamegawanywa katika Sehemu Nne za majuma 12, 13, 12 tena na matano. Yamegawanywa hivyo ili iwe rahisi kupumzika katikati ya sehemu, kama ukitaka. Hapa katika jangwa la Arizona huwa tunapumzika kidogo wakati wa joto kali la majira ya kiangazi kwa sababu watu wengi huondoka kwenda kutafuta maeneo baridi kidogo.

 

Sehemu tatu za kwanza ni mafundisho yote na amri za Yesu, bila kurudiwa. Injili inarudia-rudia mambo mengi sana. Hoja yaweza kutolewa kwamba Mungu hutumia mtindo wa marudio ili kuhakikisha kwamba mafundisho fulani na amri fulani vinapata kuangaliwa kwa makini zaidi. Lakini, mimi nilitaka kuhakikisha kwamba kila mtu atapata nafasi ya kujifunza mafundisho yote na amri zote kwa haraka iwezekanavyo. Marudio yangechelewesha hilo.

 

Kuna vichwa 382 tofauti katika zile sehemu tatu za kwanza. Kila kichwa kina fundisho moja au amri moja. Sehemu ya Nne ina vichwa 80 tofauti, vyenye kurudia mafundisho na amri za Yesu, yaliyo dhahiri kabisa kwamba yanahusiana na wokovu – yale yenye kutaja au kuonyesha kwamba lazima kuyatii ili kupata wokovu.

 

Nitakushirikisha pia baadhi ya mbinu ninazotumia kufundisha kwa ufanisi. Pengine hizo pia zitakuwa msaada kwako. Mimi huchapisha nakala kiasi fulani kwa ajili ya masomo manne ya kila juma kwa mara moja. Ninachapisha nakala zaidi kadiri watu wanavyojiunga na kundi. Ni rahisi sana kurekebisha idadi ya nakala zinazohitajika kila majuma manne. Ninatengeneza za ziada kwa ajili ya watu wanaoweza kujiunga baada ya kuchapishwa kwa nakala zangu.

 

Halafu, ninanunua madaftari yanayofanana. Ninachomeka majalada ya yale masomo katika madaftari hayo, ili kusaidia kutambua ni somo gani. Majalada yanaweza kupatikana na kuchapishwa ukiingia kwenye tovuti hii: www.bereanpublishers.com |tafuta ‘Bible Study”.

 

Watu kumi hadi ishirini walihudhuria masomo mawili ya mwisho. Makundi ya ukubwa huo yanafaa zaidi kwa sababu watu wanaondoa hofu ya kushiriki. Kundi moja lilikuwa na watu zaidi ya ishirini, na likawa zuri tu.

 

Mimi huendesha mafunzo hayo kwa njia ya ajabu sana. Wanafunzi wana siku tano za kazi ya nyumbani, ambayo ni rahisi tu: kujaza sehemu zilizo wazi, kuchagua majibu, na kadhalika. Hiyo kazi wanayofanyia nyumbani lazima ikamilishwe kabla ya kikao kinachofuata. Mafunzo yetu ya kila juma hudumu kwa muda wa saa moja na nusu tu. Sisi tunaanza saa moja kamili jioni. Ninamwomba mwanafunzi mmoja afungue kipindi kwa sala. Tunakaa karibu karibu (katika mduara labda) ili iwe rahisi kusikilizana vizuri. Halafu tunaanza kusoma yale maelezo tuliyopitia juma zima. Kila mtu anasoma isipokuwa mimi, na wale ambao hawajakamilisha kazi yao ya nyumbani (japo si mara nyingi utakuta mtu hajakamilisha). Wanafunzi wanaruhusiwa kuingilia wakati wowote kama kuna swali au hoja ya kuchangia. Mimi mwenyewe ninaingilia kati hapa na pale kuongezea kitu au kuweka jambo wazi. Ninagawanya usomaji ili kila mwanafunzi asome nusu ukurasa hadi ukurasa mzima. Halafu tunafunga kwa maombi kama saa mbili unusu hivi jioni.

 

Katika kipindi kimoja wanafunzi walijadili juu ya masomo baada ya kipindi. Nilishangaa sana kuwasikia wakisema kwamba walifurahia kuifanya ile kazi ya nyumbani. Wakasema, sehemu iliyokuwa ngumu ni kumaliza baada ya kazi ya siku moja. Mara nyingi walitaka kuendelea. Nimewaagiza waendelee kwa utaratibu wa siku moja moja ili waweze kuelewa vizuri kile walichojifunza, na waweze kukifanyia kazi.

 

Kukawa na mambo ya kusisimua sana katika vipindi vya somo lililopita. Wanafunzi walipotambua umuhimu wa kile walichokuwa wanajifunza, walishauri kwamba kila mtu aliyeko kanisani ahusike katika masomo hayo, pamoja na wachungaji. Waliamini kwamba yangebadilisha kanisa, kama yalivyowabadilisha wao.

 

Tumebarikiwa kwamba mchungaji wetu, Trent Renner, anahubiri mafundisho na amri za Yesu – licha ya kuonywa kwamba itakuwa kosa kubwa. Wengi walimwambia kwamba hawezi kufundisha somo kwa zaidi ya majuma kati ya manne hadi nane maana watu watachoka. Mchungaji Trent aliamini kwamba somo hilo ni muhimu, naye akapuuza maonyo hayo. Hivi karibuni amemaliza mwaka wake wa kwanza – kama majuma 50 – akiwa anahubiri juu ya mafundisho na amri za Yesu. Ninapoandika kitabu hiki, amefikia Mathayo sura ya 14. Kwa mara ya kwanza, kanisa liliendelea kukua hata katika majira ya kiangazi ambapo ni joto sana. Mchungaji Trent alinitumia barua pepe aliyopokea toka kwa mchungaji mmoja aliyetumiwa masomo hayo. “Nashukuru tena kwa kunitumia masomo ya Ndugu Bernie mwaka jana. Nilianza kuhubiri masomo hayo Desemba, na mambo yanakwenda vizuri sana. Nadhani masomo haya yatakuwa na matokeo ya kudumu.”

 

Kweli napendekeza kwamba kila mtu ajifunze masomo hayo. Yanaweza kutumika kwa mikutano ya nyumba kwa nyumba, kwa ajili ya makundi ya vijana, makundi ya watu wazima, na kadhalika. Unaweza kuaokoa watu wengi wasiohesabika wasiende jehanamu milele kwa kufundisha. Kila mtu asiyejifunza kutii mafundisho na amri za Yesu kutoka kwetu ni mtu mwingine ambaye hataweza kuingia katika ufalme wa Mungu. Wanaweza wasitende mapenzi ya Mungu kwa sababu hawajui mapenzi ya Mungu.

 

Ukiamua kuhubiri mafundisho na amri za Yesu, kujifunza hili somo kunaweza kuwa msaada kwako pia, kwa sababu mara nyingi linatoa maandiko ya ziada yanayosaidia kufafanua fundisho fulani au amri fulani.

 

Tena, watu waliojifunza Mafundisho na Amri watakuwa wenye kukuunga mkono sana.

 

Hitimisho

 

Tunahitimisha kitabu hiki kwa onyo la Bwana wetu Yesu, ambalo umelisoma mara nyingi sana.

           

“Si kila mtu aniambiaye: ‘Bwana! Bwana!’ atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 7:21).

 

Mafundisho na amri za Yesu ni mapenzi ya Mungu. Kazi yako na yangu ni kufanya kila tunachoweza ili kuwasaidia watu wajue mapenzi ya Mungu kwa kuwafundisha kuyatii mafundisho ya Yesu na amri Zake, kama ambavyo Yesu alituagiza katika Mathayo 28:18-20. Yaliyobaki ni juu ya Mungu Mwenyewe.

 

Mungu akubariki katika juhudi zako za kumtii Bwana Yesu na kupanua ufalme Wake unapojifunza na kufundisha amri Zake.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


 

[1] Stanley, Charles, katika Eternal Security: Can You Be Sure? (Kimechapishwa Nashville, TN na Oliver Nelson, 1990).

[2] Stanley, Charles, katika kanda iitwayo “Eternal Security: What Do We Have To Lose?” Namba 6, MI090.

[3] Kitabu kilichotajwa hapo nyuma, ukurasa wa 70.

[4] Kitabu kilichotajwa hapo nyuma, ukurasa 79 hadi 80.

[5] Kitabu kilichotajwa hapo nyuma, ukurasa wa 74.

[6] Kitabu kilichotajwa hapo nyuma, ukurasa wa 93.

[7] Kitabu kinachotajwa hapo nyuma, ukurasa wa 94.

[8] Ili kupata mjadala kamili unaopinga fundisho hili la usalama wa wokovu milele bila masharti, tembelea tovuti ya www.bereanpublishers.co.nz, False Doctrines, “Is the Believer Eternally Secure?”

[9] Hoja Yangu namba 6, ukurasa wa 80.

[10] Kitabu kinachotajwa hapo nyuma, ukurasa wa 81.

[11] Kitabu kinachotajwa hapo nyuma, ukurasa wa 94.

[12] Kitabu kilichotajwa hapo nyuma, ukurasa wa 121.

[13] Kitabu kilichotajwa hapo nyuma, ukurasa wa 71.

[14] 2Petro 3:17

[15] Kitabu kilichotajwa hapo nyuma, ukurasa wa 79-80.